Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akiulizwa swali na Mwandishi wa habari kuhusu kuwepo na wimbi kubwa la askari walioshikilia silaha za moto mitaani tofauti na ilivyozoeleka, Kamanda wa Kanda ya Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema kuwa wananchi hawana hofu wanaendelea na majukumu yao kama kawaida.
Amesema kuwa Watu wema wanatamani hata askari wenye silaha wawepo hadi mafike hadi majumbani kwao huku akidai kuwa kama kuna wenye wanaoshangaa basi wana vimelea vya uharifu.
"Mtu Mwema anafurahi kuona hiyo unayoita mitutu kwa sababu haina uhusiano na yeye, wanatamani iwe mpaka milangoni, watu wema wanataka amani wantaka usalama, kwahiyo watu wanaoshangaa ni watu wenye vimelea vya kiharifu, lakini wale watu wazuri wanatamani hali hii iende kule waliko chini"
Amesisitiza kuwa doria za aina hiyo zitakuwa endelevu katika kulinda wananchi na mali zao.
Hata hivyo kuanzia September 21, 2024 imeshuhudiwa baadhi ya askari wakiwa wameshikiria silaha za moto na magari yanayodhaniwa kuwa ya 'washawasha' wakiwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Ambapo baadhi ya Watu waliosikika wakihojiwa na vyombo vya habari mbalimbali walidai kuwa na hofu wakidai kuwa haijazoeleka kushuhudia askari wengi wakiwa na silaha za moto maeneo ya mitaani ambapo shughuli za kijamii zinafanyika isipokuwa kama kuna sababu maalumu.
Pia, soma: LIVE - Yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024