Muhtasari wa kilimo cha baadhi ya mazao jamii ya kunde

Muhtasari wa kilimo cha baadhi ya mazao jamii ya kunde

Wakuu habari za jioni.

Kuna mteja wangu anahitaji kununua dengu na mbaazi tani 50 kila zao kuanzia mwezi wa tatu.

Naomba kujuzwa wapi naweza kupata dengu na pia mbaazi kwa wingi kipindi hiki, bei ikoje Kwa kilo na msimu wa mazao haya ni miezi ipi katika mikoa ipi.

Shukrani kwa ushirikiano.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mimi niko maeneo ya kilimo cha mbaazi na dengu huku manyara. Kama uko serious mda wa mavuno ya dengu na mbaazi unaendana ni kuanzia mwezi wa 7&8. Bei ya dengu mara nyingi huanzia 800 kwa kilo alafu mbaazi huanzia 500 kwa kilo na bei huweza kubadilika kutokana na uhitaji.

Mimi nipo wilaya ya Hanang na ninajishungulisha na biashara ya mazao. Kama unaona nitakufaa njoo tupige hiyo kazi zaidi tupeane mawasiliano kwa details zaidi
 
Mkuu nakutafuta mwezi wa nne nikiwa nakuja kupanda dengu. mie nina eneo hapo galapo but lipo mpakani na domu kama heka 25 za kulima dengu. pia store kuna mzigo wangu nasubiri bei ichanganye niuze
Mkuu mimi niko maeneo ya kilimo cha mbaazi na dengu huku manyara. Kama uko serious mda wa mavuno ya dengu na mbaazi unaendana ni kuanzia mwezi wa 7&8. Bei ya dengu mara nyingi huanzia 800 kwa kilo alafu mbaazi huanzia 500 kwa kilo na bei huweza kubadilika kutokana na uhitaji.

Mimi nipo wilaya ya Hanang na ninajishungulisha na biashara ya mazao. Kama unaona nitakufaa njoo tupige hiyo kazi zaidi tupeane mawasiliano kwa details zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dengu na mbaazi mpaka miezi ya nane na tisa,mwezi machi huwezi pata hayo mazao njoo wilaya ya Hanang miezi hiyo utapata mzigo wa kutosha.
 
Wakuu habari za jioni.

Kuna mteja wangu anahitaji kununua dengu na mbaazi tani 50 kila zao kuanzia mwezi wa tatu.

Naomba kujuzwa wapi naweza kupata dengu na pia mbaazi kwa wingi kipindi hiki, bei ikoje Kwa kilo na msimu wa mazao haya ni miezi ipi katika mikoa ipi.

Shukrani kwa ushirikiano.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkoani simiyu dengu na mbaazi utazipata kuanzia mwezi wa nane maana dengu inapandwa mwezi wa tano. bei zinatofautiana kulingana na msimu, wanunuzi ndio wanakuja na bei zao uhitaji ukiongezeka na bei zinapanda. ukija na bei nzuri tani 50 unajaza kwa wiki moja.
 
Kilimo cha zao la Choroko

Choroko ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini na madini ya phosphorus na calicium. Zao hili likilimwa vizuri hutoa mavuno kati ya Kg 400 hadi 900 kwa ekari.

Udongo na hali ya hewa
Choroko hustawi katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji. Hulimwa kutoka mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari japokuwa kuna mbegu nyingine zinaweza kukubali zaidi ya ukanda huu.Hili ni zao linalostahimili ukame.

Aina za Choroko
Kuna aina kuu mbili za choroko ambazo pia zimegawanyika katika makundi mawili,choroko nyeusi na choroko za kijani.

A) Choroko zinazotambaa, hizi ni choroko ambazo zinarefuka sana na hutambaa sehemu mbalimbali.

B) Choroko zinazosimama, hizi ni choroko ambazo zinakuwa kwa kusimama kwenda juu.

Kipindi kizuri cha upandaji wa choroko
Choroko hazihitaji maji mengi hivyo ni budi zipandwe mwishoni mwa msimu wa mvua,Pia zinaweza kupandwa katika shamba lililolimwa mpunga.

Nafasi cha upandaji wa choroko na kiasi cha mbegu
Choroko huitaji mbegu kiasi cha kilogram 8 hadi kumi kwa ekari moja.

Panda choroko zako kwa nafasi ya sentimeta 30 mastari na mstari na sentimeta 10 shina hadi shina (30 x10 )sentimeta au (40 x 8 )sentimeta

Samadi na mbolea ya viwanda
Kama shmba lako halina rutuba ya kutosha unaweza kuongeza samadi kiasi cha tani tano kwa ekari na pia unaweza kupanda kwa kutumia mbolea ya NPK kg 50 kwa ekari.weka mbolea zote kabla ya kupanda.

Umwagiliaji
Kama umepanda kipindi cha ukame sana au unalima kilimo cha umwagiliaji basi mwagilia shamba lako upate unyevu wa kuotesha mbegu, kisha baada ya mbegu kuota kaa siku 6 hadi 10 na umawgilie tena. Mara tatu za kumwagilia zinatosha kwa choroko. Na palilia shamba lako mapema kuzuia magugu kuota ndani ya shamba lako na kwa palizi moja inaweza kutosha.

Magonjwa ya Choroko
1-yellow mosaic virus ( Ugonjwa wa manjano)

Dalili- mmea unakuwa wa njano na madoa ya njano katika majani.

Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimili magonjwa.

2-Powdery Mildew (Ukungu)
Dalili-Majani yanakuwa na vidoti vya njano ambavyo vinabadilika kuwa vya kahawia au kijivu haraka na ambapo kunakuwa na unga unga katika majani.

Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimili ukungu,Pulizia dawa za ukungu (Fungicide).

anza kupuliza wiki tatu baada ya mimea kuota na kuendelea kulingana na hali halisi.

3-Leaf spot (Vidoti katika majani)
Dalili-majani yanakuwa na vidoti vya mviringo na visivyo na umbo maalum ambapo katikati yanakuwa na rangi rangi ya kijivu na weupe na mistari ya rangi ya wekundu-kahawia au nyeusi-kahawia.ugonjwa huu husababisha hasara hadi ya asilimia 58 ya mapato.

Kinga na Tiba-Panda mbegu inayostahimili ugonjwa huu,Choma mabaki ya mimea hii na ile ya jamii moja baada ya kuvuna.Pulizia dawa za ukungu (Fungicide) Katika nafasi ya wiki mbili mbili kama eneo hilom linashambuliwa mara kwa mara na ukungu.

Wadudu
Kuna wadudu mbalimbali wanaoshambulia choroko kama vile aphidi,funza wa vitumba,nzi wa maharage.Wazui wadudu hawa kwa kupuliza dawa za wadudu mara tu baada ya mimea kuota,dawa kama karate,twigathoate,dimethote na nyinginezo zinaweza kutumika.

Uvunaji
Mara tuu choroko zinapofikia asilimia 85 ya ukaukaji zinabidi zivunwe ukichelewa zitapukutikia shambani.
 
Kilimo cha Njegere

Mara nyingi huwa napenda kula ubwabwa na njegere, sijui kama na wewe mwenzangu unapenda kula njegere? Kama jibu ndiyo basi nakusihi uungane nami katika makala haya ili uweze kujifunza namna ya kulima kilimo hiki.

Nakusihi kulima kilimo hiki kwa kwa sababu , kilimo cha njegere ni kilimo chenye tija kwa wakulima. Njegere ni mbegu za spishi za mimea katika jamii ya kunde ambayo hukuzwa sehemu mbalimbali duniani katika maeneo ya ukanda wa juu.

Spishi kadhaa za njegere ni:
1. Njegere kubwa (chickpea)
2. Njegere ya kizungu (common pea)
3. Njegere sukari (snow pea and snap pea)

Hapa nchini Tanzania njegere hulimwa nyanda za juu kusini, nyanda za juu kaskazini na kwenye miinuko ya Usambara na Uluguru. Katika ulimwengu njegere hulimwa kwa wingi katika Asia ya kati, Mediterania na Afrika ya kaskazini.
Kuna aina mbalimbali za njegere zinazopatikana Tanzania kama Tanganyika yellow, Idaho white, Rondo na Mbegu za kienyeji.

HALI YA HEWA:
Kwa tafiti inaonesha zao la njegere hustawi vizuri maeneo yenye hali ya ubaridi wa sentigredi 17 – 21 C, na mwinuko zaidi ya mita 1200 usawa wa bahari na mvua, unyevu wa kutosha na maji yasiyotuama. Udongo uliowekwa mbolea, kulimwa kwa kina na wenye tindikali ya PH 5.5 – 6.5.

UTAYARISHAJI WA SHAMBA:

Maandalizi yanatakiwa yaanze kabla msimu wa mvua haanza, Shamba / bustani itayarishwe kwa trekta au pawatila au jembe la mkono au jembe la ng’ombe kwa kufuata mahitaji ya udongo kama kutotuamisha maji, kulimwa kwa kina. Changanya mbolea za asili (samadi au mboji) na udongo ili kurutubisha ardhi.

UTAYARISHAJI WA MBEGU
Chambua mbegu nzuri zinazoonekana hazina matatizo, zilizo na afya ili kupata mazao mengi. Unashauriwa kuandaa mbegu mapema ili kuweka maandalizi mazuri.

UPANDAJI
Njegere hupandwa kipindi cha mvua ama kwa umwagiliziaji, maana udongo unatakiwa uwe na unyevu ili kufanya mmea kukua vyema, nafasi za kupanda:-

i) 60 sm – 90 sm x 5.7 sentimita kwa mbegu fupi.
ii) 12 sm – 15 sm x 5 – 7.5 sentimita katika safu mbili za sentimita 90 kwa mbegu inayotambaa.
iii) Njegere hustawi vizuri zikipata sehemu za kutambalia.
iv) Mbegu ya njegere huota baada ya siku 7 – 10.

MBOLEA
Ukitumia mbolea za asili (samadi au Mboji) njegere hustawi vizuri. Katika kipindi cha ukuaji ni muhimu kuweka mbolea ya chumvichumvi za nitrogen kwa kipimo cha kg 40 kwa hekari.

UPALILIAJI
Njegere zipaliliwe zikiwa changa shamba lililotayarishwa vizuri na kuondolewa magugu ya mda mrefu (Perrenial weeds) linaweza kupalliwa mara moja, kwa sababu njegere hukua haraka, na zinaweza kushindana na magugu. Baada ya kutoa maua, njegere zisipaliliwe ili kuongeza mazao.

Magugu hushindana na kunyanganyana na mimea kutumia virutubisho. Pia huongeza kivuli wakati wa utoaji maua na kusababisha upungufu mkubwa wa mazao. Palizi hufanyika kwa mkono au kutumia dawa za kuua magugu.

MAGONJWA & WADUDU

MAGONJWA

Ascochyta


Kutokea kwa mabaka makubwa ya kahawia kwenye majani na matunda. Pia hutokea hata kwenye shina. Katikati ya baka huwa rangi ya kijivu, kingo nyekundu / nyeupe husababishwa na fangasi aina ya Ascochyta pisi.

Root Rot na Blight disease.(kuoza kwa mizizi na Blingt)
Husababishwa na fangasiA. pinodella na mycosphaerella pinodes.

Dalili: – madoa madogomadogo yenye rangi ya zambarau / rangi ya kahawia iliyokaza au madoa meusi ambayo huungana na kusababisha jani na maua kuwa yenye rangi nyeusi .

Kuzuia.
1. Kutumia mbegu zisizo na magonjwa.
2. Kuzika mabaki ya mazao yaliyoadhirika kwa miaka 3 – 4.

Downy mildew
Husababishwa na fangasi Erysiphe polygoni.

Dalili: Majani kuonekana kama yamemwagiwa unga na baadae na

kufa. Ugonjwa unaathiri zaidi mimea kipindi cha uhaba wa unyevunyevu.

Kuzuia: – Kutumia sulphur ya unga kama inavyoshauriwa.

Fusarium wilt:– Husababishwa na fangasi / ukungu Fusarium oxysporum.

Dalili:
1. Majani kubadilika rangi kuwa manjano.
2. Mimea kudumaa.
3. Ugonjwa ukitokea kwenye mimea michanga huua mmea wote.

Kuzuia: – Tumia mbegu yenye uvumilivu kwa ugonjwa huu.
Virusi
– Mmea huonekana kuwa na uvimbeuvimbe kuzunguka jani. Mmea hudumaa.
Kuzuia: – Kutumia mbegu zisizo na maradhi.

WADUDU
Wapo wadudu wengi ambao hushambulia zao la njegere. Baadhi ni kama American bollworm, Bean flies, Bean Aphids, Pea Aphids huambukiza virusi na Green peach aphids.

Inashauriwa kumwona mtaalam wa kilimo aliye karibu yako kwa ufafanuzi wa kuwazuia wadudu waharibifu.

UVUNAJI
Kwa njegere teke / mbichi hukomaa siku 60 – 90 na kwa njegere kavu huchukua siku 80 -150 kukomaa . Njegere teke huvunwa punje zikiwa bado mbichi, Uvunaji hufanyika mara 2 – 3 kwa wiki wakati wa kipindi cha ukuaji. Zaidi ya kilo 3000 kwa hekta za njegere teke huvunwa, Njegere kavu huvunwa wakati punje zimekauka na kuwa ngumu na ni muhimu kuwahi kuvuna njegere kavu ili kutopoteza mavuno zikipasuka. Mavuno ya punje kavu na kilo 1500 kwa hekta.
 
MUHTASARI WA KILIMO CHA MBAAZI

Mbaazi ni zao jamii ya mikunde inayostawi katika nchi za kitropiki zenye mvua chache. Zao hili ni muhimu sana kwa nchi za Asia ambako ni mojawapo ya chakula kikuu hasa katika nchi ya India.

Kwa miaka ya hivi karibuni, zao la mbaazi limekuwa moja ya mazao muhimu ya biashara katika maeneo mengi ulimwenguni. Hii ni kutokana na ongezeko la walaji na uwezo wake wa kustahimili ukame na mvua chache ambao unaendana na mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni kote. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Manyara (Hanang na Mbulu), Arusha (Arusha vijijini na Meru), Dodoma (Kondoa), Kilimanjaro (Same, Mwanga, Rombo, Hai na Moshi vijijini) Mbaazi kwa kawaida hupandwa kwa msimu mmoja lakini aina za kienyeji zinaweza kulimwa kama zao la kudumu ambapo huweza kukaa shambani miaka mitatu hadi mitano ingawa uzalishaji wa mazao hupungua msimu hadi msimu.

Matumizi ya Mbaazi
Chakula/mboga hasa zikiwa mbichi. Mbaazi mbichi huwa na protini zaidi ya asilimia 21%, wanga asilimia 44.8%, mafuta asilimia 2.3% pamoja na baadhi ya virutubisho vya madini kama chokaa na chuma.

Zao la biashara. Kutokana na kuwepo kwa aina bora za mbaazi zinazohitajika kwa wingi katika soko la ndani na nje pamoja na kuwepo kwa aina zinazokomaa mapema na kuwahi soko la dunia, zao hili limekuwa likilimwa kwa ajili ya biashara hasa katika wilaya za Babati, Karatu, Arumeru pamoja na Kondoa

Chanzo cha nishati (kuni). Miti ya mbaazi hutumiwa kwa ajili ya kuni katika maeneo ya ukanda wa chini ambayo haina miti. Matumizi haya pia husaidia kupunguza uharibifu wa mazingira kutokana na watu kutokukata miti ovyo.
Kirutubisho cha udongo. Mbaazi ni jamii ya mikunde ambayo huongeza mbolea aina ya Naitrojeni kwenye udongo. Majani yake yanapopukutika na kudondoka ardhini huoza na kubadilika kuwa mbolea ambayo pia huboresha muundo wa udongo. Chakula cha mifugo. Maganda na majani ya mbaazi hutumika kama chakula kwa ajili ya kulishia mifugo.

Hali ya hewa
Mbaazi hustawi vizuri katika nyuzi joto 29 hadi 38, na hupandwa kuanzia usawa wa bahari hadi mita 1900 kutegemeana na aina ya mbegu. Kuna mbegu zinazostawi katika ukanda wa chini, wa kati na wa juu. Aidha kuna aina zinazostawi zaidi ya mita 2000 kutoka usawa wa bahari Zao hili huhitaji kiasi cha milimita 600 hadi 1000 cha mvua kwa mwaka. Aina za mbaazi za muda mfupi hutosha kustawi katika mvua kiasi cha milimita 250 hadi 370 kwa mwaka.

Udongo
Kwa kilimo chenye tija, ni vizuri kuotesha mbaazi kwenye udongo unaoruhusu maji, wenye mbolea kiasi na wenye tindikali kiasi cha pH kuanzia 5 hadi 7.

UTAYARISHAJI WA SHAMBA
Shamba la mbaazi litayarishwe mapema kwa kung’oa mabaki yote ya mimea pamoja visiki kabla ya kulilima.
Lima shamba kiasi kisichopungua sentimeta 30.
Lainisha udongo kwa kupitisha haro.
Tayarisha matuta au makinga maji kama shamba liko kwenye mteremko.
Kuandaa mbegu
Mbegu bora iliyochaguliwa vizuri na kuhakikiwa kiwango cha uotaji ziandaliwe.
Mbegu ziwekewe dawa ya kuzuia kuvu (fungus) kabla ya kupanda ili kuzuia magonjwa yatokanayo na mbegu na udongo.
Mbegu bora
Mbegu za mbaazi zimegawanyika katika makundi makubwa matatu nazo ni, mbegu za muda mfupi, mbegu za muda wa kati, mbegu za muda mrefu.

KUPANDA
1. Mbaazi za muda mfupi, zipandwe peke yake bila kuchanganya na mazao mengine. Nafasi: Kuwe na nafasi ya sentimeta 75 toka mstari na mstari, sentimita 20 toka shimo hadi shimo. Kiasi cha mbegu: Kilo 5 hadi 6 zaweza kutumika kwa ekari moja.

2. Mbaazi za muda wa kati, zipandwe peke yake na katika mwinuko kutoka usawa wa bahari wa mita 1000 hadi 1880 Nafasi: Kuwe na nafasi ya sentimita 120 toka mstari hadi mstari na sentimita 30 toka shimo hadi shimo. Kiasi cha mbegu: Waweza kutumia kilo 5 kwa ekari moja.

3. Mbaazi za muda mrefu, zipandwe peke yake katika mwinuko toka usawa wa bahari wa mita 1000 hadi 1880. Nafasi: Kuwe na sentimita 150 toka mstari hadi mstari na sentimita 50 toka shimo hadi shimo. Kiasi cha mbegu: Waweza kutumia kilo 5 kwa ekari moja

PALIZI NA KUPUNGUZIA MIMEA
Ni muhimu kupalilia mapema (angalau mara mbili kulingana na kiasi cha unyevu au mvua) na kuondoa magugu ambayo hushindana na mimea michanga. Miche ikiwa mingi kwenye shina husababisha mazao kuoza. Kwa hivyo ni muhimu kupunguza miche na kubaki miwili au kutegemeana na nafasi.

WADUDU
Kuna wadudu wa aina mbalimbali ambao kushambulia mbaazi, wakati zikiwa shambani au zikiwa galani.
1. Vidukari
Vidukari weusi wanaotembea kwa makundi na ambao huonekana zaidi katika sehemu changa za mimea kama vichomozo, matawi na majani. Wadudu hawa husambaa kwa wingi wakati wa majira ya ukame. Wadudu hawa hufyonza majimaji au utomvu ulio kwenye maeneo hayo na kusababisha mbaazi kubadilika rangi na kukauka. Udhibiti….Wadudu hawa hudhibitiwa kwa kutumia njia bora za kilimo na kufanya kilimo cha mzunguko.

2. Kunguni wa mifuko ya mbaazi
Kuna aina nne za wadudu hawa ambao ni Kunguni wa kahawia (Claiigralla spp), Kunguni wakubwa (Anoploenemies spp), Riptutasi (Riptortus dentipes), Kunguni wa kijani (Nezara viridula). Wadudu hawa hufyonza mbegu inayokuwa kupitia kuta za mifuko na kufanya mbegu kuoza na kukosa thamani ya kuwa mbegu na chakula cha binadamu. Udhibiti….Wadudu wanaofyonza mifuko ni vigumu kuwadhibiti kwani huruka kutoka sehemu moja na kwenda nyingine hivyo wanaweza kukusanywa kwa chandarua na kuangamizwa.

3. Mbawakavu wa maua na chavua (Blister beetles)
Wadudu hawa wenye rangi ya njano hula maua na kupunguza uzalishaji wa mifuko ya mbaazi. Katika eneo ambalo uzalishaji wa mbaazi ni mkubwa, wadudu hawa hufanya uharibifu mdogo kuliko katika eneo ambalo mbaazi huzalishwa kwa kiasi kidogo. Udhibiti….Wadudu hawa wanaweza kudhibitiwa kwa kuwaondoa kwa mikono na kuwauwa isipokuwa wakati wa kuwashika kuwepo na uangalifu kwani wakisumbuliwa huweza kutoa kemikali ambayo inaweza kuunguza mikono au mwili.

4. Funza wa vitumba (Maruca vitrata)
Wadudu hawa hutaga mayai kwenye vikonyo vya mbaazi kabla ya kuchanua au juu ya mifuko hula vikonyo vya maua na mbegu iliyoko ndani ya mifuko ya mbaazi. Udhibiti. Mkulima anaweza kuwadhibiti wadudu hawa kwa kufanya ukaguzi wa shamba mara kwa mara ili kufahamu uwepo wa wadudu hawa, pamoja na kutumia viuatilifu kulingana na maelekezo ya mtaalamu wa kilimo. Ni vyema ukaguzi ukafanyika wiki moja kabla ya mbaazi kuchanua na baada.

5. Inzi wa mifuko (Melanagromyza chacosoma)
Hawa ni wadudu wadogo weusi warukao na wanaotaga mayai katika kuta za mifuko za mbaazi inavyokua. Funza wake ni weupe na wana urefu wa sentimeta 3. Wadudu hawa hufanya uharibifu mkubwa kwa kula mbegu changa iliyopo kwenye mifuko. Udhibiti. Katika maeneo ambayo wadudu warukao ni tatizo, jamii ya mikunde inayokomaa kwa muda tofauti isipandwe kwenye shamba moja ili kuzuia mwendelezo wa kuzaliwa kwa inzi hawa hasa kila aina ya mikunde inapotoa maua. Pia mwarobaini waweza kunyunyiziwa mara 4 kila baada ya wiki kwa kiwango cha gramu 50.

6. Vithiripi (Megalurothrips spp. And Frankliniella schultzei)
Wadudu hawa wadogo na wenye rangi ya kahawia na mabawa ya njano huathiri mbaazi hasa kwa kufyonza utomvu kwenye majani na maua.Husababisha maua na vikonyo kusinyaa, kufifia rangi na kudondoka kabla ya kukomaa. Udhibiti. Kagua shamba kila mara ili kufahamu uwepo wa wadudu hao kabla ya mimea kuchanua ili kudhibiti mapema.

7. Vipekeche
Hawa ni wadudu wanaoshambulia mbaazi ikiwa ghalani. Wadudu hawa hutoboa mbegu na kutengeneza mashimo ya kutokea wadudu kamili.
 
Back
Top Bottom