Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
RIPOTI YA MWAKA YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KUHUSU UKAGUZI WA MASHIRIKA YA UMMA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24
Ripoti hii inaonesha ukaguzi wa mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni 2024. Inajumuisha utendaji wa kifedha na uendeshaji wa mashirika ya umma 217, kubainisha changamoto na kutoa mapendekezo ya kuimarisha utawala na uwajibikaji:
Hati za Ukaguzi Kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2024, nilikamilisha kaguzi 217 za mashirika ya umma na kutoa hati za ukaguzi. Kati ya hati 217 nilizotoa, 213 zilikuwa ni hati zinazoridhisha na nne zilikuwa ni hati zenye shaka. Asilimia ya hati zinazoridhisha imendelea kuwa asilimia 98 sawa na mwaka jana.
Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kaguzi Zilizopita na Maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Tathimini yangu ya mapendekezo ya kaguzi zilizopita na maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali inaangazia uhitaji wa kuimarisha juhudi za utekelezaji.
Kati ya mapendekezo 6,749 yaliyotolewa kwa mashirika ya umma 217 katika miaka iliyopita, 2,589 (Asilimia 38) yalitekelezwa kikamilifu, huku 2,916 (Asilimia 43) yakiwa katika hatua ya utekelezaji. Aidha, 1012 (Asilimia 15) hayakutekelezwa, na 232 (Asilimia 3) yalipitwa na wakati kwa muktadha wa mabadiliko ya matukio.
Vilevile, kati ya maagizo 209 ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali yaliyotolewa kwa mashirika ya umma 53 katika mwaka wa 2023/24, Maagizo 100 (Asilimia 48) yalitekelezwa kikamilifu, maagizo 99 (Asilimia 47) yakiwa katika hatua ya utekelezaji, na maagizo 10 (Asilimia 5) bado hayajatekelezwa.
Kuharakisha utekelezaji wa mapendekezo na maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ni muhimu katika kushughulikia changamoto zilizopo. Utendaji wa Kifedha wa Mashirika ya Umma Nilikagua utendaji wa kifedha wa mashirika ya umma 217 kwa mwaka wa fedha wa 2023/24, nikilinganisha na mwaka wa fedha uliopita 2022/23 na kubaini mashirika ya umma 12 yalipata hasara ya kifedha kwa miaka mitatu mfululizo, mashirika matano yalipata hasara kwa miaka miwili mfululizo, wakati mashirika mawili yalipata hasara kwa mwaka wa 2023/24.
Pia, nilibaini mashirika ya umma 64 yalikabiliwa na ukata, yakiwa na madeni ya muda mfupi kuliko mali za muda mfupi kwa zaidi ya mwaka mmoja. Miongoni mwao, mashirika ya umma ya biashara yalikuwa 14 , wakati mashirika ya umma yasiyo ya kibiashara yakiwa 50. Uwiano wa mashirika haya ulianzia 0.00 hadi 0.96 ikionesha upungufu wa kifedha na ukosefu wa ufanisi katika kusimamia fedha za muda mfupi.
Zaidi ya hayo, nilibaini mashirika ya umma yasiyo ya kibiashara 28 yameendelea kupata nakisi kwa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na ukusanyaji mdogo wa mapato ya vyanzo vya ndani na utegemezi mkubwa wa ruzuku ya serikali, na kuibua shaka kuhusu uendelevu wao wa kifedha.
Pia, niliabini mashirika ya umma 11 yameshindwa kuchangia asilimia 15 ya mapato ghafi kwenda serikalini kama inavyotakiwa, kwa miaka miwili mfululizo, huku shirika moja likilimbikiza michango ambayo haijalipwa kwa zaidi ya miaka minne.
Ufanisi wa Mashirika ya Umma Katika Kuimarisha Biashara Katika tathmini yangu ya ufanisi wa uendeshaji wa mashirika ya umma ya biashara na ya kimkakati, nilibaini Shirika la Reli Tanzania limeshindwa kufikia asilimia 61 ya mkakati wake wa usafirishaji wa shehena kwa wafanyabiashara wakubwa watano.
Pia Shirika la Reli Tanzania limeshindwa kutoa huduma za usafiri kwa abiria katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa asilimia 72 kutokana na upungufu wa treni za kisasa zinazoendana na huduma hiyo. Katika Kampuni ya ndege Tanzania, nilibaini tozo za ukodishaji wa ndege na akiba ya matengenezo kwa miaka sita mfululizo yenye jumla ya shilingi bilioni 369.13 ambazo hazijalipwa, na matengenezo yasiyo na tija kiasi cha shilingi bilioni 20.63 ya Ndege-5H-MWF (Q300) ambayo ilikuwa haifanyi kazi, hadi kufikia tarehe 30 Juni 2024.
Hii imesababisha kampuni ya ndege Tanzania kupata hasara kubwa ya kifedha na kupunguza utendaji wake. Hatimaye, Kampuni ya Ndege Tanzania ilipata hasara ya shilingi bilioni 91.80 na kupunguza uwezo wa utendaji.
Zaidi ya hayo, katika Kampuni ya huduma za meli Tanzania nilibaini miradi minne mikubwa, ambayo inahusisha ukarabati wa meli, ujenzi wa maeneo ya meli, na ujenzi wa gati katika Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria, ulikuwa haujaanza.Miradi hii ilikuwa na thamani ya shilingi bilioni 8.89 na dola za Marekani milioni 251.07.
Katika ukaguzi wangu nilibaini mashirika ya umma saba yalipata hasara ya shilingi milioni 966.42 itokanayo na mapato yasiyotozwa kwa kiwango sahihi. Vilevile nilibaini upotevu wa mapato ya shilingi bilioni 6.97 kutokana na hali mbaya ya barabara ya Rongai na ukiukwaji wa mkataba wa ukodishaji katika Hifadhi za Taifa Tanzania .
Sambamba na hayo, nilibaini utendaji duni wa Shirika la Madini la Taifa katika huduma ya uchimbaji, uliopelekea hasara ya mapato yaliyotarajiwa ya dola za Marekani milioni 15.52 sawa na shilingi bilioni 40.77. Kwenye ukusanyaji wa mapato nilibaini mapato yaliyokusanywa nje ya mfumo wa GePG shilingi bilioni 89.73 katika mashirika ya umma kumi (asilimia 4) kati ya mashirika ya umma 217 niliyoyapitia mwaka 2023/24. Hili ni ongezeko la shilingi bilioni 68.27 (sawa na asilimia 318) kutoka shilingi bilioni 21.46 zilizoripotiwa kwa mwaka uliopita. Pamoja na hayo nilibaini mashirika ya umma 106 yanamadai makubwa ya zaidi ya mwaka mmoja yanayofikia shilingi trilioni 3.58, yanayohusiana na huduma zilizotolewa kwa wateja.
Usimamizi wa Matumizi Katika Mashirika ya Umma Nilibaini kuwa mashirika ya umma 12 yalifanya matumizi yasiyokuwa na tija ya jumla ya shilingi bilioni 371.42, hii ni ongezeko la asilimia 413 ikilinganishwa na shilingi bilioni 72.36 katika mashirika ya umma 17 mwaka uliopita.
Vilevile, nilibaini kuwa mashirika 10 yalifanya matumizi yasiyostahili ya jumla ya shilingi bilioni 6.75, ikiwa ni ongezeko la asilimia 45 ikilinganishwa na shilingi bilioni 4.64 katika mashirika ya umma 11 mwaka uliopita.
Vilevile, ukaguzi wangu ulibaini kuwa mashirika 66 ya umma yalikuwa na madeni ya jumla ya shilingi trilioni 3.70, ambayo yalikuwa hayajalipwa kwa zaidi ya miezi 12. Usimamizi wa Bajeti Katika Mashirika ya Umma Nilibaini Serikali haikutoa shilingi bilioni 485.91 kwa mashirika ya Umma 66 kama ilivyopangwa katika mwaka wa fedha 2023/24.
Aidha, kwa kipindi cha mwaka wa 2022/23, Serikali haikutoa shilingi trilioni 1.01 kwa mashirika 50. Vilevile, nilibaini mashirika ya umma 80 hayakukusanya fedha kiasi cha shilingi trilioni 2.07 kutoka katika bajeti ya vyanzo vya ndani katika mwaka wa fedha 2023/24.
Aidha, kwa kipindi cha mwaka wa 2022/23, mashirika ya umma 66 hayakukusanya fedha kiasi cha shilingi bilioni 284.71 kutoka katika bajeti ya vyanzo vya ndani.Pia, nilibaini mashirika ya umma 12 yalitumia zaidi ya bajeti kwa kiasi cha shilingi bilioni 7.65 bila idhini ya afisa masuuli au Bodi ya Wakurugenzi,
Aidha, kwa mwaka wa fedha 2022/23, niliripoti mashirika ya umma nane kati ya mashirika 215 yalitumia zaidi ya bajeti kwa kiasi cha shilingi bilioni 21.14 bila idhini ya Afisa Masuuli au Bodi ya Wakurugenzi. Usimamizi wa Mali Katika Mashirika ya Umma Katika uhakiki wangu nilibaini mashirika 18 yanamiliki viwanja 259 vyenye thamani ya shilingi bilioni 201.67 bila ya kuwa na hati miliki.
Vilevile, mashirika ya umma 24 hayakuandaa na kutekeleza ipasavyo mipango ya matengenezo ya mali.
Aidha, nilibaini ucheleweshaji katika uhamishaji wa mali zenye thamani ya shilingi bilioni 3.59 kwenda Kampuni ya Sisalana Tanzania.
Pia, Kampuni ya Ndege Tanzania haikukabidhiwa mali zilizokuwa chini ya lililokuwa Shirika la kusimamia Mali za Shirika la Ndege la Zamani (Air Tanzania Holding Corporation).
Pia, nilibaini kuwepo kwa ucheleweshaji wa muda mrefu wa uhamishaji wa mali za Mgodi wa Tulawaka zenye thamani ya shilingi bilioni 22.42 kutoka Kampuni ya Pangea Minerals kwenda Kampuni ya STAMIGOLD, kutokana na kukosekana na hati ya kulipa kodi.
Usimamizi wa Mikataba na Ununuzi Mapitio yangu katika mashirika ya umma saba yalibaini wasambazaji na watoa huduma walichelewesha utoaji wa bidhaa na huduma zenye thamani ya shilingi bilioni 8.68 na dola za Marekani milioni 16.25 hadi kufikia siku 330.
Vilevile, nilibaini mashirika ya umma 12 yalichelewesha malipo ya madai ya wakandarasi na wazabuni wa bidhaa yenye thamani ya shilingi bilioni 54.84, Euro 194,000 na dola za Marekani milioni 354.45 kwa muda wa siku 7 hadi siku 365.Aidha, nilibaini mashirika ya umma saba yalibadili njia za ununuzi kwa mikataba yenye thamani ya shilingi bilioni 11.31. Hii inakiuka Kanuni za Ununuzi wa Umma kwa kupunguza ushindani pasipo idhini ya bodi ya zabuni.
Tathmini ya Utawala na Usimamizi na Vihatarishi Nilibaini mashirika ya umma 36 yaliendeshwa bila kuwa na Bodi ya Wakurugenzi; mashirika matatu yalikuwa na Bodi ya Wakurugenzi lakini yalikosa Mwenyekiti wa Bodi; mashirika saba yalikuwa na xi Mwenyekiti wa Bodi lakini hayakuwa na wajumbe wa Bodi
na mashirika 12 yalikosa kamati za Bodi, katiba ya Bodi, au makubaliano ya mkataba wa utendaji, vyote vinapunguza ufanisi wa utawala na kazi za uangalizi ndani ya mashirika ya umma.
Pia, nilibaini mashirika ya umma saba yalishindwa kuandaa au kuhuisha mpango mkakati na mpango wa biashara. Jumla ya mashirika ya umma 38 hayakuwa na nyenzo sahihi zilizowezesha mashirika hayo kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Aidha mashirika ya umma 30 yalikuwa na mapungufu katika utumiaji wa mifumo ya kiuendeshaji ya kielektroniki. Usimamizi wa Rasilimali Watu Nilibaini ukusanyaji hafifu wa madeni ya Mikopo kwa wafanyakazi wa mashirika ya umma shilingi bilioni 1.28.
Vilevile, hadi kufikia tarehe 30 Juni 2024, jumla ya mashirika ya umma 10 yalikuwa na deni la shilingi bilioni 12.64, ambalo kimsingi lilitokana na madai ya wafanyakazi na madai yasiyolipwa, wakati jumla ya mashirika ya umma tisa hayakuwa yamewasilisha makato ya kisheria ya wafanyakazi wake yenye jumla ya shilingi bilioni 11.89, kwa kipindi cha kuanzia siku 30 hadi siku 1095.
Aidha, ukaguzi wangu ulibaini kuwapo kwa mashirika ya umma 29 ambayo yanaendelea kutumia miongozo ya Rasilimali watu isiyoidhinishwa. Hii inajumuisha, kuwa na miongozo na sera zilizopitwa na wakati, kutokuwa na mpango bora wa kurithisha madaraka, mpango wa kubakiza watumishi, pamoja na kuwa na ikama.
Vilevile, nilibaini mashirika ya umma matano yaliajiri au kukaimisha madaraka bila idhini ya Katibu Mkuu Utumishi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Aidha nilibaini kuwapo kwa maafisa 136 waliokaimu nafasi mbalimbali kwa zaidi ya miezi sita katika mashirika ya umma 19 ambapo kipindi cha zaidi ya miezi sita kilikuwa kati ya mwezi mmoja hadi miezi 57.
Nilibaini uwepo wa wafanyakazi 31 wanaofanya kazi au walioteuliwa kukaimu nafasi mbalimbali katika mashirika ya umma sita bila kuwa na sifa zinazohitajika.
Usimamizi wa Kodi katika Mashirika ya Umma Tathmini yangu ya ufuataji wa Sheria za kodi kwenye mashirika ya umma ilibaini mashirika ya umma 17 hayakuwasilisha kodi kiasi cha shilingi bilioni 9.65 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. Hali hii inaonesha kuimarika kwa kiasi kinachowasilishwa ikilinganishwa na mwaka 2022/23 ambapo mashirika 16 hayakuwasilisha kodi za jumla ya shilingi bilioni 33.45 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Aidha, Malipo yaliyofanyika bila risiti za kielektroniki yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 2.17 (kwa mashirika tisa) mwaka 2022/23 hadi shilingi bilioni 4.14 (kwa mashirika 12) mwaka 2023/24. Utendaji wa Benki za Serikali na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nilibaini Benki ya Biashara Tanzania, Benki ya TIB Maendeleo na Benki ya Azania hazikusimamia ipasavyo mikopo iliyotolewa ya shilingi bilioni 558.53. Mikopo hiyo ilijumuisha shilingi bilioni 104.84 kutoka Benki ya Biashara Tanzania wakati shilingi bilioni 277.07 ni kutoka benki ya Azania na shilingi bilioni 176.62 ilikuwa ni ya Benki ya TIB Maendeleo.
Dhamana zilizoahidiwa za mikopo hiyo ama hazikuwa zimekatiwa bima, au zilikuwa bandia au hazikuwepo. Mapungufu katika usimamizi wa dhamana husababisha hatari ya mikopo kwa benki na wakopajiwanaweza kutorejesha mikopo hiyo.
Pia, nilibaini Benki ya Biashara Tanzania haikuweza kuendana na kiwango cha awali kilichowekwa na Benki Kuu ambapo ilikuwa na uwiano wa mtaji wa asilimia 13.41 ambao ni chini ya uwiano unaohitajika wa asilimia 14.5.
Wakati huohuo, Benki ilikuwa na akaunti za amana za makampuni ya simu yanayotoa huduma za fedha zenye jumla ya shilingi bilioni 129.18 sawa na uwiano wa asilimia 97 ya mtaji mkuu dhidi ya uwiano unaohitajika wa asilimia 50. Vilevile, uwiano wa gharama kwa mapato ulikuwa asilimia 76 dhidi ya mahitaji ya uwiano wa asilima 55.
Kutofuatiana kwa uwiano uliotajwa hapo juu kunaweza pia kuathiri ufanisi wa uendeshaji wa Benki.
Katika ukaguzi nilibaini Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta Binafsi na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma ina salio la mikopo isiyolipwa kwa muda mrefu inayofikia shilingi trilioni 3.57, ambapo shilingi trilioni 2.28 ni ya iliyokuwa PSPF zamani na inatarajiwa kulipwa na Serikali na shilingi trilioni 1.29 ni mkopo uliotolewa kwa Serikali kwa kipindi kinachotofautiana kati ya mwaka 1 hadi miaka 17. Mikopo hii isiyolipwa na Serikali imezuia uwezo wa mifuko ya pensheni kufanya uwekezaji zaidi, wakati Serikali hailipi riba ya mikopo na mifuko imesitisha kutoza riba.
Aidha, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta Binafsi ulishindwa kukusanya kodi ya pango linayofikia shilingi bilioni 19.52 kutoka kwa wapangaji wake. Kiasi hiki kingetumika kwa uwekezaji zaidi.
Pia, katika mwaka wa fedha 2023/24, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta Binafsi, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi zilishindwa xiii kukusanya michango inayodaiwa kufikia shilingi trilioni 1.18 kutoka kwa wanufaika wanaostahiki, jambo ambalo linaathiri ukwasi wa fedha, kwani linaweza kuathiri ulipaji wa madeni wakati yanapofika muda wa kulipwa.
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma ulikuwa na uwekezaji katika maeneo nane unaofikia shilingi bilioni 161.53 ambao mfuko haukupata faida yoyote. Kuwekeza kwenye miradi ambayo haizalishi faida yoyote inamaanisha kuwa hakuna thamani ya fedha katika uwekezaji huo.
Tathmini ya Sekta ya Utalii Nchini Tanzania Juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya utalii, hasa baada ya kuathiriwa sana na Uviko 19, ziko wazi na zinaonesha matokeo chanya.Hata hivyo, nilibaini masuala ambayo bado ni thabiti kwa sekta yakiwemo; ukosefu wa fedha za kutosha kwa ajili ya kutangaza utalii na kushiriki kwenye maonesho; kuenea kwa kasi kwa mimea vamizi inayotishia mifumo ya ikolojia ya hifadhi
pia, niliona usimamizi duni wa miundombinu ikiwa ni pamoja na utunzaji duni wa taka ngumu na usimamizi wa barabara. Vilevile, nilibaini kutotangazwa kwa maeneo ya urithi wa kale kama vile Engaruka na Mumba, na Mapango ya Amboni yaliyopo mkoa wa Tanga.
Pia, nilibaini usimamizi duni wa mtandao wa intaneti katika uendeshaji shughuli za kitalii ndani ya Hifadhi za Taifa. Utendaji wa Mamlaka za Maji Nilibaini ucheleweshaji wa hadi siku 622 katika kukamilisha miradi ya maji katika Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira, kutokana na changamoto za fedha na usimamizi wa mikataba, zikihusisha miradi 13 yenye thamani ya shilingi bilioni 34.27.
Pia, nilibaini uhaba mkubwa wa maji ulioathiri Mamlaka 26 kati ya 34 za Maji, na upungufu ulio kati ya 30% hadi 77% ya mahitaji, hasa kutokana na kukosekana kwa fedha na ucheleweshaji wa miradi hiyo. bilioni
Aidha, hasara ya mapato iliyotokana na upotevu wa maji ilifikia shilingi 182.21 (2022/23: shilingi bilioni 162.25), iliyosababishwa na uchakavu wa miundombinu inayosababisha uvujaji wa maji. Madeni ya Mamlaka za Maji yaliongezeka hadi shilingi bilioni 149.71, kutoka shilingi bilioni 138.64 (2022/23), kutokana na malimbikizo ya tozo za maji na usafi wa mazingira.
Tathimini ya Utendaji wa Taasisi za Mafunzo, Utafiti na Elimu ya Juu Katika uhakiki wangu nilibaini mapungufu katika usimamizi wa utafiti na ushauri, pamoja na udahili duni wa wanafunzi katika taasisi saba za elimu ya juu.
Pia, nilibaini ukosefu wa vifaa vya mafunzo, kama vile uhaba wa madarasa katika Chuo cha Usafirishaji cha Taifa, uhaba wa zana na vifaa vya mafunzo katika Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
Zaidi ya hayo, nilibaini usimamizi usiofaa wa shughuli za mafunzo, ikijumuisha kutokuzingatia uwiano wa wanafunzi na wahadhiri katika Chuo cha Usafirishaji cha Taifa, Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini na Chuo Kikuu cha Dodoma, utoaji wa programu zisizoidhinishwa, ucheleweshaji wa utekelezaji wa programu zilizoidhinishwa, na uendeshaji wa taasisi bila mitaala iliyoidhinishwa.
Aidha, nilibaini ongezeko la utegemezi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa ruzuku ya Serikali. Utegemezi huo, umekua kwa asilimia 84 ndani ya miaka mitano, kutoka shilingi bilioni 255.62 mwaka 2019/20 hadi shilingi bilioni 469.67 mwaka 2023/24. Kwa upande mwingine, marejesho ya mikopo yalipungua kwa asilimia 7, kutoka shilingi bilioni 190.72 mwaka 2019/20 hadi shilingi bilioni 176.61 mwaka 2023/24. Hali hii ilitokana na kutokuwa na mbinu za kutosheleza za kukusanya mikopo na kuwekeza fedha.
Zaidi ya hayo, nilibaini mafunzo yasiyotosheleza kwa Mtaala wa Mafunzo ya Elimu yenye Msingi wa Umahiri katika taasisi 51 na pia, taasisi 12 za ufundi zilidahili wanafunzi wapya licha ya kuzuiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
Ufanisi wa Mamlaka za Udhibiti katika Kutekeleza Majukumu Yao Katika ukaguzi wa Mamlaka za udhibiti katika kutekeleza majukumu yao, nilibaini kasoro mbalimbali kama vile udhaifu katika kusimamia hatua za kiudhibiti, Kushindwa kutumia teknolojia kikamilifu kuboresha na kuongeza ufanisi wa kutekeleza majukumu ya kiudhibiti, na kukosa ufanisi katika utoaji na usimamizi wa leseni.
Pia nilibaini mapungufu ya Bodi za Mazao katika usimamizi wa mazao ya biashara kama vile; Uwezekano wa kukwama kwa upanuzi wa maeneo mapya ya kilimo cha kahawa kutokana na vikwazo vilivyowekwa katika Mkataba wa Ulaya wa kuzuia uharibifu wa misitu, na kutotekelezwa kwa mkakati wa kuimarisha bei ya kahawa.
Vilevile, nilibaini uratibu duni kati ya bodi za mazao na halmashauri za wilaya na wadau wengine; uwezo mdogo wa uzalishaji wa mbolea nchini hali inayopelekea utegemezi mkubwa wa uagizaji wa mbolea kutoka nje ya nchi; na haja ya kutathmini upya utekelezekaji wa ununuzi wa mbolea kupitia Mfumo wa Ununuzi wa Pamoja.
Ufanisi wa Mashirika ya Umma Katika Sekta ya Afya Katika ukaguzi wangu wa utendaji wa mashirika ya umma katika sekta ya afya nilibaini gharama za matibabu ya msamaha kiasi cha shilingi bilioni 17.84 katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ambazo hazikurejeshwa kwenye hospitali hizo.
Pia, nilibaini uwepo wa dawa zilizokwisha muda wake katika Bohari Kuu ya Dawa, Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Taifa Muhimbili -Mloganzila zenye thamani ya shilingi bilioni 4.44. Kwa upande wa Bohari Kuu ya Dawa, dawa zilizokwisha muda wake zilipungua kutoka shilingi bilioni 11.74 mwaka 2020/21 hadi shilingi bilioni 4.18 mwaka 2023/24.
Aidha, nilibaini kulikuwa na dawa zilizobakiza mwezi mmoja hadi miezi sita kabla ya muda wake wa matumizi kwisha zikiwa zimehifadhiwa katika Bohari Kuu ya Dawa zenye thamani ya shilingi bilioni 4.86 ambazo aidha hazikugawiwa bure au kwa bei pungufu ili kuepuka kuharibikia bohari.Pia, nilibaini Mfuko wa Bima ya Afya ulikataa madai ya mashirika ya umma mawili yenye jumla ya shilingi bilioni 11.23 kwa mwaka 2023/24, ambapo madai ya aina hiyo yamepungua kutoka shilingi bilioni 11.83 yaliyokataliwa mwaka 2022/23 kwa mashirika manne.
Aidha Mfuko wa Bima wa Afya ulichelewa kufanyia kazi madai ya watoa huduma ya afya kiasi cha shilingi bilioni 416.08, huku baadhi ya madai yakifikia siku 122. Utendaji Katika Sekta ya Uziduaji Nilibaini ucheleweshaji wa miradi inayotekelezwa na Shirika la Maendeleo ya Taifa ikiwewo Mradi wa Engaruka Soda Ash na Ucheleweshaji wa Uanzishwaji wa Mradi wa Liganga wa Chuma na Chuma cha Pua.
Vilevile nilibaini ucheleweshaji wa Kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi wa ngozi wa megawati 30 unaotekelezwa na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania. Mradi ulikuwa ukamilike kufikia mwaka 2023 hata hivyo wakati wa ukaguzi wangu kufikia tarehe 20 Machi 2024 mradi ulikuwa umechelewa kwa miezi 27 nyuma ya muda, mradi ulikuwa hatua za awali za uchimbaji wa visima vidogo vya uchunguzi ili kuthibitisha uwepo wa rasilimali za jotoardhi.
Vilevile, katika kampuni ya STAMIGOLD nilibaini Kiwango Kikubwa cha sumu katika mabaki ya kiwanda cha uchakataji zaidi ya 50 ppm, nilibaini kuwa viwango vya cyanide vilikuwa juu kwa mwaka mzima, vikivuka mara kwa mara kikomo salama cha 50 ppm, huku kiwango cha wastani kikiwa 87.5 ppm.
Sambamba na hayo nilibaini utendaji duni wa mkandarasi wa uendeshaji wa migodi katika Kampuni (STAMIGOLD), Utendaji wa uchimbaji madini haukufikia malengo yaliyopangwa, ambapo, uzalishaji wa madini ulikuwa chini kwa asilimia 44, uhamishaji wa mabaki ya mgodi ulikuwa chini kwa asilimia 22, na jumla ya uhamishaji wa malighafi ulikuwa chini kwa asilimia 24.
Zaidi ya hayo, kuhusiana na Kampuni ya Gesi Tanzania kudumisha miundombinu ya gesi asilia, nilibaini takriban mita 80 za bomba la gesi asilia (mabomba ya Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania na SONGAS) kuwa wazi kutokana na mmomonyoko wa udongo kando ya bomba la gesi asilia.
Hii ni kinyume na Kanuni ya 58 ya Petroli (Gesi Asilia) (Shughuli za Usafirishaji na Usambazaji), ya mwaka 2018. Aidha nilibaini kasi duni na upungufu katika uwekezaji wa vituo vya kujaza Gesi asilia ya CNG.
Ukaguzi wangu ulibaini kuwa ni vituo vitatu tu vilivyofanikiwa kuanzishwa, wakati kampuni nyingine 32 zilikutana na changamoto kama vile ucheleweshaji katika kupata vibali vya kisheria kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.