JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
Watuhumiwa 202 wa kesi ya uhaini waachiwa huru Dar na Arusha, 18 warudishwa rumande
Watuhumiwa 198 kati ya washtakiwa 216 waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhaini, kufuatia maandamano wakati wa Uchaguzi, wameachiwa huru leo Novemba 25, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, baada Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na mashauri yao.
Kati ya washtakiwa waliorudishwa rumande, ni mfanyabiashara Jenifer Jovin (Niffer) na Mika Lucas Chavala, Muuandaji wa kipindi cha Swahili Nation (SN), ambapo sababu za kutoachiwa kwao hazikuwekwa wazi.
Kwa upande wa Arusha, Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani humo iliwaachia huru na kuwafutia mashtaka ya uhaini washtakiwa wanne akiwemo Mwandishi wa Habari, Godfrey Ng’omba, pamoja na vijana watatu wa kiume wenye umri wa miaka 13, 16 na 17, baada DPP kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka hayo. Hii inafuatia hatua ya jana Novemba 24, ambapo washtakiwa wengine 24 waliachiwa mkoani humo, chini ya uangalizi wa mwaka mmoja na kupewa masharti ya kuripoti polisi kila mwezi.
Maoni ya wananchi: Wengi wamechukulia hatua hiyo kama namna ya kupunguza makali ya maandamano yanayodaiwa kupangwa kufanyika Desemba 9 kwa kuonyesha kuwa serikali inawajali na ina huruma. Wengi wa vijana mitandaoni wanasema hilo halitawafanya waache kwenda kwenye maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika siku ya uhuru hasa baada ya kuwa baadhi yao kama Niffer, kurudishwa rumande.
Baadhi wamekosea ukimya wa mmiliki wa Ayo TV, Millard Ayo katika kipindi chote ambacho mfanyakazi wake alikamatwa na kufunguliwa mashtaka hayo, wakisema anachojali ni yale anayopata kutoka kwa serikali pamoja na viongozi pale anapofanya kazi ya kuwasafisha machoni pa wananchi, na sio hali ya wafanyakazi
Wanasheria wamfungulia Samia mashtaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC)
Muungano wa kimataifa wa wanasheria na makundi ya haki za binadamu umeiomba rasmi mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC) kumchunguza rais wa Tanzania, Samia Suluhu, pamoja na maafisa wake wa ngazi za juu, kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu zinazodaiwa kutokea wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, ikiwemo vifo vya raia wakati wa maandamano ya baada ya uchaguzi.
Hatua hii inakuja juma moja baada ya Rais Samia kuzindua Tume ya Uchunguzi kuhusu vurugu hizo, akiwatuhumu wapinzani na asasi za kiraia za ndani na nje ya nchi kwa kusababisha machafuko hayo.
Kwa upande mwingine, Kamati ya Mahusiano ya Nje ya Seneti ya Marekani, kupitia seneta Jeanne Shaheen, imeeleza wasiwasi mkubwa juu ya mauaji na ukatili wa Polisi wakati wa uchaguzi Tanzania. Ikirejea uchunguzi wa CNN ambao pia umeonyesha ushahidi wa kaburi la halaiki linaloashiria jaribio la kuficha ukiukaji wa haki za binadamu, kamati imeagiza uchunguzi huru ufanywe mara moja.
Maoni ya wananchi: Wengi wameonyesha furaha na matumaini kuwa haki inaenda kuanza kutendeka kwa wote waliohusika kwenye mauaji na matukio mengine ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyotokea wakati wa uchaguzi, wakishukuru vyombo vya habari vya nje kupaza sauti za Watanzania na kuonyesha uhalisia wa yalitokea.
Aidha, wengine wamependekeza mbali na kukemea yaliyotokea nchini na kutoa matamko, viongozi wa serikali wawekewe vikwazo kama vile vya kuingia kwenye nchi zao pamoja na mali zao kuzuiwa kama njia ya kuongeza shinikizo kwao kuchukua hatua za kiuwajibikaji dhidi ya wote waliohusika na mauaji hayo.
Mwigulu: Vurugu za Oktoba 29 zilichochewa na wanaoishi nje, waandamanji walikuwa na silaha hawakuongea kishwahili. Hatuwezi kutoa idadi ya waliouwa, tutalinda rasilimali za Tanzania kwa nguvu zote
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini, Novemba 25, jijini Dar es Salaam, amesema vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi zilisababisha vifo vya raia na Polisi, na uharibifu mkubwa wa mali. Ametoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu na kusisitiza kuwa “kumwaga damu ya mtu asiye na hatia si baraka nchini.”
Amesema, maandamano hayo hayakuwa ya kawaida kwani washiriki walikuwa na silaha za kutosha na hawakuongea Kiswahili jambo linaloashiria uwepo wa raia wa kigeni, akidai uchochezi ulitoka kwa watu wanaoishi nje ya nchi wanaolipwa kuharibu Tanzania.
Ametahadharisha kuwa Serikali itatumia nguvu na rasilimali zote kulinda Usalama wa Taifa, huku akibainisha kuwa hawawezi kutaja idadi ya waliofariki kwa sasa kwani watu bado wanaomboleza na wana machungu kupoteza wapendwa wao; na kutaja idadi hiyo inakuwa kama kusheherekea vifo hivyo.
Mwigulu amesisitiza kuwa tume ya uchunguzi, inayoongozwa na Jaji Mstaafu Mohamed Chande, imebobea kwenye sheria na haki na inaongozwa na ‘wazee wenye uzoefu’ kwenye kazi hiyo, hivyo Watanzania waunge mkono juhudi za Rais Samia katika maridhiano kurejesha utulivu.
Mwigulu ametoa wito kwa wananchi kutoingia kwenye mtego wa kuharibu nchi kwa kuwapa nafasi wale wenye nia ovu ya kuharibu uchumi wa Tanzania (Economic Sabotage) na pia kutojihusisha katika mipango ya maandamano ya Disemba 9, 2025 na kuendelea kutoa onyo kwa watumishi wa umma wazembe na wala rushwa kushughulikiwa.
Japokuwa Mwigulu hakutaja idadi ya waliopoteza maisha wakati wa maandamano, alitoa tathmini ya awali ya uharibifu uliotokea, akisema Ofisi za Serikali 756, Vituo vya Mwendokasi (BRT) 26, Vituo vya Polisi 159, Vituo vya mafuta 672, magari binafsi 1,642, Pikipiki binafsi 2,268 na Magari ya Serikali 976 yalichomwa moto.
Aidha, wahariri walipata nafasi ya kuuliza maswali kwa Waziri Mkuu, na kati ya maswali yalioulizwa lilikuwa ni kuhusu matukio ya utekaji nchini, Polisi kupewa amri ya kuua raia, idadi ya vifo wakati wa uchaguzi pamoja na wananchi kunyimwa miili ya wapendwa wao waliofariki wakati wa uchaguzi. Majibu yalitolewa na Waziri Mkuu japokuwa hakujibu moja kwa moja yale yaliyoulizwa.
Maoni ya wananchi: Wengi wamelalamika kuwa kitendo cha kutaja uharibifu wa mali bila idadi ya vifo kwa kisingizio cha ubinadamu na huruma kwa waliopoteza wapendwa wao ni namna ya kupunguza uzito wa ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika. Pia, wamesema kutaja idadi kubwa ya vitu vilivyoharibiwa inaashiria kuwa takwimu zimepikwa ili kuhalalisha ‘uovu’ wa maandamano na kuondoa uwezekano wa maandamano mengine mbeleni kuungwa mkono na wananchi.
Aidha, kuna waliosifia wahariri kwa kumbana Waziri Mkuu na maswali magumu, ingawa kuna baadhi wamehisi wahariri hao walipangwa kuuliza maswali hayo huku Mwigulu akiwa mejiandaa na majibu yenye hisia ili kuwashawishi wananchi kuwa kweli ana uchungu wakati muda wote wamekuwa wakikwepa kuongelea utekaji na vifo vilivyotokea wakati wa uchaguzi na kuonyesha uharibifu wa mali ni muhimu zaidi.
Kitendo cha wahariri wote kuuliza maswali magumu kwa wakati mmoja imeonekana kuwa timilifu sana, na hivyo kukosa uhalisia. Wamedokeza ni jana yake tu, mwandishi kutoka kituo cha Clouds TV aliweka bayana kuwa wengi walishidwa kuripoti matukio wakati wa uchaguzi kutokana na kuogopa kupoteza kazi ama vyombo vyao kufungiwa, hivyo maswali ya wahiriri yanaonekana kama njia ya serikali kujisafisha kuwa vyombo vya habari vinafanya kazi kwa uhuru na kwamba wanaweza kuuliza hata maswali magumu na serikali ikatoa mrejesho bila shida yoyote.
Tanzania: Bunge la Ulaya halitendi haki kujadili mauaji wakati wa uchaguzi na kufungwa kwa Lissu bila ya kutupa nafasi ya kusikilizwa
Serikali ya Tanzania imetuma malalamiko kwa Bunge la Ulaya kuhusu mpango wa kufanya kikao kitakachojadili mauaji ya baada ya uchaguzi, kuzorota kwa haki za binadamu nchini, na kesi ya kiongozi wa upinzani Tundu Lissu, bila kuipa serikali nafasi ya kutoa maelezo.
Serikali imesisitiza Mkataba wa Samoa unaotaka mazungumzo kabla ya hatua zozote kuendelea, ikisisitiza haki ya kusikilizwa kwa upande husika. Aidha, imesema tayari imeanzisha Tume ya Kitaifa kuchunguza matukio hayo na kuwahakikishia juu ya demokrasia na utawala wa sheria.
Ubalozi wa Tanzania umeomba kikao cha Bunge la Ulaya kipangwe upya ili Serikali ipate fursa ya kuwasilisha msimamo wake na iwapo ratiba haitaruhusu, imeomba wabunge waruhusu Serikali kusikilizwa wakati wa kikao kijacho.
Maoni ya Wananchi: Wengi wamesema kama serikali haiwasikilizi wala kuwalinda raia, kwanini wao wapewe nafasi ya kusikilizwa? Na kuongeza kuwa wananchi wamekuwa wakisisitiza HAKI wakati wote lakini walikuwa wanaambiwa amani ndio inaleta haki, na kama huo ndio kweli basi na wao wasiombe haki, bali wasisitize Bunge la ulaya kuwa na amani.
Aidha wengine wamewasihi Bunge hilo kutosikiliza hoja za Tanzania kuhusu kuanzishwa tume ‘huru’ ya uchunguzi, kwani tume hiyo imejaa viongozi wa CCM pamoja na waliokuwa viongozi wa serikali ya nyuma ambao nao ni sehemu ya tatizo kwenye mfumo wa haki nchini, hivyo matokeo ya tume hiyo hayatakuwa ya haki, huru ama ya kuleta uwajibikaji kwa wote waliohusika kwenye mauaji wakati wa uchaguzi.