JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
UN yatoa wito kwa Mamlaka za Tanzania kutoa taarifa za waliopotea na waliokufa Oktoba 29
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu imesema kuna taarifa za vifo, majeruhi na watu kukamatwa katika kile kilichokea wakati wa uchaguzi, Oktoba 29 nchini Tanzania. Kamishna Mkuu Volker Turk ametoa wito kwa mamlaka kuhakikisha familia zinapata taarifa za wapendwa wao na kuheshimu haki za msingi kama uhuru wa kujieleza na kukusanyika kwa amani, sambamba na uwajibikaji kwa matukio yaliyotokea.
Umoja wa Mataifa unakubaliana na hatua ya Serikali kuanzisha uchunguzi, lakini umesisitiza uchunguzi huo uzingatie viwango vya kimataifa ikiwemo uhuru, uwazi na ulinzi kwa wanaotoa ushahidi.
Aidha, imeeleza kuwa kumekuwa na matukio ya kukamatwa kwa wasomi, viongozi wa kisiasa na watendaji wa asasi za kiraia tangu katikati ya Novemba 2025, na imetaka wote waliokamatwa kiholela, waachiwe mara moja.
Maoni ya wananchi:
Wananchi wengi wamesema wamechoka kuona matamko na sasa wakataka vitendo, kwani kama matamko yangekuwa yamefanya kazi, basi wale wote waliohusika katika mauaji ya wannachi wangekuwa wameshawajibishwa. Wameitaka UN kuichukulia hatua Tanzania ili kulazimisha uwajibikaji.
Aidha, wengine wamesema maandamano hayataisha mpaka wote waliohusika na mauaji wamechukuliwa hatua, pamoja na uchaguzi wa huru na haki kufanyika upya.
Polisi yathibitisha kumshikilia Geofrey Mwambe, yasisitiza hali ya usalama kuwa shwari nchini
Jeshi la Polisi limethibitisha kumshikilia aliyekuwa Waziri wa Uwekezaji na Mbunge wa Masasi katika awamu ya 5, Geofrey Mwambe, aliyekamatwa usiku wa Desemba 7 katika eneo la Tegeta, Kinondoni, kwa tuhuma za jinai ambazo zinaendelea kuchunguzwa. Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa hatua za kisheria kuhusu tukio hilo zinafuatwa ipasavyo.
Kabla ya taarifa hiyo rasmi, kulikuwa na tetesi zilizosambaa kupitia mitandao ya kijamii zikidai kuwa Mwambe alikamatwa na Polisi na kushikiliwa kwa siri, huku ikidaiwa kuwa alikumbana na ukiukwaji wa taratibu za kisheria.
Pamoja na hayo, Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa hali ya usalama mkoa wa Dar es Salaam ni shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku.
Maoni ya wananchi:
Wengi wameendelea kukosoa namna jeshi hilo linavyokamata watuhumiwa kiholela, bila kufuata utaratibu na kukaa kimya kuhusu ukamatajii huo mpaka pale wananchi watakapopiga kelele jambo ambalo linaendelea kukandamiza haki za raia.
Wengine wamesema ni dhahiri kuwa wanaohusika kwenye matukio wa utekaji, watu kupotea na kuuliwa ni vyombo ya dola, na kwamba matukio yote ambayo Polisi hujitokeza na kufafanua ni majaribio ya utekaji yaliyofeli.
Kuhusu tamko la Jeshi la Polisi, wengi wameona ni njia ya kuwatisha wananchi ili wasijitokeze kuandamana wakati mwingine.