JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
TEC yalaani mauaji ya raia Oktoba 29. Yataka uwajibishwaji wa viongozi wa vyombo vya usalama, uchunguzi huru kufanyika na Katiba Mpya
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa tafakuri yake juu ya yale yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, likilaani mauaji, utekaji, kuumizwa na kupotea kwa watu. Wametuma pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na kuwaombea majeruhi kupata nafuu, wakisisitiza kuwa uhai ni zawadi takatifu na mauaji yaliyotokea ni uovu mkubwa na chukizo kwa Mungu.
Katika tafakuri yao, Maaskofu wamesema kila maandamano si uhalifu, cha msingi yawe ya maandamano ya amani kwani kuandamana ni haki ya kikatiba, na kuonyesha masikitiko yao kuona waandamanaji wote waliojitokeza siku ya uchaguzi kuwekwa katika mwavuli wa uhalifu.
Aidha, TEC wameeleza kuwa vurugu zilitokana na ukosefu wa usalama, kukandamizwa kwa demokrasia, na baadhi ya mihimili ya dola kushindwa kushughulikia malalamiko ya wananchi. Pia, wamekosoa matumizi ya nguvu kupita kiasi na matumizi ya risasi za moto dhidi ya raia wasio na silaha, kuwanyima majeruhi haki ya huduma za afya pamoja na ndugu kunyimwa miili ya wapendwa wao ili kufanya taratibu za mazishi.
TEC imependekeza hatua kadhaa za kuponya taifa, ikiwemo viongozi kukiri makosa, kuwajibika au kuwajibishwa na mamlaka zilizowateua wale wote waliotumia nguvu kupita kiasi, na kuanzisha uchunguzi huru unaojumuisha timu ya watu wa ndani na nje ili kubaini ukweli wa yaliyotokea huku wakiitaka Serikali kuwa tayari kuipokea ripoti hiyo na kuifanyia kazi.
TEC wameitaka Serikali kuwaachia huru wote waliokamatwa kwa hila kabla na baada ya uchaguzi bila masharti yoyote, pamoja na kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya yenye misingi ya haki, usawa na utawala wa sheria.
Maaskofu wamehimiza viongozi kuishi kwa uadilifu na uwazi, na kusikiliza sauti za wananchi ili kuepusha mgawanyiko zaidi. Wamewataka Watanzania kuendelea kusali kwa ajili ya amani, haki na uponyaji wa taifa, wakisisitiza kuwa risasi haziwezi kunyamazisha watu na kwamba hekima ndiyo njia ya kujenga mwanzo mpya kwa nchi.
Maoni ya wananchi: Wengi wamepongeza na kuunga mkono hoja za TEC wakilinganisha na tamko la BAKWATA ambao moja kwa moja liliwalaumu wananchi waliodaiwa kuanzisha vurugu kama chanzo cha mauaji yaliyofanywa na vyombo vya ulinzi.
Wengine wameendelea kusisitiza kuwa bila uwajibikaji hakuna kusogea mbele, maana hiyo itamaanisha wauaji wameachwa waendelee kumaliza wananchi.
‘Shura ya Maimamu’ yalaani mauaji ya wananchi wakati wa Uchaguzi Mkuu, wakataa kupongeza uchaguzi uliofanyika
Shura ya Maimamu Tanzania imelaani vikali vifo, majeruhi, na uharibifu wa mali vilivyotokea wakati wa uchaguzi, ikisema mioyo yao imejaa huzuni lakini bado wana matumaini ya kurejea kwa haki na utu wa binadamu.
Akiwasilisha waraka wao mbele ya wanahabari, Novemba 15, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda amesema wanashauri Viongozi wa Dini, Viongozi Wastaafu wa Serikali na Taasisi za Haki za Binadamu, waombe kukutanisha Serikali ya CCM na Wapinzani wake kujadili Mustakbali wa Taifa.
Sheikh Ponda ameeleza kuwa hawawezi kupongeza uchaguzi uliofanyika kwani waangalizi wa Shura hiyo walibaini ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi na haki za binadamu unaofanana na ripoti za SADC, AU na EU, ikiwemo kukandamizwa kwa haki za wapiga kura na mauaji ya raia wasiokuwa na hatia.
Pia, amesisitiza kuua mtu asiye na hatia ni dhambi kubwa katika dini zote, na huku akiikosoa BAKWATA kwa kupongeza uchaguzi akidai haijulikani vigezo walivyotumia.
Maoni ya wananchi: Wananchi walio wengi wamepongeza waraka wa Shura ya Maimamu kwa kusimama kwenye ukweli na haki huku wakikosoa tamko la BAKWATA wakisema wapo kwaajili ya kuitetea Serikali na kwamba sio wawakilishi wa kweli wa waislamu.
Baadhi wamekuwa tofauti na waraka huo wakisema Sheikh Ponda ni sehemu ya tatizo kwa kukubali kuingia kwenye uchaguzi (aligombea Ubunge Temeke) pamoja na chama chake cha ACT-Wazalendo hata baada ya kuonywa na kujua fika matokeo yatakuwaje.
Waziri Mkuu afanya ziara ya kushtukiza Hospitali ya Rufaa Dodoma, atoa maagizo
Waziri Mkuu Mpya wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya ziara ya kushtukiza Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Novemba 15, akiziagiza hospitali zote nchini kuwahudumia wajawazito kwa haraka ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Ameitaka Wizara ya Afya, Bohari ya Dawa (MSD) na hospitali zote nchini kuhakikisha dawa zinapatikana muda wote na kuacha kuwaelekeza wananchi kununua dawa nje. Pia, ametoa maelekezo ya kuwepo kwa vifaa vya usafi vya dharura kwenye wodi za wazazi na matumizi sahihi ya mifumo ya malipo.
Maoni ya wananchi: Wengi wameiona ziara hiyo kama mzaha na kusema ni maigizo ya kuwashawishi wananchi kuwa wanafanya kazi ili waachane na maandamano, wakiongeza kuwa haiwezi kuwa ziara ya kushtukiza huku akiwa ameambatana na msururu wa watu wengi hospitalini hapo.
Wengine wamepingana na wananchi waliotoa maoni yao kwa Waziri Mkuu kuwa ‘wamepata huduma nzuri hospitalini hapo’ wakisema wametoa maoni hayo ili kunusuru uhai wao, kwani wangesema vinginevyo huenda wangepotezwa, lakini pia huduma za hospitali za serikali zinajulikana zilivyo, hivyo majibu ya watu hao hayaonyeshi kuwa halisi.
Aidha, wengine wamesema badala ya kutoa matamko hospitalini anatikiwa kuhakikisha zinatungwa sera kwa ajili ya kuhakikisha huduma hizo zinatolewa kwa ubora vinginevyo yatabaki kuwa matamko tu bila utekelezaji.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa: Rais Samia kutoa Msamaha siyo uoga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Chama cha Mapinduzi (CCM), Fadhil Maganya amesema vurugu zilizotokea Oktoba 29 hazijawahi kushuhudiwa nchini, na msamaha alioutoa Rais Samia kwa baadhi ya vijana waliokuwa wakifuata mkumbo si dalili ya uoga, bali ni hatua ya kutibu maumivu ya Taifa akisema Rais Samia angeweza kufanya lolote lakini kama kiongozi, mzazi, mlezi na mfariji mkuu akaamua kutoa msamaha badala yake.
Akizungumza leo Novemba 15 jijini Dodoma, Maganya amesema hatua hiyo inalenga kuirudisha Tanzania kwenye umoja na mshikamano baada ya uchaguzi na kutoa wito kwa familia, viongozi na jamii kuwaongoza vijana kutambua thamani ya amani na kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa nchi.
Moani ya wananchi: Wengi wameonyesha hasira juu ya hoja ya tamko hilo wakihoji Rais ametoa msamaha kwa kosa gani? Lakini, pia wanamaanisha nini kusema wananchi waliandamana kwa kufuata mkumbo; wanamaanisha kuwa hawaelewi kuwa sheria za uchaguzi zilikuwa kandamizi na hawaoni maovu yanayofanywa na CCM pamoja na Serikali yake?
Aidha, wengine wameshangazwa na kauli ya Mwenyekiti huyo aliposema Rais angeweza kufanya chochote, je hiyo inamaanisha ni uuaji na vitendo vingine vya ukatili zaidi? Huku wakiongeza kuwa wananchi sio wajinga, hawatakaa kimya na kwamba maandamano ya awamu ya pili yanakuja kwaajili ya kuikataa serikali hiyo.