The Genius
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 822
- 2,095
Ameandika Janet Otieno muimbaji nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya:
Wapendwa wanaume,
Muda mwingine Mimi hujiuliza mnatoa wapi hizi nguvu. Kwa miezi unakaa bila hata kujinunulia mwenyewe nguo yoyote ili tu ulete chakula mezani (nyumbani). Unashinda njaa ili familia yako ipate chakula iweze kuishi. Unaamka unavaa na kuondoka nyumbani bila hata kujua unaenda wapi lakini unarudi nyumbani na pesa baada ya mihangaiko.
Iwe mchana au usiku wengi wenu mmekuwa mkiaibishwa, kudharauliwa na kunyanyaswa kwa ajili ya kuzitafutia riziki familia zenu. Baadhi yenu hamjaweza kupata kazi zenye heshima na unapopeleka "karanga" nyumbani wanakurushia usoni.
Najua mmekuwa mkijinyima ili watoto wenu wapate chakula, nguo, malazi na elimu. Mara nyingine mmetukanwa na kunyanyaswa na watu mliowazidi umri lakini mmeyachukua maumivu yote kwa ajili ya wake zenu, watoto, na wazazi wenu wanaowategemea.
Mara nyingine haijalishi kama una kazi ama lah, umepata au umekosa, unatakiwa uitunze familia. Hilo ni jukumu lako kama mwanaume.
Unalipa mahari kubwa ili umuoe mwanamke unayempenda na mara nyingine unajikuta unaitunza familia yake, kwa sababu ndugu zake ni ndugu zako pia.
Mnawezaje kufanya hayo yote ya kushangaza? Ninawaombea BWANA Mungu abariki juhudi zenu. Jasho lenu lisiwe bure. Muendelee kuishi kwenye mioyo ya mama zenu, wake zenu, watoto wenu na wote muwapendao katika Kristo.
Nawaombea Mungu aendelee kuwabariki kwa upendo wenu usio na kipimo na dhabihu mnazotoa kwa ajili ya familia zenu. Amen.!