JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
CNN waachia ripoti ya uchunguzi wa mauaji wakati wa uchaguzi, wasema huenda kaburi la halaiki lipo katika Makaburi ya Kondo, Dar
Kituo cha Habari cha Kimataifa cha Cable News Network (CNN) kimeachia ripoti yake ya uchunguzi kuhusu mauaji ya raia wakati wa uchaguzi mkuu nchini Tanzania, ikibainisha kuwa polisi wa Tanzania walitumia risasi za moto na nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji wakati wa maandamano yaliyokuwa yakiendelea wakati wa uchaguzi na siku zilizofuata. Ripoti yao imeonyesha ushahidi wa picha, video, picha za satelaiti na kupitia mahojiano na watu kadhaa walioelezea hali ilivyokuwa wakati huo.
Ripoti hiyo pia inadai baadhi ya Madaktari waliowahoji, walisema walikatazwa na polisi kuwahudumia majeruhi waliokuwa wanafikishwa hospitalini kwaajili ya kupatiwa huduma, badala yake waliambiwa wawapeleke mochwari na wawaache huko wafe! Pia, CNN imeeleza kuwa video zinazoonyesha miili ya waandamanaji katika mochwari za Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza na Mwananyamala inayopatikana Dar es Salaam ni halisi.
Aidha, sehemu ya ripoti hiyo inadai uwepo wa kaburi la halaiki katika Makaburi ya Kondo, Kunduchi, mkoani Dar es Salaam, ambapo vijana waliiambia CNN kuwa walipewa kazi ya kuchimba sehemu hiyo kwaajili ya miili ya waandamanaji kuzikwa hapo. Japokuwa CNN haikuweza kuthibitisha moja kwa moja kuhusu hilo, picha za satelaiti zimeonyesha alama za sehemu hiyo kuchimbwa ambazo hazikuwepo kabla ya mauaji hayo kufanyika.
Maoni ya wananchi:
Wengi wameipongeza CNN kwa uchunguzi huo na kuzidi kuithibitishia Dunia juu ya yale yalifanywa na polisi pamoja na serikali ya Tanzania kwa wananchi waliondamana kupinga uchaguzi waliodai sio huru wala wa haki, pamoja na vitendo vya utekaji na watu kupotea nchini, na unyanyasaji kwa wapinzani na wanaokosoa serikali pamoja na uminywaji wa demokrasia. Wananchi wengine wanaamini hakutakuwa na namna ya serikali kukana yaliyotokea kwa kusema video zinazoonyesha miili ya watu waliokufa sehemu mbalimbali ni za kutengenezwa, kama ilivyokuwa imeelezwa na Polisi.
Wengine wamehofia kuwa kunaweza kutokea jitihada za kuficha ukweli, hivyo watatumwa watu kwenye makaburi ya Kondo na kuondoa miili iliyozikwa katika eneo hilo, japokuwa hata ikitokea hivyo haitasaida.
Aidha, wengine wamesema ripoti hii imezidi kuwapa hamasa ya kushiriki katika maandamno yanayotarajiwa kufanyika siku ya uhuru wa Tanganyika, Disemba 9 wakisema ‘wataikomboa nchi’.
Serikali: Tutahakiki Makala ya CNN kuhusu mauaji ya raia kabla ya kutoa tamko rasmi
Serikali ya Tanzania imesema inaendelea kufanya uchambuzi wa makala iliyochapishwa na Kituo cha Habari cha Kimataifa cha Cable News Network (CNN) kuhusu mauaji yaliyotokea wakati wa uchaguzi, kisha watatoa tamko baada ya uhakiki kukamilika. Hilo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.
Maoni ya wananchi:
Hatua hiyo imepokelewa kwa mitazamo tofauti. Baadhi ya wananchi wameonyesha kutokuwa na imani kama Serikali itatoa maelezo ya kina na ya wazi kuhusu yaliyotokea. Wameeleza kuwa kutokana na namna matukio mengine yalivyowahi kushughulikiwa katika nyakati zilizopita, hawatarajii kupata maelezo yanayojibu maswali muhimu ya umma.
Wananchi wengine wamesema wanaiona CNN kama chombo kikubwa cha habari chenye utafiti huru, hivyo wanaiamini zaidi katika utoaji wa taarifa kuhusu tukio hilo.
Wengine wamekejeli tamko hilo la serikali wakisema kuwa serikali haiwezi kuchunguza madai inayoshukiwa kuhusika nayo, hasa baada ya kusema uongo kuanzia maandamano yalivyoanza kuwa ni ‘vijana kutoka nje ndio wanaoandamana’. Pia wanasema ni kutokana na serikali kutokiri mpaka sasa kuwa waliouawa ni Watanzania walioandamana bila shinikizo kutoka taasisi za nje au kulipwa na mtu, bali kutokana na kutokubaliana na ukandamizaji wa haki nchini na uwajibikaji kukosekana kwenye masuala mengi serikalini.
Kwa upande mwingine, wananchi wameonyesha kuiamini zaidi CNN na vyombo vingine vya nje kusema ukweli katika ripoti zao kuliko serikali yao ambayo wanadai imekuwa ikijaribu kuficha ukweli na kupuuzia maumivu ya wananchi waliopoteza wapendwa wao hata baada ya uthiibitisho kuwa dhahiri kuwa ni polisi ndio waliofanya mauaji hayo.
Polisi: Tunaendelea kuchunguza matamko yenye kuashiria uvunjifu wa amani
Jeshi la Polisi limetangaza kuwa linafuatilia kwa ukaribu hali ya usalama nchini na litachukua hatua kwa yeyote atakayekiuka sheria, hasa ikijumuisha makundi na watu binafsi wanaotoa kauli zinazoashiria uchochezi, chuki au uvunjifu wa amani.
Polisi imeonya kuwa haitasita kuchukua hatua dhidi ya lugha yoyote, iwe laini au kali, yenye mwelekeo wa kuvuruga amani. Polisi imesisitiza kuwa matamko ya kuchochea chuki na vurugu yanahatarisha juhudi za maridhiano na utulivu wa taifa, na kwamba vurugu zikizuka, athari zake zitamgusa kila mwananchi katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kiusalama.
Maoni ya wananchi:
Wengi wamekosoa tamko la polisi wakisema linawalenga wananchi badala ya wahusika wakuu ambao ni viongozi wa dini ya kiislamu waliotoa kauli kali zenye kuchochea chuki za kidin. Mmoja wa viongozi wao alinukuliwa akisema watawakata vichwa waandamanaji na hajakamatwa wala kuhojiwa. Wananchi wanasema huu ni uonevu kwani kauli hizo wangetoa viongozi wa vyama vya upinzani au wananchi wanaokosoa serikali, basi wangekamatwa haraka na kupewa kesi za uhaini, ugaidi au uchochezi wa kuvunja amani nchini, ila kwakuwa viongozi hao wanaonekana kuwa upande wa Rais na serikali, basi wanaachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote.
Wengine wamesema hawatambui juhudi zozote za maridhiano zinazofanywa na serikali mpaka wawajibike na mauaji yaliyotokea wakati wa uchaguzi, kwani wao ndio wahusika wakuu.
Waziri Mkuu: Pesa za kununua vijana na kuwarundika zilitoka kwa wasioipenda nchi yetu, mabasi ya Esther sio yangu
Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba akiwa ziarani mkoani Singida, amewasihi wananchi kulinda amani na mshikamano wa kitaifa. Amesisitiza kuwa wengi wanaochochea vurugu na machafuko hawako nchini bali katika mataifa mengine; na mataifa jirani wanaifanyia Tanzania vurugu kwa kuwa imewazidi maendeleo hivyo ni wivu wa kiuchumi.
Aidha, amekana kuwa mmiliki wa mabasi yanayofanya safari zake mikoa ya Kaskazini – Esther, akisema hamiliki mabasi hayo na kwamba mabasi hayo hayana jina linalofanana na mke wake, kwani mkewe anaitwa Neema, lakini pia si jina la mama yake anaitwa Asha, akisema waliochoma mabasi hayo wakati wa maandamano wakidhani ni yake ni kutokana na watu kumsingizia na kusema uongo bila uoga.
Maoni ya wananchi:
Wengi wamehoji kwamba nchi jirani ndio zinateka na kuua wananchi na kufanya ubadhirifu nchini? Maana hayo na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu ndio zimewasukuma wananchi kuandamana, ukandamizaji ambao serikali na vyombo vyake imekuwa ikiwafanyia raia kwa muda mrefu!
Kuhusu magari ya Esther, wananchi wamehoji mbona mmiliki halali wa mabasi hayo hajatoka kuongea mpaka sasa? Kama sio mabasi yake, yeye anaongea kama nani? Wamesisitiza badala ya kujaribu kuwapoteza wananchi kuacha mjadala wa mauaji yaliyotokea nchini, serikali inatakiwa kuhakikisha wale wote waliohusika na mauaji wanawajibishwa.
Wengine wameenda mbali na kuja na Ushahidi kuonyesha nyaraka zinazoonyesha kuwa Neema Peter Thomas, ni Mmiliki mwenza wa mabasi hayo hivyo moja kwa moja kumhusisha mke wake.
IGP Wambura: Siasa, dini visitugawe Watanzania
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania, IGP Camillius Wambura, amewataka Watanzania wasikubali kugawanyika kwa misingi ya kisiasa, kidini au rasilimali na amewaomba washirikiane na Polisi kuhakikisha nchi inabaki salama.
Novemba 21, akiwa Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi, IGP Wambura alifunga mafunzo ya awali kwa askari wapya 4,826, akiwahimiza kutojihusisha na utendaji usiozingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi na akisisitiza kuwa kazi ya kulinda raia na mali zao ni jukumu la kipekee Duniani kote, na kwamba linahitaji uzalendo, utii, nidhamu na ujasiri ili kutekelezwa kwa ufanisi.
Maoni ya Wananchi:
Wengi wamekosoa vikali suala la utekaji, mauaji na watu kupotezwa huku Polisi wakiwa washukiwa wakubwa hasa kutokana na uzembe wa kufuatilia matukio hayo na kuwakamata wahusika, wakisisitiza siasa wala dini haziwezi kuwagawa Watanzania, lakini inapokena haki na uwajibikaji hakuwezi kuwa na amani.
Wengine wamesema ingekuwa nchi nyingine, Wambura alitakiwa awe amejiuzulu huku uchunguzi dhidi yake na viongozi wengine wa jeshi hilo ukiendelea kutokana na mauaji ya raia yaliyofanywa na jeshi hilo wakati wa uchaguzi chini ya uongozi wake.
Aidha, wengine wamesema jeshi hilo limekuwa la kuua raia badala ya kulinda raia, kutokana na mauaji wakati wa uchaguzi na vitendo vya utekaji vinavyoendelea kufanyika mpaka wakati huu, na kwamba suluhisho pekee ni kulifumua jeshi hilo, kuhakikisha linaundwa upya likifuata misingi ya uwajibikaji na kuajiri vijana wanaokidhi vigezo vya kitaaluma na si matumizi ya nguvu au ukatili.
Wananchi waendelea kuhamasishana na kuelimishana kutokubali kugawanywa kutokana na imani zao
Katika mitandao ya kijamii, wananchi wameendelea kutoa mawazo yao wakipinga suala la chuki za kidini na kuhasishana kuwa Watanzania bila kujali imani zao ni ndugu.
Salamu za utani zinazohusisha imani ya Kikristo na Kiislamu, ‘challenge’ za mtandaoni, nyimbo za dini zimekuwa zikitumika kwa wingi na watanzania wenye imani tofauti kuonyesha kuwa wao ni ndugu na hakuna anayeweza kuja kuingiza chuki na kufanya wabaguane sababu ya imani wala itikadi zao za kisiasa na kuacha kudai haki na uwajibikaji nchini pale serikali inapotenda kinyume na matarajio ya wananchi.