JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
Mwigulu: Rais Samia ameagiza Polisi waache kumtafuta Askofu Gwajima
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, amesema Rais Samia amelielekeza Jeshi la Polisi kusitisha kumtafuta Askofu Josephat Gwajima kama lilivyotangaza awali, ili aendelee na shughuli zake na kutoa fursa ya kujenga umoja wa kitaifa.
Waziri Mwigulu akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Magufuli - Leganga, Usa River wilayani Arumeru jijini Arusha alieleza kuwa baada ya Kanisa la Ufufuo na Uzima kupewa msamaha ni muhimu kiongozi wake naye akajitokeza hadharani kuendelea na majukumu yake kama kawaida.
Maoni ya wananchi:
Wengi wanahoji Gwajima amesamehewa kwa kosa gani? Alifanya nini mpaka wakawa wanamsaka? Kutoa ushauri kwa vyombo vya ulinzi kuongezewa mamlaka katika utendaji kazi ili waweze kufanya majukumu yao kwa uhuru kwa kutoathiriwa na mamlaka za uteuzi, ndilo lilikuwa kosa lake?
Wengine wameona hiyo kama mbinu ya kumfanya Gwajima ajitokeze hadharani ili waweze kumkamata kirahisi kwani imeonyesha wamemtafuta sana lakini juhudi zao hazikuzaa matunda. Wamemsihi Gwajima kuendelea kutoonekana ili yasije kumpata kama yale yaliyomkuta Humphrey Polepole, mpaka pale atakapojiridhisha kwa 100% kuwa ni salama kwa yeye kujitokeza.
Mwigulu: Wanaharakati wanalipwa kuchochea vurugu nchini, juzi kuna kijana amepewa Tsh. Bilioni 5
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba amedai kuwa Serikali imebaini uwepo wa wachochezi na wanaharakati wanaofadhiliwa kutoka nje ya nchi ili kuvuruga amani nchini. Ametolea mfano wa kijana mmoja ambaye hakumtaja jina, kuwa, wakati wa maandamano yaliyopita walikamata ujumbe unaoonesha kuwa alipewa takribani Tsh. Bilioni 5 ili kuchochea vurugu kwa jina la ‘Demokrasia’.
Akiwa katika ziara mkoni Arusha, Waziri Mwigulu amesema kadri vurugu zinavyoongezeka nchini ndivyo wanaharakati hao wanavyoingiza kipato zaidi, na kuwataka wananchi kukataa kushawishiwa kujihusisha na vurugu zozote zinazopangwa kufanyika nchini ili kuwanufaisha wanaharati hao.
Maoni ya wananchi:
Wengi wanaiona kauli hiyo kama propaganda ya Serikali inayolenga kupotosha na kukwepa kujibu maswali mazito kuhusu mauaji, ukatili, utekaji, rushwa, na ukosefu wa uwajibikaji. Wapo pia waliosema kama madai hayo yangekuwa ya kweli, mtuhumiwa angekamatwa na kufikishwa mahakamani pamoja na kuwasilishwa kwa ushahidi madhubuti, lakini kwakuwa ni mpango wa kukwepa uwajibikaji, wanatafuta tu chochote na kuangalia kama umma utakubali maelezo hayo au lah!
Aidha, wengine wanasema kwa cheo cha Waziri Mkuu, hakutakiwa kuja mbele ya umma na kusambaza uzushi, alitakiwa kutoka akiwa na taarifa zilizokamilika vinginevyo inakuwa umbeya na kuonyesha ni kiasi gani hatoshi kwenye nafasi hiyo.
Wengine wamefanya utani na kusema kama kuna mtu analipa Bilioni 5 ili wananchi wadai haki basi awape na wao wafanye kazi hiyo yenye manufaa kwa taifa, huku wakiiambia Serikali waache kuja kwa wananchi na ufafanuzi ambao hata mtoto mdogo anajua ni uongo, kwani kiongozi bora ni yule anayewajibika
CHADEMA: Gereza la Ukonga limezuia Viongozi wa chama kumwona Mwenyekiti Lissu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa taarifa ikilalamikia hatua ya Jeshi la Magereza kuzuia viongozi wa chama, akiwemo Katibu Mkuu, John Mnyika na Mjumbe wa Kamati Kuu Godbless Lema, kumwona Mwenyekiti wao Taifa, Tundu Lissu, katika Gereza la Ukonga. Chama kinasema zuio hilo, ambalo limeelezwa na askari kuwa ni maelekezo maalum, linakiuka haki za msingi za mahabusu kutembelewa na ndugu au viongozi wao.
CHADEMA imeitaja hatua hiyo kuwa ni unyanyasaji wa kisiasa na matumizi mabaya ya vyombo vya dola, na inataka Magereza kutoa maelezo ya zuio hilo, huku ikitoa wito kwa wadau wa ndani na nje kufuatilia hatari inayoweza kutishia demokrasia na usalama wa Lissu. Chama kimesema kitachukua hatua za kisheria, kisiasa na kidiplomasia kulinda haki za viongozi wake.
Maoni ya wananchi:
Wananchi wengi wameonyesha kukasirishwa na hatua hiyo, wakisema hili linafanywa kutokana na presha ya maandamano kuongezeka, ambapo kumruhusu Lissu kuonana na watu wengine kunaweza kuongeza hamasa kwa wananchi kudai haki na kushiriki kwenye maandamano hayo.
Aidha kuna waliohisi pengine Lissu amedhurika na hivyo wanatafuta njia ya kuficha hilo kabla ya kumtoa akiwa ametibiwa, maana ikijulikana inaweza kuongeza hasira kwa wananchi na hivyo vurugu zikaanza mapema kabla ya Disemba 9.