BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
MUIMBAJI Qaswida Afrika Mashariki na Kati, Abdulhamid Fannan amealikwa kushiriki tamasha kubwa la nyimbo linalotarajia kufanyika Idd Mosi kwenye ukumbi wa Markaz uliopo Bujumbura, Burundi.
Akizungumza na mwandishi wa Habari hizi, Fannan alisema amealikwa kushiriki tamasha hilo ambalo ni la aina yake ambako amejipanga kuonesha makali yake akiwa mwakilishi pekee wa Tanzania nchini humo.
Fannan alisema amejipanga kuonesha kiwango chake cha uimbaji wa Qaswida nchini humo na kutoa wito wakazi wa nchini hiyo kujiandaa kupokea sauti nzuri ya miondoko hiyo.
Aidha Fannan alisema katika tamasha hilo ataoneshana kazi na wenzake Hassan Asadullah ‘Mugisha’ kinara wa Qaswida nchini Burundi huku wengine ni Hassan bin Hadj kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wakishirikiana na makundi mbalimbali kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki.
Fannan alitoa wito kwa mashabiki wa Qaswida nchini Burumdi kujiandaa kupokea burudani ya aina yake kutoka kwake, kwa sababu ni eneo ambalo analimudu ipasavyo.
Fannan akiwa na Crew yake amefanikiwa kuachia albamu za Dunia Mapito, Walinini mwanangu, Tazama mwema rafiki, Gubu la mawifi na Kifo chake mke wangu.