JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
CHADEMA, ACT Wazalendo na CUF wapinga Tume ya uchunguzi aliyoiteua Rais Samia
Vyama vya CHADEMA, CUF na ACT-Wazalendo vimepinga Tume ya Uchunguzi iliyoteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, vikieleza kuwa haina uhalali wa kisheria, kisiasa na kimaadili. Vyama hivyo vinasema tume hiyo imeundwa na wajumbe ambao wengi wao ni watumishi wa serikali, wateule wa marais kwenye uongozi uliopita huku wengine wakiwa wanachama wa CCM, hali inayodhoofisha uhuru, uadilifu na uwezo wa tume kufanya uchunguzi huru.
Aidha, vyama hivyo vimesema serikali inayotuhumiwa kwa mauaji, utekaji na uvunjaji wa haki za binadamu haiwezi kuunda chombo cha kujichunguza yenyewe, na kwamba muundo wa tume hiyo unaweza kuficha ukweli au kupotosha matokeo ya uchunguzi.
Kwa nyakati tofauti, vyama hivyo vimependekeza kuundwa kwa tume huru na yenye uwakilishi mpana wa kitaifa na kimataifa ili kufanya uchunguzi wa kuaminika kuhusu matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi. Vinasisitiza kuwa uchunguzi huo unahitaji chombo kisichotegemea serikali na ambacho hakina mgongano wa maslahi, na kwamba bila uwazi, uwajibikaji na haki, haiwezekani kupata amani ya kweli wala maridhiano ya kitaifa.
Maoni ya wananchi: Wengi wamepongeza msimamo wa vyama hivi na kuunga mkono matamko haya wakiamini bila ushiriki wa vyombo kimataifa na asasi huru za kiraia ripoti itapikwa kuwabeba CCM na serikali iliyopo madarakani licha ya ushahidi wa video na picha kuonyesha mamia ya raia kuuawa.
Viongozi wa dini waendelea kuishambulia TEC kutokana na tafakuri yao ya Uchaguzi, watoa vitisho waziwazi
Mvutano baina ya viongozi wa dini nchini umeendelea kushika kasi kufuatia tafakuri ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), ambapo baadhi ya wahadhiri wa dini ya Kiislamu wametoa maneno makali wakilituhumu baraza hilo, kwa madai ya kuikosoa serikali ya Rais Samia kwa misingi ya ubaguzi wa uzanzibari, jinsia na dini yake. Wakizungumza kwa tahadhari lakini kwa lugha yenye ukali, baadhi yao wameonya kuwa “wakimwaga ugali, nasi tutamwaga mboga,”. Wanadai TEC ilikuwa kimya wakati Marais Wakristo walipoongoza na kufanya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu wakitolea mfano matukio ya nyuma wakidai pia kulikuwa na ukimya wa TEC wakati wa jaribio la mauji kwa Tundu Lissu aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki wakati huo.
Wakati huo huo, Askofu Pius Ikonga wa ‘Kanisa la Matendo Makuu ya Mungu’ ameitupia lawama TEC, akidai ilichangia kwa asilimia 90 vurugu za uchaguzi mkuu wa 2025, na kuitaka iombe radhi kwa tamko lake ambalo, kwa mtazamo wake, limeibua taharuki mpya katika kipindi hiki tete nchini.
Maoni ya wananchi: Wananchi wamesema mvutano wa viongozi wa dini umevuka mipaka, wakisisitiza kwamba ibada si jukwaa la siasa. Wamebainisha kuwa TEC imekuwa sauti ya kukemea mifumo kandamizi katika awamu zote, ilhali baadhi ya wahadhiri wanatajwa kupotosha kwa kuweka “amani” mbele ya haki. Kwa mtazamo wao, haki ikikosekana, amani ni nadharia tu.
Wengi wameonyesha kushangazwa namna viongozi wa dini hasa ya Kiislamu wanavyoituhumu TEC badala ya kutoa hoja zao juu ya Mauaji wakati wa uchaguzi wakisema TEC imepeleka lawama kwa serikali lakini wanaojibu ni BAKWATA na viongozi wengine wa dini hiyo na baadhi ya Wakristo kana kwamba wao ndio wasemaji wa serikali ama wametumwa kuishambulia TEC.
Aidha wengine wamesema TEC imekuwa sauti ya kukemea mifumo kandamizi katika awamu zote bila kujali imani ya Rais anayeongoza wakati huo na kutoa mifano kadhaa ambapo TEC imekuwa ikitoa matamko ya kukemea matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu wakati Marais walipokuwa Wakatoliki. Wananchi waliibua mijadala ya kuonyesha ushahidi wa waraka wa TEC wa Pasaka mwaka 2018 wakikemea matukio ya utekaji, uminywaji wa demokrasia nchini na uhuru wa Vyombo vya Habari pia wakilaani shambulizi dhidi ya Tundu Lissu.
Kwa upande mwingine, wengine wamesema chuki hizi za kidini zinaachwa kuendelea kuwepo bila kukemewa na serikali kwasababu inawaganya wananchi kwenye udini na kuwafanya waache kudai uwajibikaji kutokana na mauaji yaliyotokea wakati wa uchaguzi.
CCM: Wengi walipiga kura kabla ya vurugu, ni maeneo machache yaliyokuwa yameathiriwa na vurugu na ndio maana hatukupata 100%
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi wakati akizungumza na vyombo vya habari katika Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, amesema madai yanayosambaa kwamba ushindi wa chama hicho katika uchaguzi wa Oktoba 29 ni batili, hayana msingi, akibainisha kuwa wingi wa vituo vya kupigia kura ulirahisisha wananchi kupiga kura kwa haraka zaidi kuliko chaguzi za miaka iliyopita.
Amedai pia hamasa kubwa ya wananchi kwenye kampeni za CCM ndiyo iliyoonyesha mapema matokeo ya ushindi huo, akiongeza kuwa kutofikia 100% kwenye matokeo ya uchaguzi kumetokana na vurugu zilizotokea katika baadhi ya maeneo.
Maoni ya wananchi: Kauli yake imepingwa na wananchi wengi wakishuhudia uchache wa watu vituoni na katika maeneo mengine kutojitokeza kabisa. Wengine wamesema wao au ndugu zao waliokuwa wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo mbalimbali ni mashahidi kuwa mpaka muda wa kufunga zoezi la kupiga kura, waliojitokeza walikuwa ni chini ya robo ya idadi ya wapiga kura wote katika maeneo waliyokuwa wakisimamia. Wamesisitiza kuwa asilimia 98 alizopata Rais Samia hazina ukweli wowote.
Wengine wametaja ripoti za wachunguzi wa kimataifa kama uthibitisho kuwa kura “ziliibiwa,” wakisisitiza kuwa matokeo hayo hayaakisi uhalisia wa sauti ya wananchi.
Polisi: MC Pilipili alishambuliwa na watu wasiojulikana
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limethibitisha kifo cha msanii na mtangazaji Emmanuel Mathias Matebe (maarufu MC Pilipili), aliyefariki Oktoba 16 katika Kituo cha Afya Ilazo baada ya kupokelewa akiwa katika hali mbaya. Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, MC Pilipili aliletwa na watu watatu wasiojulikana ambao walimkabidhi kwa msaidizi wake kisha kutoweka.
Kwa mujibu wa Polisi, uchunguzi wao umeonyesha kuwa marehemu alifariki kutokana na kushambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake, na wao Polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwakamata waliohusika na mauaji hayo ili kuwachukulia hatua za kisheria.
Maoni ya wananchi: Wengi wameonyesha kutoiamini taarifa hiyo ya Polisi wakihoji kama kuna watu walipiga simu, kwanini namba haijafuatiliwa, lakini pia gari walilokuwa nalo lina namba za usajili, kwanini taarifa hizo hazijafuatiliwa ili kuwapata watu hao na kuanza kuwahoji?
Aidha, wengine wameonyesha wasiwasi kuwa wa tukio hili la Pilipili halitofanyiwa kazi kama matukio mengine ya utekaji na mauji yaliyopita, ambapo ni tukio moja tu mpaka sasa (jaribio la utekaji wa Tarimo) waliohusika walikamatwa na kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa.
Wengine mitandaoni wamesema kuna taarifa zinazosema walinzi wa Waziri Mkuu (Mwigulu Nchemba) ndio wanahusika na mauji hayo, lakini wamehoji kama Polisi wana uwezo wa kwenda na kuwahoji walinzi hao ukizingatia kumekuwa na tuhuma za viongozi kuhusika na kusimamia magenge ya utekaji.
Wanaoshikiliwa kwa ‘Uhaini wakati wa Uchaguzi’ wanaendelea kusota Gerezani hadi Desemba 3, wazazi na walezi waomba waachiliwe kama Rais alivyoagiza
Watanzania kadhaa wanaokabiliwa na mashtaka ya uhaini kuhusiana na matukio ya uchaguzi wa Oktoba 29 bado wanashikiliwa mahabusu huku upelelezi ukiendelea. Mawakili wa utetezi wanasema jambo hili limezua wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya washtakiwa, na kesi zao, ikiwemo ya Paulina Palangyo na wenzake 25, Jennifer Jovin (Niffer) na wenzake 21, pamoja na watuhumiwa wengine 38, zimeahirishwa hadi kati ya Novemba 25 na Desemba 3, 2025.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa watuhumiwa hao wamejitokeza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu huku wakiomba ndugu zao waachiwe baada ya agizo la Rais Samia ambapo wengine wamesema ndugu zao walikamatwa wakiwa nyumbani na wala hawakutenda kosa lolote.
Maoni ya Wananchi: Wengi wanahoji kama Rais aliagiza wengine waachiwe, mbona hakuna waliyesikia ameachiwa? Je, ilikuwa ni kuwadanganya wananchi ili kuwatuliza hasira za watoto na ndugu zao kukamatwa?
Wengine wamesema hali hiyo inazidi kuchochea chuki kwa wananchi dhidi ya watawala na wamesisitiza kuwa imeacha maumivu kwa wengi na kusisitiza, ikiachwa - hakutakuwa na mwisho mzuri.
Rais Samia awateua Tido Mhando, Bakari Machumu na Razaro Nyalandu kwenye nafasi tofauti za uongozi
Rais Samia amemteua Bakari Machumu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, akichukua nafasi ya Sharifa Nyanga ambaye amepewa majukumu mengine. Machumu, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BSM Washauri (TZ) Limited, amewahi pia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).
Aidha, Rais Samia amemteua pia Tido Mhando kuwa Mshauri wa Rais, Habari na Mawasiliano, na Lazaro Samuel Nyalandu ameteuliwa kuwa Balozi.
Maoni ya Wananchi: Baadhi wamepongeza uteuzi wa Machumu, huku uteuzi wa Nyalandu ukionekana kama ulipaji wa fadhila baada ya kuonekana kwenye kampeni za Samia na mikutano ya dini akihimiza wananchi wamchague Samia.
Hata hivyo, kuna waliodokeza kuwa watu watatu waliowahi kuwa wahariri watendaji wa Mwananchi Communications (MCL) sasa wamepewa teuzi ndani ya CCM au Serikalini. Wahariri hao mbali na Machumu, ni Francis Majige Nanai na Denis Joe Msacky.