JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
Serikali yavitaka vyombo vya habari vya nje kutozingatia weledi na taratibu za uandishi, yasisitiza nchi ipo salama
Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, amesema serikali ya Tanzania imesikitishwa na ongezeko la vyombo vya habari vya kimataifa kuchapisha taarifa zinazoegemea upande mmoja kuhusu matukio yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa 2025.
Akizungumza Novemba 23, katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam, Msigwa amesema baadhi ya vyombo hivyo, vikiwemo CNN, Al Jazeera, BBC na DW vimechapisha habari zenye tuhuma bila kuipa serikali nafasi ya kujibu, jambo alilolieleza kuwa ni kukiuka maadili na misingi ya uandishi wa habari.
Amesema uhakiki wa makala ya CNN unaendelea na kubainisha kuwa si kweli chombo hicho kilishindwa kupata upande wa serikali. Amevitaka vyombo vya habari vya nje kufuata vyanzo rasmi na kuzingatia usawa, haki na uwajibikaji ili kuepusha taharuki.
Msigwa ameongeza kuwa, serikali, akiwemo Rais Samia, imesikitishwa na kuumizwa na matukio yaliyotokea wakati wa uchaguzi, na kuendeleza majadiliano yanayochochea hasira hakutaleta manufaa kwa taifa.
Aidha, amesema serikali ipo tayari kusikiliza maswali na ushauri kutoka kwa umma, huku akisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi vinaendelea kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao. Amewahakikishia watalii kuwa Tanzania inabaki kuwa nchi salama na huru kupokea wageni, akiwataka kupuuzia taarifa potofu.
Kuhusu takwimu za vifo na majeruhi, Msigwa amesema wanaozitoa bila mamlaka ni wachochezi kwani takwimu sahihi zinapaswa kutoka kwa serikali baada ya tathmini ya kina.
Aidha, Msigwa amewapongeza waandishi wa Habari wa ndani, kwa kuweka mbele maslahi ya taifa (uzalendo) na kuwataka kutoogopa mashambulizi kutoka mtandaoni. Amewahakikishia kuwa serikali itahakikisha vyombo vya habari vya Tanzania vinafanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa.
Kuhusu maandamano yaliyopangwa Desemba 9, Msigwa ametoa rai kwa vijana kutofuata mkumbo wa vitendo vinavyoweza kuharibu amani, akisisitiza kuwa serikali imejipanga kulinda usalama wa raia na mali zao. Ameongeza kuwa, taarifa kuhusu maadhimisho ya Uhuru zitatolewa ndani ya siku mbili.
Hata hivyo, Larry Madowo, mwandishi wa CNN aliyetayarisha ripoti ya uchaguzi kwa kushirikiana na wenzake amesema hakupewa mwaliko kwenye mkutano huu wa serikali na vyombo vya Habari, hata kama serikali wana mawasiliano yao, na kusisitiza serikali haikutoa ushirikiano walipowatafuta kuhusu ripoti ya uchunguzi waliyoiandaa.
Maoni ya wananchi:
Wengi wamepinga ufafanuzi wa serikali kuwa vyombo hivyo vya habari vimeripoti upande mmoja, wakisema vyote vilisema vimeitafuta serikali lakini hawakuwa tayari kuzungumza nao. Wananchi wanaamini vyombo vyote hivyo haviwezi kusema uongo kuhusu hilo. Wanadai wanajua serikali pale inapotokea wanatakiwa kutoa majibu kwa maswali magumu, hata kwa matukio mengine wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano.
Wengine wamesema kwa serikali kupinga namna vyombo hivyo vilivyotoa taarifa na sio kupinga maudhui yaliyoripotiwa, inathibitisha kuwa yote yaliyosemwa ni kweli, na kinachotakiwa sasa ni uwajibikaji kwa wote waliohusika.
Baadhi wamesema vyombo hivyo vimepata nafasi ya kufanya uchunguzi huo kwasababu wamekuwa kimbilio la mwisho kwa wananchi baada ya kukosa majibu kutoka kwa serikali toka mauaji yalipotokea. Wanasema hata tume ya uchunguzi imeundwa kutokana na msukumo kutoka nje, vinginevyo serikali ingekaa kimya na kuendelea na shughuli zake kanakwamba hakuna kilichotokea.
Aidha, wengine wameendelea kuvipongeza vyombo vya habari vya nje kwa kuendelea kuripoti matukio yaliyotokea wakati wa uchaguzi na kufichua ukweli ambao serikali imejaribu kuuficha ili kukwepa uwajibikaji kwani vyombo vya ndani vinanyimwa uhuru wa kufanya hivyo. Ingawa Msigwa alisema vyombo vya ndani vinafanya kazi kwa ‘uhuru’, wananchi wanadai kuwa vyombo vya nje kutoalikwa kwenye mkutano wake ni sababu wote walioalikwa wanadhibitiwa na serikali na wanatarajiwa kutouliza chochote ambacho kitawaweka serikali kwenye nafasi mbaya tofauti na kina CNN ambao wana uhuru kwenye kazi zao.
ACT-Wazalendo wafungua kesi kupinga ushindi wa Baba Levo
Wanachama wa ACT-Wazalendo Jimbo la Kigoma Mjini wamefungua kesi kupinga ushindi wa Mbunge Clayton Chipando (Baba Levo), wakidai matokeo ya uchaguzi yalichakachuliwa.
Wamesema matokeo ya awali matokeo yalionesha Baba Levo kupata kura 35,725 dhidi ya 16,619 za Zitto Kabwe huku Samia akitangazwa kupata kura 85,000 ambapo watu walihoji hilo liliwezekana vipi wakati kura za wabunge hazikufikia hata elfu 60. Ili kuhakikisha matokeo hayo ya wabunge yanaendana na ya Samia, kura za Baba Levo na Zitto ziliongezwa na kuwa 50,000 na 35,000 mtawalia.
Katika mkutano na waandishi wa habari Novemba 23, wanachama hao walimtuhumu Baba Levo kutumia nguvu na vitisho kwa kushirikiana na Polisi kuwakamata mawakala wa ACT-Wazalendo.
Aidha, wamedai kuwa Uchaguzi wa Oktoba 29 ulijaa uchafuzi, uhuni, udanganyifu, uonevu, ubabe, hujuma, vitisho, uporaji, utemi na unyangaji dhidi ya haki na uhuru wa wananchi kuchagua viongozi wanaowataka, kwani mawakala wao walizuiliwa kuingia na daftari la INEC lenye picha za wapiga kura wote kituoni ili wasiweze kuwatambua watu walioongezwa kupiga kura kituoni hapo kinyume na sheria.
Maoni ya wananchi:
Wananchi wengi wameshangaa wanachama wa ACT-Wazalendo kulalamika kuhusu kuibiwa kura wakati katika kampeni zao waliwahakikishia Watanzania kuwa watalinda kura Oktoba 29 hata baada ya kuonywa kuwa hata iweje CCM lazima wacheze rafu, huku wakiwaambia waache kuzua taharuki kwani watu wana mambo ya msingi ya kufuatilia wakati huu.
Polisi: Paroko wa Parokia ya Ngaruka, Padre Josephat Misigaro na wananchi wengine wawili hawajatekwa
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limekanusha taarifa zinazosambaa mtandaoni zikidai Padri Josephat Misigaro na wananchi wawili, Vedasto na Selule, wametekwa na watu wasiojulikana, likieleza kuwa madai hayo hayana ukweli.
Kwa mujibu wa Kamanda ACP Philemon Makungu, Padri Misigaro ‘aliitwa tu’ kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kijinai tarehe Novemba 20 na kuachiwa huru siku hiyo hiyo, huku Polisi wakisema hakuna taarifa yoyote waliyopata kuhusu kupotea kwa Vedasto au Selule.
Polisi wamewataka wananchi kubaki watulivu wakati uchunguzi juu ya waliotoa taarifa hizo za upotoshaji ukiendelea, na wameonya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuhusika kusambaza taarifa zisizo sahihi.
Maoni ya wananchi:
Wengi wamekosoa jinsi Polisi inavyoshughulikia matukio ya utekaji na watu kupotea, wakisema Polisi hujitokeza kukanusha madai ya kutekwa pale wananchi wakipaza sauti baada ya kuwa walionekana wakimkamata muhusika. Wanahoji, kwanini taratibu hazifuatwi kama wao sio wahalifu wanaoteka watanzania? Kwanini waende kama wezi na kuja kujitambulisha baada ya kuwa watu kuanza kumtafuta mpedwa wao wakidhani ametekwa?
Aidha wengine wamesema matukio ya watu kutekwa na kupotea yamekuwa kawaida nchini, kiasi kwamba watu hawashtuki tena, jambo linalotia mashaka kuhusu usalama wa nchi na maelendeleo yake kwa ujumla. Wengine wanaona nchi imekuwa kama genge la wahalifu na yeyote anaweza kuamua kufanya chochote bila kuwajibishwa!