Mulika: Hali ya usalama Dar es Salaam ni tete, Kova amelala fofofo

Mulika: Hali ya usalama Dar es Salaam ni tete, Kova amelala fofofo

Joined
Jul 14, 2013
Posts
16
Reaction score
13
Ndugu Wana JF

Kwanza ni declare interest..mimi ni Private Detective nina degree ya criminology kutoka chuo kimoja huko Salt Lake nchini America.....nina takribani mwaka mmoja toka nimerudi nchini sikutaka na kamwe sitaki kuomba kazi kwenye vyombo vyetu vya usalama kwani bado vinavafanya kazi in a primitive way hata i doubt kama wana value professionalism....vyombo vingi vya usalama vinafanya kazi kwa mazoea ( INTUITIVE APPEAL) badala ya kisayansi zaidi ( SCIENTIFIC APPEAL).

Kwahiyo i decided not be part of this out of touch system. Just imagine mpaka kwenye karne hii bado jeshi letu la polisi linatumia madaftari ya COUNTER BOOK kuchukua na kuhifadhi taarifa za makosa, jamani hata DESKTOP inawashinda?? hakuna efficiency hapo ni ubabishaji tu, halafu mwisho wa siku unapewa kijikaratasi cha RB ambacho inabidi ukitunze kama mboni ya jicho otherwise kikipotea inakua ni hasara kwako. Kusema kweli hali ya jeshi letu la POLISI inatia huzuni, people are too busy to discuss politics and economics but bila usalama uliotengemaa hatuwezi kufanya siasa wala kufanya shughuli za kiuchumi. TUAMKE na TUMULIKE Usalama wetu na mali zetu ulio mashakani.

Now, let me come back to my topic. Siku za karibuni kumezuka wizi wa vifaa vya magari hapa jijini hapa Dar Es Salaam. Wizi huu unahusisha vifaa vya magari kama taa za mbele na nyuma, power windows, bumper za mbele na show, radio, control box na site mirrors. Wizi huu unahusisha mtandao mkubwa unaohusisha Majambazi, Baadhi ya Polisi, Mafundi wa Magari na Wauzaji Wa Vifaa vya magari pale Karume na Gerezani. Haya ninayoandika nina ushahidi nao kwani kwa takribani miezi mitatu nimekua nikifanya private investigation kwenye maeneo ya Mburahati, Temeke, Karume na Gerezani. Na taarifa ya awali inanifanya niseme bila kuficha HALI YA USALAMA NI HATARI kwani huu mtandao ni mkubwa sana na kama juhudi hazitafanyika hakika wataitawala DAR.

KARUME PANATISHA

Upelelezi wangu ulihusisha pale KARUME ambapo ni eneo maarufu kwa uuzaji wa vifaa vya magari, nilienda pale nikakutana na wauzaji na kuwaambia ya kuwa na tafuta taa za mbele za gari yangu ya HARRIER walianimbia niwaachie order then nirude siku inayofuata, niliporudi the following day nilikuta taa ziko tayari nilipowauliza wamezitoa wapi walinijibu zimeagizwa kutoka nje, moyo wangu ulinishtuka ila kuendelea na upelelezi wangu niliwaambia wanipatie uthibitisho wa kuwa hizo taa zimeagizwa kutoka nje, nilichoambuliwa ni matusi na kuambiwa nipotee haraka iwezekanavyo kabla hawajanifanyia kitu mbaya......ni wakati sasa vyombo vya usalama kuamka na kufanya kazi kwani naamini vifaa vingi vya magari vilivyotapakaa kwenye maduka havina vithibitisho vya uhalali kwani vingi ni vya wizi.

NDUGU SULEIMA KOVA, badala ya kutumia nguvu na rasilimali nyingi kwenye maandamano ya wanafunzi, CHADEMA na WAISLAMU ni wakati sasa wa kuelekezea nguvu hizo kwa wahalifu ambao kila kukicha wanaigeuza DAR kuwa their PLAYING GROUND.

THE WAY FORWARD

1. Ndugu Suleiman Kova Ajiuzulu kwani ame prove failure katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao

2. Upekuzi yakinifu ufanyika katika maduka ya spare parts yaliyozagaa pale Karume na Gerezani kujua vifaaa wanavyouza wamevitoa wapi

3.Kwa wenye magari hakikisheni mnaweka alama ama initials kwenye vifaaa muhimu kama taa, vioo na site mirrors. Ingiwa sio suluhisho but linapunguza thamana ya vifaa hivyo kwa atakaeiba

Nakaribisha mawazo yenu kupambana na mtandao huu hatari hapa Jijini.

Nawasilisha
 
Ndugu yangu usidhani kwamba taarifa hizo za wizi hawana,Wanazo tatizo na wao wana hisa pia.

Si unajua tena mkuu kamwe hauwezi kuung'ata mkono unaokulisha?Watu Dar ndivyo wanavyoishi na hapo hauwezi ukakitenganisha Chama Tawala na mitandao hii ya kiuharifu maana CCM imetengeneza symbiotic relationships na hizi criminal syndicates.Amini nakuambia ndugu yangu maadam CCM wataendelea kuwepo madarakani basi hizi cells kamwe hazitakufa.

Siku CCM iking'oka madarakani automatically tutakuwa tumeung'oa na Mtandao wa Uhalifu.CCM ndio mzizi wa Uhalifu Nchini tushirikiane kuung'oa 2015.
 
Maelezo yako ni mazuri sana, na hakuna ubishi juu ya mambo hayo,
sasa toa mawazo yako nini kifanyike kama ulivo diclare intrest yako.
 
Mkuu mbona wizi wa vifaa vya magari upo siku nyingi!!! Me nilipigwa vifaa vyote vidogo vidogo vinavyoweza kuchomoka hadi taa ya ndani and spare tire mwaka 2009. Nilivyooenda Ununio Street (ndo hapo karibu na Karume) nikavipata freeesh, nilivinunua tena, sikutaka hata kufatilia polisi wala nini tungepotezeana muda na muda kwangu ni pesa. Kama ndo umetoka US majuzi basi karibu sana Tz.
 
BigTime

Sasa ni wakati muafaka wa sisi kushirikiana kupambana na mtando huu kwani unarusdisha nyuma harakati zetu za kujikwamua kiuchumi... just imagine kama hiyo pesa uliotumia ku purchase back your spare parts ungewekeza si leo ungekua umepiga hatua moja mbele?
 
Ndiyo hasara za kuwa na POLISI uchwara (njaa) badala ya kufanya Upelelezi na Kuwatia hatiani Wahusika. Wao wapo kwa Maslahi ya KUTUMIKA KISIASA.
 
Mkuu unapoona watu wako tayari kutoa roho za watu waendelee kuwepo madarakani unadhani ni kwa nini? CCM imetengeneza mitandao ya uhalifu mingi sana. Wanajua kuwa chama kingine kikiingia madarakani kuna uwezekano mkubwa hii mitandao itachunguzwa na watu watakamatwa na kuwekwa ndani. Ndiyo maana wanapigana kufa na kupona waendelee kuwepo madarakani wafiche mitandao yao ya uhalifu.
 
Mkuu jamaa yangu aliibiwa taa za mbele, kesho yake akaenda ilala kununua second hand alipata shock ya mwaka. Aliletewa zile zile zilizofunguliwa kwenye gari yake.(zilikuwa na alama flani hivi). Alipoenda polisi wakamwambia alete ushahidi! Ataleta ushahidi gani wakati taa zilikuja na gari? Kwani ukinunua gari taa unauziwa peke yake na risiti yake? Mi nadhani the right approach would have been kuwadai ushahidi hao wanaoziuza kwamba wathibitishe walizipata kihalali.
 
Wakikujbia kioo chako wakakuuzia tena usiseme ni chako, maana watakipiga chini kinakuwa chumvi chumvi
 
Mkuu,

Kwanza nikupongeze kwa uzi wako wenye mashiko, kwani suala la usalama ni kipaumbele cha serikali ya CCM.

Pia kuhusu mapungufu uliyo yasema hasa kwenye mazingira ya kazi kwa askari wetu ni sahihi kabisa, hii inatokana na uwepo wa vituo vingi vya polisi kwenye maeneo mbalimbali hapa Dar.

Tuje kwenye kiini cha hoja yako, huo mtandao uliosema ni kweli upo, ila ni ngumu kuweza kuwadhibiti wahalifu hao kwa kuwa parts hizo za magari mara nyingi haziwekwi eneo ambalo wanafanyia kazi hao wahalifu.

Katika kudhibiti uhalifu wa namna hii ina hitajika ushirikiano mkubwa kati ya jamii na polisi, na kwa kulifanikisha hili la ushirikiano ndio tukapata kitu kinachoitwa polisi jamii.

Mkuu, hii nchi yetu ni moja, watanzania ni wamoja, dhamira yetu ni moja ya kuhakikisha ulinzi na usalama vinalindwa. Si vyema kwa wewe kusema hautaki kuwa sehemu ya juhudi za polisi za kupambana na uhalifu, nadhani ni vyema utumie utaalamu wako huo uwe karibu na polisi ili tuweze kufikia azma yetu ya Tanzania bila uhalifu inawezekana.
 
Now, let me come back to my topic. Siku za karibuni kumezuka wizi wa vifaa vya magari hapa jijini hapa Dar Es Salaam. Wizi huu unahusisha vifaa vya magari kama taa za mbele na nyuma, power windows, bumper za mbele na show, radio, control box na site mirrors.

A minor correction: side mirrors instead of site mirrors. Kamanda, kama walivyochangia wengine, hii ni biashara ya muda mrefu Dar na siyo kwamba polisi hawawezi kuimaliza isipokuwa wana maslahi ndani yake. Mwezi uliopita niliibiwa side mirrors za gari yangu nilipoenda gerezani wakaniuliza nimeibiwa eneo gani nikawatajia, then wakapiga simu kwa mwenzao anayefanya kazi ya wizi eneo husika akasema anazo, wakaniambia bei yake ni laki mbili zote mbili nikaachana nao nikaenda duka jingine la used spare parts nikanunua kwa laki na sabini.
 
okon

Najua wahanga wa wizi vifaa vya magari ni wengi hapa mjini ila kama tuki share experience tunaweza kupata solutions kwani vyombo vyetu vya usalama viko weak sana.....intelejensia haifanyi kazi wezi wanatamba mtaani hakuna wa kuwachukulia hatua.....TUAMKE
 
nauliza hivii nani ambaye hajui police wadada na baadhi ya mapolice waume wamejicream na vipodozi vilivyo pigwa marufuku
 
A minor correction: side mirrors instead of site mirrors. Kamanda, kama walivyochangia wengine, hii ni biashara ya muda mrefu Dar na siyo kwamba polisi hawawezi kuimaliza isipokuwa wana maslahi ndani yake. Mwezi uliopita niliibiwa side mirrors za gari yangu nilipoenda gerezani wakaniuliza nimeibiwa eneo gani nikawatajia, then wakapiga simu kwa mwenzao anayefanya kazi ya wizi eneo husika akasema anazo, wakaniambia bei yake ni laki mbili zote mbili nikaachana nao nikaenda duka jingine la used spare parts nikanunua kwa laki na sabini.

Mkuu Keen, huyu private mpelelezi sijui anasema nini. Sidhani kama kuna mtu hajui kama kuna wezi wamejaa gerezani na karume, na kuna watu wanawajua kabisa wezi na matapeli wa maeneo hayo. Hapa Dar hata ukiibiwa gari ukiwaona baadhi ya watu kwa urafiki wanaweza kukwambia toa milioni gari yako unapata, na kweli unapata. Imetoka mara nyingi tu. Wezi wanajulikana, lakini unachosema hakitatokea, Kova hatajiuzulu na wizi utaendelea tu kutokea, na wezi wataendelea tu kuwepo na hawatakamatwa.

Unachoongea Mkuu private ni too naive.
 
Nimeufurahia uchambuzi wako. Imeshakua utamaduni sasa kwenda kuvinunua vifaa ulivyoibiwa gerezani. Kunamtu aliridishiwa kila kitu hadi vilivyokuwemo kwenye dash board yaani miwani funguo na documents mbalimbali...kwakua tunaendelea kununua vitu vya wizi "biashara" hii itaendelea
 
na wenye magari mnachangia wizi kwa asilimia fulani....mnanunua vitu vya wizi,leo nimeibiwa unavinunua wewe,kesho natoa oda anaibiwa mwingine na kuendelea hivyohivyo......mkiibiwa nunueni vipya kwenye duka lenye VAT tuone wakiiba watamuuzia nani.......ulaya magari yanalala barabarani si benz,si bmw na takataka zote zinalala barabarani hawaibi vitu kama taa,side mirror,power window coz hamna mtu ananunua taa za wizi,side mirror barabarani.ikivunjika unaenda dukani au junk yard zinazotambulika unatoa kwenye gari iliokuwa scrapped.....
 
Kaka, nakuunga mkono.

Na mm niweke historia yng miaka kumi iliyopita nikiwa askari polisi mwenye cheo cha constable kwa maana ya pc.

Baada ya kumaliza Advance Diploma in Marine Engineering and Technology mwaka 2009, niliamua kuachana na hiyo kazi ya upolisi kwann nilikuja kugundua kuwa huku sio sehemu inayolingana na elimu yangu na upeo wangu. Jamaa hawataki kubadilika kabisa, wamezoea kufanya kazi kwa style ya kizamani tulikuwa tunaita style ya pundugu, huyu pundugu alikuwa moja ya viongozi wa jeshi la polisi; enzi hizo polisi wanatumia uniform kaputur! Sasa ndio jamaa bado wapo kwenye mfumo huo wa utendaji wao kazi inakuwa vigumu kubadilika labda ikibadilika serikali na kuja chama kingine lkn kwa chama hiki cha CCM kamwe hakuna mabadiliko yoyote ndani ya jeshi hilo
 
Bora ume-declare interest, nimekuelewa zaidi vinginevyo.

Sasa wewe mtaalamu hutaki kufanya kazi na polisi, nani ataleta mabadiliko? Unadhani wewe ni spesho sana hufai kuwa part ya mabadiliko unataka ready made?

Majanga japo you have a point.
 
Back
Top Bottom