Muliro: Aprili 20 Jeshi limewakamata watuhumiwa 37 kwa Makosa ya Kimtandao, kutoa vitisho na Matusi mazito

Muliro: Aprili 20 Jeshi limewakamata watuhumiwa 37 kwa Makosa ya Kimtandao, kutoa vitisho na Matusi mazito

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, akizungumza na waandishi wa habari leo, Aprili 27, 2026, ameeleza kuwa Jeshi la Polisi liliwakamata watuhumiwa 37 katika eneo la Ubungo mnamo Aprili 20, 2026, kwa makosa mbalimbali ikiwemo Makosa ya Kimtandao kama Kutoa vitisho na Matusi mazito pamoja na Kashfa

Muliro amesema Uchunguzi wa awali umebaini kuwa baadhi ya watuhumiwa hao ni wafanyakazi wa makampuni yanayojihusisha na masuala ya mikopo ya fedha kwa njia ya mtandao. Makampuni yaliyotajwa ni:
  • Innovix Call Co. Limited
  • Otaigo Financial Services Company Limited
Miongoni mwa waliokamatwa ni mshukiwa anayefahamika kama Hashim Kassim, maarufu kama Duma. Kamanda Muliro amesisitiza kuwa jeshi hilo linaendelea na taratibu za kisheria na watuhumiwa wote 37 watafikishwa mahakamani.

 
Hizi habari wangebaki nazo hazitusadii lolote, ujinga mtupu
 
Back
Top Bottom