Muliro mkiendelea kushupaza shingo mjue tu hali itazidi kuwa mbaya, kwa akina Soka na Sativa mko kimya hadi leo halafu mnakuja na vitisho!

Muliro mkiendelea kushupaza shingo mjue tu hali itazidi kuwa mbaya, kwa akina Soka na Sativa mko kimya hadi leo halafu mnakuja na vitisho!

Wakuu,

Muliro umeuliza swali la rahisi tu mtu anaruhusiwa vipi kukamata mtu bila polisi? Unakimbilia kuanza kuuliza vifungu.

Kwahiyo maafisa TRA waha haki ya kuarrest mtu? Na wakimkamata wanampeleka wapi? Wana selo kwenye ofisi zao?


Wakuu naomba muongozo hapa maana sheria za TZ kizungumkuti.

Kama ofisa wa TRA anaruhusiwa kukamata mtu bila polisi, si yoyote anaweza kujifanya ofisa wa hapo akafanya mambo yao. Si ni nyinyi polisi mnasema ukija kukamatwa lazima mtu awe ana utambulisho husika?

So, mbali na polisi nani mwingine ana mamlaka ya kukukamata na anatakiwa kuwa na utambulisho gani?

Pia soma: News Alert: - Jeshi la Polisi linawashikilia watu 4 kwa tuhuma za mauji ya Mtumishi wa TRA Amani Simbayao kutoka tukio la Tegeta

Badala ya kucontrol damage unakuja kufokoea watu😂😂, etu anasema hawapigi risasi ovyo ovyo, yule mwanafunzi aliyekufa akijaribu joho risasi kichwani ilimfikiaje?

As long as hakuna majibu yuko wapi Soka, suala la Sativa linaendeleaje, waliojaribu kumteka Mkurugenzi wa Dar 24, Uchunguzi kwa Mafwele anayetumihumiwa kuhusika kwenye utekaji, wananchi wameamua kujilinda!
all criminals must be accountable against their proven crimes.

and most of them belongs to jail 🐒
 
Hakuna binadamu mwenye akili timamu akaelewa kwanini maafisa wa TRA walienda kumkamata raia saa 5 usiku bila usaidizi wa Polisi, aliua? Alikuwa na jinai gani? Gari ipo barabarani miaka zaidi 4 na analipa mpaka faini. Mbegu mlizopanda acha ziendelee kuota, malipo ni hapa hapa. [emoji1666]
TRA,UHAMIAJI,POLISI,TAKUKURU wanapenda sana vya kunyonga
Siku nyingine ntakuja na uzi wa uhamiaji
 
Nchi yetu serikali ndio sheria.... nakumbuka kuna mawaziri waliapa kabla ya kula kiapo cha ubunge, wakati tunaambiwa waziri inabidi awe mbunge!
 
Yaani hata iweje ilibidi escort ya polisi iwepo, kama utaratibu umebadilika na afisa yoyotr anaweza kukamata mtu basi kuna kazi na huu utakuwa mwanzo tu
TRA walitaka kumtoa hela tu huyo
Rushwa rushwa pesa mbele

Ova
 
Nchi yetu serikali ndio sheria.... nakumbuka kuna mawaziri waliapa kabla ya kula kiapo cha ubunge, wakati tunaambiwa waziri inabidi awe mbunge!
katiba ni kijitabu tu
nani alitoa kauli hii?😳
 
Back
Top Bottom