Pre GE2025 Muliro azungumzia kauli ya Lissu kutaka kuumizwa na wasiyojulikana kisha kumsingizia Mbowe

Pre GE2025 Muliro azungumzia kauli ya Lissu kutaka kuumizwa na wasiyojulikana kisha kumsingizia Mbowe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Ila Muliro😂😂 hapa wameshindwa tu kumuita mchochezi na mzua taharuki, si ndio haya mapuuzo yalipekea mtu akafanyiwa assassination attempt? Hii statement imenishangaza kwakweli, leo ndio anafahamu kuwa ni sehemu yao ya uhuru wa kujieleza ila wakitaka kuandamana kwa amani wabatendewa kama magaidi?!

Kuna ka kitu hapa hakajakaa sawa.



Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limejibu madai yaliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu, kuhusu kuwepo kwa watu wanaodaiwa kutaka kumuumiza kwa nia ya kumsingizia Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Lissu mbali na kuzungumzia suala hilo kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha Clouds leo Desemba 17,2024, jana kupitia ukurasa wake wa X aliliandika hilo akisema, “Enyi watu wabaya mjulikanao kama watu wasiojulikana nimezisikia njama zenu mnataka kuniumiza halafu mumsingizie mwenyekiti wetu wa chama Freeman Mbowe.”

Pia soma: Tundu Lissu: Watekaji wanataka wanimalize wamsingizie Mbowe

Akizungumza leo Jumanne, Desemba 17, 2024, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, amesema kuwa madai hayo ni sehemu ya uhuru wa kikatiba wa Lissu kutoa maoni yake.

“Mimi siwezi kupambana na hisia hizo, ila sisi tutaendelea kutekeleza jukumu letu la kikatiba kuhakikisha usalama wa watu wote pamoja na mali zao halali,” amesema Muliro.

Aidha, Kamanda huyo alibainisha kuwa kazi ya jeshi hilo ni kuchunguza na kuzuia matukio yoyote yanayohusisha uvunjifu wa sheria, lakini si kumlinda mtu mmoja pekee.
 
Back
Top Bottom