JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
Maadhimisho ya Miaka 64 Uhuru wa Tanganyika Vyombo vya Ulinzi vyatanda barabarani. Serikali yasema haikutoa amri ya watu kukaa ndani. Maandamano yakwama…
Maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika kwa mwaka 2025 yamekuwa ya aina yake baada ya vijana kutangaza kufanya maandamano yasiyo na kikomo kuanzia siku hii mpaka matakwa yao yatakapotekelezwa.
Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilitanda katika barabara zote za mijini na maeneo yaliyokuwa na ushiriki wa watu wengi katika maandamano ya Oktoba 29. Vizuizi vya barabarani viliwekwa vingi na ukaguzi wa watu ulifanyika huku wakiwahoji wanaenda wapi na kufanya shughuli gani.
Ikumbukwe, jana Rais Samia aliagiza wananchi kufanya maadhimisho hayo nyumbani na kutoka pale tu mtu anapolazimika, jambo ambalo kwa wananchi lilichukuliwa kama amri kwani mitaa ilionesha kuwa mitupu, japokuwa vizuizi vya Polisi navyo viliongeza ugumu wa watu kufanya shughuli zao.
Vyombo vya usafiri kwa kiasi kikubwa havikufanya kazi na hivyo kuongeza ugumu kwa wananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kutokana na changamoto hizi, wafanyabiashara waliofungua sehemu zao za kazi wamelalamika kukosa wateja, huku wengine wakiilaumu Serikali bidhaa zao kuharibika kutokana na kuzuiliwa kusafirisha na kushusha bidhaa zao.
Upande wa maandano, kwa kiasi kikubwa hayakufanikiwa licha ya matamko kutoka Bunge la Ulaya pamoja na Umoja wa Mataifa kuhusu wananchi kuachwa kutekeleza haki yao ya kidemokrasia ya kuandamana. Wengi walishindwa kufika maeneo waliyokubalina kutokana na vizuizi vya Polisi, waliojitokeza walisalia katika maeneo yao yaliyopo mbali na vizuizi hivyo kuepusha kukamatwa. Kuna baadhi ya sehemu ilidaiwa wananachi walikamatwa na kushikiliwa kwa muda waliposhukiwa kuwa waandamanaji.
Aidha, mitandao ya kijamii iligubikwa na taarifa nyingi potofu kuhusu maandamano kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini zikiwa za matukio ya nyuma ikiwemo matukio ya Oktoba 29 na siku zilizofuata. Upande wa upatikanaji wa intaneti, wananchi waliripoti baadhi ya mitandao ya kijamii (JamiiForums, X, TikTok, Telegram, WhatsApp na Clubhouse) kutopatikana bila matumizi ya VPN huku sehemu nyingine wakipata kasi ndogo ya mtandao na hivyo kuathiri shughuli zao.
Kwa upande mwingine, Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, imesema haikutoa amri ya watu kukaa ndani bali Rais Samia ‘alishauri’ wananchi washerekee siku hiyo kwa kuwa maeneo ya karibu na nyumbani na sio kujifungia ndani, huku Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akisema watu waliamua wenyewe kusherekea siku hii kwa kukaa ndani! Simbachawene amesema kuanzia kesho, Disemba 10 wananchi wataendelea na ratiba zao kama kawaida huku Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikiendelea kuimarisha usalama kuelekea sherehe za mwisho wa mwaka.
Maoni ya wananchi:
Wengi wameonyesha mshangao kutokana na kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar na Simbachawene kuwa wananchi walikaa ndani kwa hiyari yao wenyewe. Wanasema mbali na agizo la Rais kuchukuliwa kama amri, pia wengi walipokutana na vizuizi barabarani waliambiwa na Vyombo vya Ulinzi kuwa leo sio siku ya kazi na wanatakiwa kurudi majumbani mwao.
Baadhi wamehoji kama Serikali ina mpango wa kuweka vyombo vya ulinzi pamajo na vizuizi barabarani kwa miaka yote mitano, kwani hawataacha kuandamana kwani wao wanajua ni maandamano yasiyo na kikomo.
Wengine wameita maadhimisho ya leo kama “Aibu ya Kihistoria,” ambapo watu wamesherekea Siku ya Uhuru kwa kutokuwa Huru, wakiwa na hofu kwa Serikali yao iliyotakuwa kuhakikisha siku hii inakuwa ya kujivunia! Badala ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru imekuwa ‘Maadhimisho ya Vifungo vya Ndani’.
Aidha, kwa upande mwingine wapo walioona kuwa maandamano yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kwamba wanatakiwa kujipongeza.
Pia, kuhusu kilichotokea leo wapo, wanaotoa maneno ya kejeli kuhusiana na ukimya uliotawala nchi nzima lakini wasichojua ni gharama kubwa ambazo Serikali na vyombo vyake imeingia. Kuanzia gharama za kusafirisha watu na vifaa, gharama za malazi ambapo askari na wapepelezi wengi sana wamesafirishwa na kulazwa katika nyumba za kulala wageni na lodges, posho za watu wao wote. Wanaamini imegharimu mabilioni ya pesa.
Wanahoji, endapo operesheni hii kwa wiki nzima au iendelee hadi mwisho wa mwaka italigharimu taifa kiasi gani cha pesa? Wanaamini mapato ya kodi yamepungua kutokana na kushuka shughuli za biashara, kupungua watalii, nk.
Polisi wadaiwa kuvamia nyumba ya Mwenyekiti wa CHADEMA Geita Vijijini, wakamata familia nzima
Desemba 9 majira ya Alfajiri, Polisi wameripotiwa kuvamia nyumba ya Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Geita Vijijini, Neema Steven Chozaile, na kuikamata familia yote baada Chozaile kukosekana. Waliokamatwa ni watoto wakiwemo Kelin Benedictor Jafety, mwanafunzi wa Kidato cha Pili; Eliud Thobias Moyi, mwanafunzi wa Chuo cha VETA - Umeme; Elias Sebastian Maya, mtoto wa miaka 5; na Asteria Sebastian, mtoto wa miaka 3. Wengine waliokamatwa ni mama Grand (wifi), mama Virginia (jirani), Thabiza (binti wa kazi), na Siwema Jakobo, mdogo wake Chozaile.
Taarifa hiyo imetolewa na CHADEMA ikionyesha ni ujumbe uliotumwa na Chozaile, na kubainisha kuwa Polisi hao walifanya maamuzi yao ili kupata taarifa kuhusu mahali Chozaile alipo, huku baadhi ya watoto wakiripotiwa kupigwa ili kutoa taarifa.
Maoni ya wananchi:
Wengi wameonyesha kukasirishwa na tukio hilo, ambapo wamehoji maagizo ya Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene yalikuwa na maana gani kama Polisi wanaendelea kuvunja taratibu pale wanapomkamata raia? Wameongeza kuwa, Jeshi la Polisi kwa sasa linatakiwa kufumuliwa na kuundwa upya.
Aidha, wengine wameendelea kulaani kwa wapinzani na wakosoaji wa Serikali kuendelea kukamatwa ovyo ama kumbambikiwa kesi, wakisema Serikali inatakiwa kushughulikia malalamiko ya wananchi na kuwajabika na si kuwanyamazisha wakosoaji, kwani huo ndio utawala bora.
Polisi watoa tamko kwa lugha ya Kiingereza, lazua mjadala mitandaoni
Katika hatua ambayo imewashangaza, Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) na Polisi kupitia mtandao wa Instagram wameweka tamko ambalo linaonekana kuwa na Jeshi la Polisi likiwa katika lugha ya Kiingereza.
Katika tamko hilo lililotolewa majira ya jioni saa za Afrika Mashariki, linaonyesha Jeshi la Polisi likisema hali ya usalama nchini siku ya leo, Disemba 9, 2025 ilikuwa tulivu.
Tamko hilo linaongeza kuwa Jeshi la Polisi linapenda kuwasihi wananchi kuendelea kupuuza picha za video na mnato zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa, maandamano yameanza katika maeneo mbalimbali.
Kwa mujibu wa tamko hilo, Taarifa hizo si za kweli; picha hizo ni za matukio ya nyuma, zikiwemo zile za tarehe 29, 30, na 31 Oktoba 2025. Nyingine ni za matukio ya zamani, kwa mfano, tukio moja ni la Juni 2025 ambapo jamii ya Wamasai ilikuwa ikifanya sherehe za kimila (unyago/jando) katika msitu wa TANAPA Jijini Arusha.
Maoni ya Wananchi:
Moja kati ya vitu vilivyowashtua wengi, ni tamko hilo kutolewa kwa lugha ya kiingereza huku likiwa linawalenga Watanzania ambao si wazungumzaji wa lugha hiyo na si kawaida ya Jeshi la Polisi kufanya hivyo. Wengine walikosoa barua hiyo kuwa na makosa mengi ikiwemo tarehe tisa kuandikwa '9rd' badala ya '9th'. Kuna waliosema Polisi kwa kutoa tamko hili kwa lugha ya kiingereza kunaonyesha Jeshi hilo kukosa uzalendo.
Wengine wamewashangaa Polisi kutambua video za matukio ya Oktoba 29, 30 na 31 ambapo awali walidai kuwa zilikuwa zimetenegezwa, kwa akili unde (AI). Wakaenda mbali na kutaka Polisi wakiri kuwa picha na video za maiti zilizozagaa mitaani zilikuwa halisia. Wapo pia waliofanya kejeli wakitaka tamko lifutwe kabla watu wengi hawajaona ikawa aibu. Wakahoji, kama X imefungiwa Tanzania, Msemaji Mkuu ametumia VPN gani kuweka tamko hilo
Kwa tamko hili kusema 'Msitu wa TANAPA jijini Arusha' pia ilionekana kuwashangaza baadhi ya wananchi.