Muigizaji Lulu Atimua Mbio Mahakamani | Baba Yake Ageuzwa Mlinzi

Sijaona Kesi hapo
Anakula mvua za kutosha!

Alipaswa kusema yeye alimpiga teke la kifua akaangukia kichogo na kufariki.

Mahakama ingemuachia huru kwa kuwa alipaswa kuahtakiwa kwa murder sio manslaughter.

Lulu amethibitisha kuwa ameua bila kukusudia (asingepigiwa simu na mabwana zake naye akaonyesha utata wa simu husika wakaanza purukushani na kanumba zilizosababisha akaanguka na kufa)
 

[emoji87]
 
Yaani nawashangaa sana watu wanaojizuia sijui kukwepa waandishi mahakamani wakati unajulikana.
Ukishakuwa na kesi na wewe ukiwa ni maarufu ni kwamba inakuwa inajulikana tu, mf huyu Lulu wengi wanamfahamu yeye pamoja na kesi yake
Kwa mfano mimi ikitokea nina kesi mahakamani (siombei itokee) lazima ndugu na marafiki wengi watafahamu .
Sasa kuanzia sijui kujificha sijui kukimbia waandishi siombei kuwa na kesi mahakamani lakini ikitokea hivyo sintokwepa vyombo vya habari kihivyo nikimbie nianguke niumie nipate majeraha mengine.
Nitapambana na kesi mahakamani kujinusuru na kifungo, waandishi nitawaacha wapige tu picha.
kipindi hiki cha kidigitali ni ngumu sana kuwakwepa mapaparazi.
Sio kama nawapenda hawa mapaparazi Ila inabidi Tu kuwa mpole na haya mambo ya teknologia.
Manake watu wanaweza kutumia teknologia kama za kina nasari na lema kukupiga picha hata ukiwa ndani ya mahakamani( kizimbani) bila ya wao kujulikana.
Huu ni mtazamo wangu Ila ni ukweli siku hizi kuna spy kamera zipo kama peni,miwani, vifungo inawezekana kuwa unawekwepa makamera man wa kawaida nje ya mahakamani kumbe umeshapigwa picha na video pia na spy kamera ukiwa ndani ya mahakama tena hata kizimbani unatoa ushahidi.
Nashauri tubadilike na mazingira , katika kipindi hiki cha teknologia tuwe makini sana napia tumshirikishe na Mungu
 
Hi case ya LULU nionavyo ni PARI MATERIAL na case ya OSCAR PRITORIOUS na mahakama ingetumia hukumu hiyo kama PARSUASIVE AUTHORITY wangefikia haki
exactly u make my day,Oscar alikuja kuhukumiwa kaua baada ya ripoti nyingi za kitaalamu ambazo katika kesi hii hakuna hata moja,inayoelezea kwa kina nini kilitokea pale,sijaona mwendesha mashitaka akileta mahakamani vielelezo vya kesi,kumbuka kesi ya OSCAR mfano wa ile choo ililetwa mahakamani na wataalam walichambua nini hasa kinawezekana kilitokea ile alfajiri ya tukio,profile foresinc report hamna,tabia ya Kanumba (RIP) hamna ,historia yake kama alikuwa ni mtu mwenye HAMAKI au MPOLE hamna ,hizi mahakama bado zinafanya kazi kama miaka ya 47;
 
Uzuri wa hiyo kesi ilikuwa inaonyeshwa live hivyo wafukunyungu wa mambo ya kisheria tulikuwa tunapata raahaa mustarehe kama ilivyokuwa kesi ya akina UHURU /RUTTO huko ICC. Hapa bongo hairuhusiwi kuingia na camera mahakamani na kurecord case sasa sijui hii notion ya "OPEN COURT" wasomi hawa ambao kila siku wanapishana kwenye corridors za mahakama ma masuti meusi ya kutisha hawalioni hili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…