JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
Odero: Lissu kuwa gerezani hakuzuii maridhiano kufanyika. Mazungumzo yanaweza kumaliza changamoto tunazopitia CHADEMA
Kada wa CHADEMA, Charles Odero, amesema ni muhimu kwa vyama vya siasa na Serikali kukaa meza moja ya mazungumzo ili kuimarisha mshikamano wa kisiasa na kusukuma mbele maendeleo ya taifa. Akizungumza na Vyombo vya Habari, Odero amesema kuwa CHADEMA haipaswi kuona ugumu wa kukutana na Serikali pamoja na Rais Samia, kwa ajili ya kufanya maridhiano ya kitaifa, hata katika mazingira yenye changamoto za kisiasa.
Ameeleza kuwa changamoto zinazokikabili chama hicho hazipaswi kuwa kikwazo cha mazungumzo ya kisiasa. Odero amesisitiza kuwa mazungumzo yanaweza kuzaa suluhu hata katika nyakati ngumu, akitolea mfano wa kipindi ambacho aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alishikiliwa kwa tuhuma za ugaidi, lakini mazungumzo kati ya viongozi wa CHADEMA na Rais Samia yalifungua ukurasa mpya wa kisiasa nchini.
Maoni ya Wananchi:
Wengi wamepinga wito huo wakisema kuwa maridhiano hayawezi kufanyika bila kushughulikia madai ya msingi yanayohusisha haki, ikiwemo kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa, ukamataji holela na utekaji kukoma, uwajibikaji kwa mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu uliotokea wakati wa uchaguzi, pamoja na upatikanaji wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.
Wapo waliohisi kuwa tayari Odero ‘ameshanunuliwa’ ili kuwasaidia Serikali kuwashawishi wananchi kukubali Serikali ambayo wao hawajaichagua na kufanya mazungumzo ili wasahau yaliyotokea wakati wa uchaguzi na kusonga mbele. Wametaka Odero apuuzwe na asiwatoe wananchi kwenye mambo ya msingi.
Wengi wamekosoa vikali wahusika wanaosukuma wazo la maridhiano, yakiyatafsiri kama propaganda au juhudi za kupuuza maumivu ya wananchi, huku baadhi ya wachangiaji wakitumia lugha kali, kejeli na matusi kuonesha kutoridhishwa kwao na mwelekeo wa mjadala huo.
Buyobe aachiwa kwa dhamana, alishikiliwa Kituo cha Polisi Chang’ombe
Baada ya mdau kutoka JamiiForums.com kuhoji alipo Fortunatus Buyobe ambaye alikamatwa toka Disemba 6 na watu waliojitambulisha kuwa Polisi, huku mamlaka zikiwa kimya kutoka kipindi hicho, hatimaye saa chache baadaye Buyobe ameachiwa kwa dhamana.
Buyobe alikuwa akishikiliwa katika Kituo cha Polisi Chang’ombe.
Maoni ya wananchi:
Wengi wameendelea kukosoa ukamataji wa Polisi unavyokwenda kinyume na utaratibu pamoja na sheria za nchi. Wananchi wanazidi kukosa Imani na Jeshi la Polisi kadri siku zinavyozidi Kwenda. Wapo waliofikia hatua ya kujiapiza mitandaoni (TikTok na Instagram) kuwa wataanza kulipiza kisasi kwa mambo wanayotendewa na Polisi, jambo lililoibua hisia kuwa huenda hali ikawa mbaya zaidi kwani wanatoa mwanya wa kuzuka makundi ya kigaidi na ujambazi.
Baadhi wamesema Kituo cha Polisi Chang’ombe kinatakiwa kuchunguzwa kutokana na kutumika kama ‘karakana’ ya kuwaficha watu wanaokamatwa kiholela na baadhi ya wanaodaiwa kutekwa, wakitolea mfano wa Deusdedith Soka pamoja na wenzake, ambao inadaiwa waliitwa kwenda kituoni hapo na huo ndio ukawa mwisho wa kuonekana kwao.