TANZIA Muigizaji Grace Mapunda (Tessa) amefariki dunia

TANZIA Muigizaji Grace Mapunda (Tessa) amefariki dunia

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Screenshot_2024-11-02-08-50-42-006_com.instagram.android-edit.jpg
Mwigizaji Mkongwe na Maarufu nchini Tanzania, Grace Mapunda amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.


Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Aziz Ahmed ambaye ni Muongozaji wa Tamthilia ambaye alikuwa akifanya naye kazi kwa ukaribu kwa muda mrefu.

Imeelezwa kua Grace hakuumwa muda mrefu, ila alipelekwa Hospitali juzi na usiku wa kuamkia leo Novemba 2, 2024 akapoteza uhai. Msiba upo nyumbani kwake Sinza Vatcan.

Screenshot_2024-11-02-08-51-20-610_com.instagram.android-edit.jpg

 
Sijui but apumzike kwa amani
Kwa Amani kumejaa apumzike kwa bwanaheri
Kuna kitu kimoja nataka tukumbushane binadamu wenzangu
tuishi kwa amani upendo na kumnyenyekea Mungu. Tusivimbe

Ukweli ni kwamba kadiri siku zinavyosonga ndio makaburi yetu yanakaribia
ukiona kumekucha tu ujue we are making step......towards the grave
Tafakari
 
Back
Top Bottom