Muhtasari wa Matukio Muhimu Tanzania - Novemba 16, 2025

Muhtasari wa Matukio Muhimu Tanzania - Novemba 16, 2025

JF Summary

Senior Member
Joined
Jul 3, 2015
Posts
163
Reaction score
109
Serikali yakanusha video ya miili kuonekana Hospitali ya Mwananyamala, yadai imetengenezwa kuleta taharuki
Serikali kupitia Wizara ya Afya imekanusha madai yaliyosambaa mtandaoni kuanzia Novemba 15 usiku kupitia video ambayo ilikuwa inaonyesha miili ya watu waliofariki ikiwa imelezwa sakafuni na mingine kwenye meza ikidaiwa kuwa ipo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Mwananyamala. Miili hiyo ilielezwa imetokana na mashambulizi ya polisi yaliyofanywa dhidi ya raia wakati wa uchaguzi.

Wizara imesema video hiyo si ya kweli na imatengenezwa na wahalifu kwa lengo la kuzua taharuki miongoni mwa wananchi.

Muda mfupi baada ya kanusho hilo, picha zilianza kuibuliwa na watu mbalimbali mtandaoni baadhi wakitambua ndugu zao kwenye video hiyo huku wengine wakithibitisha uhalisia wa eneo hilo kwa kulinganisha na matukio ya nyuma kwa kutumia teknolojia.

Baada ya maoni ya wananchi wenye hasira kuzidi kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya Wizara hiyo, maudhui hayo yaliondolewa kwa muda (archive) lakini walirudisha baada ya muda wakiwa wamezuia wananchi kutoa maoni yao.

Maoni ya Wananchi: Wengi wameonyeshwa kukasirishwa na kanusho hilo wakihoji, Wizara inawezaje kukanusha wakati watu kadhaa ambao walikosa miili ya ndugu zao wamewatambua kwenye video hiyo, huku picha za matukio ya nyuma zikizidi kuthibitisha uhalisa wake?

Wengine wamehoji kama kweli wana uhakika video hiyo si halisi, kwanini walifuta maudhui hayo, na zaidi kwanini wamerudisha lakini wakazuia wananchi kutoa maoni?

Pia, wananchi wengine wamesema matukio ya namna hii yanazidi kuongeza hasira kwao na hivyo kuongeza hamasa ya wananchi kushiriki katika maandamano yanayoandaliwa kufanyika Disemba 9 almaarufu “D9”.

Katika hali ya kushangaza, vyombo vya habari vya asili hawakuchapisha kabisa taarifa hiyo hata kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kama ilivyo kwa fafanuzi nyingine ambazo zimekuwa zikitolewa na idara mbalimbali serikalini!

Rais Samia awasisitiza watanzania kuendeleza maombi ya kulilinda Taifa lidumu katika amani
Rais Samia amewataka Watanzania kuendelea kuliombea Taifa ili kudumisha amani, upendo, ustahimilivu na mshikamano. Hii ni kwa mujibu wa salamu zilizowasilishwa Novemba 16, na Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba kwa waumini na viongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kisasa, Dodoma.

Mwigulu amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda amani, katika ibada hiyo iliyoendeshwa na Askofu Christian Ndossa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na Bunge, ikiwa ni pamoja na mke wa Mwigulu, Naibu Spika Daniel Sillo, na wabunge kadhaa.

Maoni ya wananchi:
Wananchi wengi wamesema kutumia nyumba za ibada kuhubiri amani huku hakuna hata mmoja kati ya waliofanya mauaji aliyewajibishwa ni kumdhikaki Mungu pamoja na Watanzania, wakisisitiza kuwa kinachohitajika ni uwajibikaji wa kweli na sio maigizo ya kujaribu kujisafisha.

Wengine wamekosoa kutumia nyumba ya ibada kufanya siasa, wakisema alichokifanya Waziri Mwigulu hakina tofauti na alichofanya Askofu Gwajima, lakini mpaka wakati huu makanisa yake yamefungwa na yeye kuendelea kusakwa kwakuwa tu alikuwa na maoni tofauti na serikali.

Dkt. Malisa: Rais Samia ajiuzulu kabla ya Desemba 9 au akabili maandamano makubwa kuwa kutokea Afrika
Aliyekuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dtk. Godfrey Malisa, kupitia mtandao wa kijamii ametangaza kuwa kutakuwa na maandamano makubwa Disemba 9 kwaajili ya kupinga uongozi wa Rais Samia na kile anachokiita "Serikali batili ya Samia," akisema siku hiyo ndio siku ambayo, “Dunia itaona maandamano ya kipekee, ya kihistoria na yasiyo na vurugu,” huku akiwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi na kudai haki zao kwa amani.

Malisa amesisitiza kuwa maandamano hayo hayataleta uharibifu, akiwakumbusha waandamanaji kutulia na kutokujibu uchokozi, na pia amewataka maafisa wa Jeshi la Polisi kutohusika moja kwa moja, akidai kwamba jeshi ndilo litakalosimamia na kulinda waandamanaji siku hiyo.

Mapema 2025, Dkt. Malisa alipinga uteuzi wa Rais Samia alipochaguliwa kupeperesha chama chao (CCM) katika mbio za Urais akisema katiba ya chama hicho haikufuatwa, hata hivyo alivuliwa uanachama baadaye kwa kosa la usaliti kwa chama.

Maoni ya wananchi:
Tamko la Dkt. Malisa limeonesha kuwapa hamasa wananchi wengi hasa vijana kujitokeza kwenye maandamano hayo ambapo wengi wameunga mkono wito huo, wakihimiza kushiriki kwa amani pamoja na kubeba mabango yenye jumbe za kudai mabadiliko, huku wakionya Jeshi la Polisi kuacha kabisa kutumia nguvu siku hiyo.
 
Back
Top Bottom