JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
Bunge la Ulaya lapiga kura ya ndiyo kuzuia misaada Tanzania, lataka Lissu aachiwe
Bunge la Ulaya limeitaka Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya (EU Council) kusitisha ufadhili kwa Serikali ya Tanzania na kuagiza fedha za misaada zielekezwe kwa asasi za kiraia, wanahabari, na watetezi wa haki za binadamu, huku likisisitiza wote waliohusika katika ukandamizaji wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi kuwekewa vikwazo.
Aidha, Bunge hilo limeishutumu Serikali ya Tanzania kwa ukandamizaji wakati wa uchaguzi, ikiwemo vifo, majeruhi, mamia kukamatwa, na taarifa za uwepo wa makaburi ya halaiki. Limesema, Serikali iache mara moja kuwakamata wapinzani, waandishi wa habari, na watetezi wa haki za binadamu, na kumwachilia huru Kiongozi Mkuu wa Upinzani, Tundu Lissu, pamoja na kurejesha huduma za mtandao pamoja na vyombo vya habari vilivyozuiliwa.
Zaidi, Bunge hilo limeitaka Tanzania kuanzisha uchunguzi huru na wa kimataifa, unaoongozwa na Afrika, juu ya mauaji, mateso na kupotezwa kwa watu, na kuanza majadiliano jumuishi kati ya serikali, upinzani, asasi za kiraia, na wawakilishi wa waathirika, ili kuwezesha uchaguzi mpya, huru, na wenye uwazi.
Maoni ya Wananchi: Wengi wameunga mkono kusitishwa kwa misaada wakisema mikopo hiyo haijawahi kuwanufaisha wananchi na kwamba mbali na kutumika kwa maslahi ya viongozi, ndizo zilizotumika kulipa vyombo vya ulinzi vinavyodaiwa kuhusika na ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi.
Aidha, wengine wamesema kufuatia Ulaya kusitisha misaada, mataifa mengine yanatakiwa kufuatia ili kuongeza msukumo kwa serikali kuwajibika. Wengi wanasubiri kuona serikali itachukua hatua gani baada ya uamuzi huo wa Bunge la Ulaya!
Mwabukusi: Kutisha mawakili wanaotoa msaada wa kisheria ni kubaka na kunajisi mfumo wa utoaji haki
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, kupitia ukurasa wake wa X leo Novemba 26, 2025, amekosoa kile alichokiita utepetevu wa vyombo vya maamuzi na kuvurugika kwa misingi ya demokrasia, uwajibikaji na utawala wa sheria, akisema ndiyo chanzo cha sintofahamu na kupotea kwa matumaini miongoni mwa vijana.
Ameonya dhidi ya vitisho kwa mawakili wanaotoa msaada wa kisheria, akisisitiza kuwa hatua hizo ni kuingilia na kudhoofisha mfumo wa utoaji haki. Mwabukusi amesema vijana wa Gen Z wana hoja zenye msingi wa kisheria na kikatiba, na ametoa wito wa kurejea kwenye ukweli, haki na uwajibikaji kuhusu kilichotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi ili nchi ipone na kurejea kwenye misingi ya utawala wa sheria.
Amezitaka mamlaka kuepuka propaganda na badala yake kufanya tathmini ya kitaalamu ya sababu zilizoliweka taifa katika hali ya sasa.
Maoni ya wananchi: Wengi wamempongeza Mwabukusi kwa jitihadi zake kuhakikisha haki inapatikana kwa wote waliobambikiwa kesi ya uhaini, wakisema serikali kuanza kuwatisha mawakili hao inamaanisha wameishiwa mbinu za kujitetea na hivyo wanatumia mbinu yoyote kuhakikisha wanakwepa kuwajibika, hali inayofanya wazidi kufanya makosa zaidi.
Golugwa: Serikali imeshindwa kukiri na kusema ukweli juu ya Maafa ya Oktoba 29
Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Amani Golugwa, amerejelea Kauli za Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu wakati wa Mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari amesema Serikali imeshindwa kueleza ukweli kuhusu tuhuma za uwepo wa makaburi ya halaiki na kutoeleza idadi ya waliofariki na kudai maelezo yake yamepuuza maumivu ya familia zilizopoteza ndugu.
Amesema matukio ya utekaji, watu kupotea na raia kuuawa yanaashiria serikali kushindwa kuchukua hatua au kukubali lawama, na amesisitiza kuwa tume huru ya kimataifa ndiyo inaweza kufichua ukweli kwa sababu, kwa mujibu wake, Serikali haiwezi kujichunguza yenyewe. Ametoa kauli hiyo leo Novemba 27 akisema wananchi wanataka majibu sahihi juu ya matukio ya ukosefu wa usalama na vifo vinavyodaiwa kutokea kwenye maandamano wakati wa uchaguzi.
Pia, Golugwa amesema Mwigulu alikiri kimyakimya kuwa askari walifyatua risasi bila utaratibu dhidi ya raia wasio na silaha. Ameeleza kuwa maswali ya waandishi likiwemo lile la maandalizi ya maandamano ya Desemba 9 ambapo moja ya chombo cha habari kiliondoa maudhui hayo yanaonyesha ukosefu wa uhuru wa vyombo vya habari, huku akiwapongeza waandishi kwa kuwasilisha hoja ambazo wananchi wamekuwa wakitaka majibu yake.
Golugwa ametoa wito kwa Serikali kuratibu mchakato wa Katiba Mpya na siyo kupotosha umma kuwa tayari kuna reforms zimefanyika, na kuitaka Serikali kusikiliza sauti za wananchi na kuwa Tanzania haiwezi kujengwa juu ya uongo na kufunika ukweli kwa maafa yaliyotokea.
Maoni ya wananchi: Wengi wameunga mkono hoja za CHADEMA wakieleza kuwa Mwigulu hakuwa na majibu kama ilivyokuwa kwa viongozi wengi serikalini na kwamba kinachofanyika sasa ni kushawishi wananchi ili waachane na mpango wa kuandamana mwezi Disemba.
Augustino Polepole: Humphrey Polepole aachiwe ndani ya saa 24, la sivyo nitalipiza
Kaka wa Humphrey Polepole, Augustino Polepole ametoa saa 24 kwa ndugu yake kuachiwa na kupelekwa nyumbani kwa mama yake Tabata Segerea, Dar, vinginevyo atalipiza kisasi kwa wote aliowatuhumu kuhusika na tukio hilo ambao amekuwa akiwataja mara kwa mara.
Ametoa angalizo kwa Rais Mstaafu Kikwete na mtoto wake Ridhiwani, Rais Samia, IGP, Mafwele na wengine kuongeza ulinzi maana safari hii hatarudi nyuma na atahakikisha analipa kisasi ikiwa ndugu yake hatorudishwa akiwa mzima.
Maoni ya wananchi: Wengi wanasema Augustino amekuwa anatoa vitisho bila utekelezaji jambo linalofanya watu wampuuze. Wanaona kiuhalisia hana uwezo wa kutelekeza anayosema. Japokuwa tamko hili limewafanya wengine waone kuwa amechoka, huenda akatekeleza azma yake kama waliomchukua ndugu yake hawatafanya walivyoagiza. Wapo waliosema wanampa nafasi ya mwisho, asipofanya alichoahidi, basi hawatamsikiliza tena, huku wakisema wanaungana naye kuhusu malakamiko yake.
Baadhi wamesema jambo hili halitakiwi kuchukuliwa kwa wepesi, hasa ukizingatia mtu amebeba machungu ya kumpoteza ndugu yake, anaweza kufanya lolote ikiwa kaka yake hatarudishwa, hivyo hawatakiwi kuchukulia kama mzaha tu, na wamrudishe ndugu yake, amani irejee.
Aidha, wengine wanasema huenda Polepole alishauawa kitambo hivyo hawawezi kumrudishia, sasa imebaki kuona je, Augustino atatekeleza azma yake ikiwa ndugu yake hatorudishwa? Muda unasubiriwa kuamua hatma hii.