JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
Serikali yaonya juu ya maandamno ya Desemba 9
Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, imetoa wito kwa vijana na wananchi kulinda amani na kuepuka kushiriki maandamano, ikielezwa kuwa nchi bado inakabiliwa na athari nzito za maandamano ya Oktoba 29.
Akizungumza usiku wa Novemba 28 katika burudani ya amani iliyofanyika Soko la Nyama Choma - Kumbilamoto, Vingunguti jijini Dar es Salaam, Simbachawene alisema maandamano hayo yalisababisha vifo, uharibifu wa mali za Serikali na binafsi, pamoja na kusitishwa kwa shughuli za kiuchumi katika maeneo mbalimbali.
Aidha, alionya kuhusu taarifa za mipango ya maandamano mapya Desemba 9, 2025, akisisitiza kuwa Serikali haitaruhusu hali hiyo kujirudia na kuwaomba wananchi kutochochewa kurudia makosa yaliyopita.
Maoni ya wananchi: Wengi wamepinga wito huo na kusema angekuwa kiongozi bora akengekemea kwa nguvu zote ukamataji wa watuhumiwa usiofuata sheria, utekaji pamoja na mauaji yaliyotokea wakati uchaguzi. Wameongeza kuwa maandamano yapo kwa mujibu wa Katiba, na kwamba hakuna kitakachowazuia kuandamana siku hiyo itakapofika.
Wengine wamesema hawakuchagua viongozi katika uchaguzi huu kwani uchaguzi haukufanyika, hivyo Serikali ya sasa pamoja na yeye hawatambuliki na kwamba Disemba 9 uhuru wa kweli utapatikana na viongozi wanaotokana na wananchi watapatikana, kwa sasa hawapokei maagizo kutoka kwa kiongozi yeyote toka serikalini.
Polisi Rufiji: Tumemkamata Winfrida Charles kwa kuhamasisha maandamno ya Desemba 9, hajatekwa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji limetoa ufafanuzi kuhusu Winfrida Charles, binti ambaye awali alidaiwa kutekwa na taarifa zake kusambaa mitandaoni, likisema kuwa hajatekwa bali ni mtuhumiwa wa uchochezi. Winfrida, ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na aliyefanya mahafali yake Novemba 2025, alikamatwa maeneo ya Kibiti Mjini kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa zinazodaiwa ‘kuhamasisha vurugu na maandamano ya Desemba 9’ kupitia mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa Polisi, Winfrida anaendelea kushikiliwa huku hatua za kisheria zikiendelea, na jeshi hilo likiwataka wananchi kuwa makini na taarifa wanazochapisha mtandaoni ili kuepuka kueneza taarifa zinazoweza kuleta taharuki katika jamii.
Maoni ya wananchi: Wengi wameendelea kukosoa namna Polisi wanavyokamata watuhumiwa bila kufuata utaratibu kwa kuwachukua watuhumiwa wakiwa wamevalia kiraia, bila vitambulisho wala uongozi wa sehemu husika kutokuwa na taarifa. Aidha, wananchi wanadai siku hizi Polisi wanavamia hasa nyakati za usiku wakiwa na silaha, magari binafsi na wakati mwingine yakiwa hayana vibao vya namba za usajili, na hata familia za watuhumiwa haziarifiwi hadi kudhania aliyekamatwa ametekwa. Hii hupelekea wananchi kupaza sauti kupitia mtandaoni ndio Polisi hujitokeza na kukanusha madai ya utekaji, jambo linalozidi kuwafanya wananchi waamini wanaoteka na kuua raia ni Polisi na ndio maana mambo hayabadiliki pamoja na kupaziwa sauti na kulalamikiwa.
Wengine wameonyesha kukerwa na kauli za Polisi kuita maandamano ‘vurugu’ huku wakisema kuwa kile kinachoenda kufanyika Disemba 9 ni maandamano ya amani, na kwamba kuwakamata raia kwa kuhamasisha maandamano ni uonevu na ukiukwaji wa Katiba, kwani ni haki yao.
Vyombo vya Ulinzi vyatanda mitaani, wengi wahisi ni joto la maandamano ya Disemba 9
Vyombo vya Ulinzi, vikijumuisha Polisi, Jeshi na helkopta za Jeshi vimeonekana katika maeneo mbalimbali nchini vikifanya doria bila taarifa rasmi juu ya uwepo wao ama doria inayofanyika jambo lililozua maswali mengi miongoni mwa wananchi.
Wakati hayao yanaendelea, viongozi na Polisi kutoka maeneo mbalimbali nchini wameendelea kuwashawishi na kuwasihi vijana kutoshiriki katika maandamano ya Disemba 9, wakisisitiza amani ndio kila kitu katika ustawi wa nchi yoyote.
Uhusiano wa wananchi na wasanii wa muziki nchini wazidi kudorora, matamasha na uzinduzi wa nyimbo waahirishwa
Wasanii wa muziki nchini Tanzania wameonakana kuendelea kuwa na hali mbaya kutokana na wananchi kuendelea kususia kazi zao. Wale waliokuwa na matamasha ya kufanya pamoja na kazi za kuzindua katika mwezi Novemba na Disemba wamesitisha kwa muda, uhamasishaji wa wananchi kutazama kazi zao kwenye mtandao wa YouTube nao umeshuka kwa kiwango kikubwa.
Kwa upande mwingine wananchi wanasema waliambiwa na wasanii hao kuwa ‘wanatakiwa kufanya kazi na sio kulialia kuwa maisha magumu’, wakisema kuwa sasa wameamua kufanya kazi, na hata wao wasanii wanatakiwa kufanya kazi pia; wakitaka waache kuwasumbua wananchi kusikiliza nyimbo zao au kwenda kwenye matamasha yao kwani ni kupoteza muda.
Je, huu ndio mwanzo wa anguko la muziki wa ‘Bongo Fleva’ ama pengine chimbuko la aina nyingine ya muziki na wasanii wanaokuwa upande wa jamii pale serikali inapofanya ukandamizaji kwa wananchi?