Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, SACP Muliro Jumanne amesema Askari wa Jeshi hilo wamemjeruhi Mtu mmoja kwa risasi katika eneo la Tanganyika Packers wakati alipokuwa eneo hilo na mwenzake wakiwapora na kuwatishia Maisha Watu waliokuwa wakipita eneo hilo kwa kutumia mapanga.