JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
OCD Chunya: Vituo vya Mafuta msiwauzie bodaboda na bajaji zaidi ya lita 2 za petroli
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Chunya, OCD Nestory John, ametoa agizo kwa vituo vya mafuta kutowauzia madereva wa bodaboda na bajaji zaidi ya lita mbili za petroli kwa siku kuelekea Disemba 9, akidai wengi wao hutumia mafuta hayo kuchoma na kuharibu miundombinu.
Amenukuliwa akisema hatua hiyo inalenga kudhibiti usalama kwa kuwa mafuta mengi huwapa hamasa na uwezo wa kusafiri na kutekeleza uhalifu. Pia, aliwataka wamiliki wa vituo vya mafuta kuongeza ulinzi wa askari wenye silaha pamoja na kufunga CCTV zitakazosaidia kubaini wahalifu hao.
Baada ya kauli hiyo kusambaa mtandaoni, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, DCP David Misime limetoa taarifa kwa umma likikana agizo hilo na kueleza kuwa linafanya uchunguzi kubaini ukweli wa taarifa hiyo. Limesema, OCD hana mamlaka ya kuita waandishi wa habari na kutoa taarifa ya aina hiyo, na kwamba endapo uchunguzi utathibitisha hilo, hatua stahiki zitachukuliwa mara moja.
Maoni ya wananchi: Wengi wamesema taarifa hiyo ilikuwa ya kweli lakini OCD alikosea kuitoa taarifa hiyo mapema, kwani inaonekana ilipangwa kutolewa siku chache kabla ya maandamano ili kuhakikisha wanadhibiti kundi hilo; ili kupunguza hasira za wananchi ikawabidi Polisi kutoka mbele kukana taarifa hiyo.
Wengine wameiona taarifa hiyo ya Polisi kuwa hata kama wamekana, imewafumbua macho juu ya mipango yao na hivyo kuwapa faida ya kujipanga zaidi na kuhakikisha mipango ya kuandamana siku hiyo haiharibiki.
Aidha, wengine wameona taarifa hiyo kama mpango wa kuendeleza propaganda kuwa maandamano yanayopangwa kufanyika Disemba 9 yatakuwa ya vurugu pamoja na uharibifu wa mali, hata kama wananchi wamesema mara nyingi kuwa ni ya amani na wanaendelea kuelimishana kutofanya vurugu pamoja kubeba mabango yenye jumbe mbalimbali.
Wanasema vyombo vya ulinzi pamoja na serikali vinafanya hivi ili, waje kuharibu mali na kuua raia kisha kuwasingizia wananchi na kupata uhalali wa kuzuia maandamano nchini.
Waziri: Waliokamatwa kwa kesi ya Uhaini wakati wa uchaguzi ni zaidi ya 2,045; watakaochiwa ni 1,736
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera, amesema zaidi ya watu 2,045 walikamatwa nchini wakati na baada ya vurugu za maandamano zilizotokea kwenye uchaguzi.
Kwa mujibu wa maelezo yake, kati yao, 1,736 wataachiwa kufuatia msamaha wa Rais Samia alioutoa Novemba 14, 2025 wakati akizindua Bunge la 13 jijini Dodoma kwa kumuagiza DPP kuchambua wanaostahili kuachiwa huru baada ya kufuata mkumbo kuandamana, huku 309 wakibaki chini ya ulinzi.
Dkt. Homera ametoa takwimu hizo leo Novemba 26, 2025 alipotembelea Ofisi ya DPP jijini Dodoma, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Maoni ya Wananchi: Wengi wanasema hakuna msamaha uliotelewa kwani waliokamatwa hawakuwa na kosa lolote bali ni mbinu ya Serikali kukwepa uwajibikaji kwa kutowakamata hasa wale walioua raia wakati wa maandamano.
Wengine wamelalamikia madaraka makubwa ya Rais na DPP yanayowawezesha kuamua nani akamatwe akasote gerezani na nani aachiwe. Wanadai madaraka hayo yamekuwa yakitumika vibaya kuwataabisha viongozi wa upinzani na wakosoaji wakubwa wa Serikali.
Aidha, wengine wametabiri hali mbaya zaidi kutokea Disemba 9 ikiwa wananchi wataendelea kupuuzwa. Wengi wana hasira ya kupoteza wapendwa wao, na walioachiwa wameunda urafiki gerezani ambao unawaunganisha na kuwapa motisha ya kushirikiana ili kufanikisha malengo yao. Hii inaelezwa kuwa inaweza kuongeza hamasa ya wananchi kushiriki kwa wingi kwenye maandamano yajayo, na kama Polisi watatumia nguvu kama ilivyokuwa Oktoba 29, huenda vifo vikawa vingi zaidi.
Mwigulu: Hata nikiwa Waziri Mkuu wa wiki moja ni sawa, sitoruhusu nchi ya mabwana na matwana
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba amejibu kauli ya mwanaharakati ‘Evarist Chahali’ aliyedai kuwa atakuwa Waziri Mkuu wa muda mfupi zaidi kuwahi kutokea, akisisitiza kwamba hata akihudumu kwa wiki moja ni sawa, lakini kwenye wiki hiyo moja hataruhusu Tanzania kuwa na sheria zinazowalinda watu wa daraja la juu na kuwakandamiza wa daraja la chini.
Amesema hatakubali nchi kuwa ya “mabwana na watwana” na kwamba ataendelea kuwawakilisha wananchi wa chini kwa kuwa wao ndio anaishi nao na hata watakaomzika, akisisitiza hakuna aliyewahi kuona kaburi likichimbwa na waliovaa suti!
Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo leo Novemba 26, 2025, katika maadhimisho ya kwanza ya Wiki ya Usafiri Endelevu Ardhini yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Maoni ya Wananchi: Wengi wamesema hao wananchi masikini anaojiapiza kuwatetea dhidi ya wakandamizaji hawakumchagua, sio waliompa nafasi ya ubunge bali hao mabwana anaosema atapambana nao ili kuondoa madaraja.
Wengine wamekebehi mtindo wa Waziri Mkuu kufanya mikutano karibu kila siku kama njia ya kuonyesha anawajali wananchi. Wananchi wanakisisitiza kama hakutakuwa na uwajibikaji kwa matukio yaliyotokea wakati wa uchaguzi basi maandamano mengine yananukia.
Dodoma: Mbunge aagiza viongozi wa mitaa kufuatilia wageni wanaoingia na kuondoka kuelekea Disemba 9
Kufuatia taarifa za mpango wa maandamano ya awamu ya pili yanayotarajiwa kufanyika Desemba 9, Mbunge wa Dodoma Mjini, Paschal Chinyele, ametoa wito kwa viongozi wa Serikali za Mitaa pamoja na wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuimarisha ufuatiliaji wa wageni wanaoingia na kutoka katika maeneo yao. Amesema wanaofanya vurugu na kuchoma miundombinu ni wageni wanaotumwa na wanaharakati ambao wao pamoja na familia zao wapo nchi za nje, akisisitiza hilo halitakiwi kutokea.
Amesema, hatua hiyo inalenga kuzuia kurudiwa kwa vurugu kama zile zilizojitokeza Oktoba 29, na kuhakikisha usalama wa jiji na taifa kwa ujumla.
Chinyele amewataka viongozi hao kutoa taarifa Polisi mara wanapowatilia shaka baadhi ya wageni, ili waweze kuchukua hatua mapema.
Maoni ya wananchi: Wengi wamekosoa namna viongozi wanavyosisitiza waliofanya ‘vurugu’ ni wageni wakijua fika walioandama ni wananchi kutokana na kukosekana uwajibikaji pamoja na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, jambo linalowaongezea hasira zaidi kwa kuona wanapuuzwa.
Wengine wamesema bila Serikali kushughulikia chimbuko la matatizo linalowafanya wananchi waandamane, basi suluhu haitapatikana, badala yake wananchi watatumia njia wanayoijua kuhakikisha haki inapatikana, na hatua hii huenda ikaleta madhara makubwa.