Konzo Ikweta
JF-Expert Member
- Oct 3, 2013
- 735
- 1,467
Wakuu kwema? Naomba mwenye historia ya MULLAH OMARY yule mataliban alipotea mwaka 1999 mpaka leo hajulikanai alipo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimeiokota sehemu mkuu
Shukrani KiongoziMullah Muhammad Omar: Shujaa wa Taliban aliyeteketeza Vifaru vingi vya Soviet was created by Asmaa
Mkusanyaji, Mfasiri S. Hussein
. Mullah Muhammad Umar Mujahid, mara nyingi akifupishwa Mullah Omari ndiye aliyekuwa Amiri Mkuu wa Chama cha Kiislamu cha Taliban. Mullah
alikuwa kiongozi wa 11 katika mlolongo wa viongozi waliopata kuiongoza Taliban.
Alishika madaraka ya kuiongoza Afghanistan mwaka 1996 hadi mwishoni mwa mwaka 2001 pale nchi yake iliposhambuliwa bila kisa na Marekani na kulazimika kuingia vitani.
Rewards for Justice Mullah Omar.png
Taarifa zilizozagaa hivi karibuni zinadai kuwa Mullah alifariki dunia mwaka 2013. Taarifa hizo zinadai kuwa Mullah alikufa kifo cha kawaida tu baada ya jitihada za Bush za kumuwinda kwa kila aina ya silaha kushindikana. Hata hivyo, hakuna chanzo chochote kilichoweza kuthibitisha kifo cha Mullah hadi kuingia mwaka huu 2015.
Mullah alikuwa ni mmoja wa Viongozi wa Taliban waliotakiwa mno na Marekani. Wakati fulani aliyekuwa Rais wa Marekani George Bush, aliwahi kujigamba kuwa angeweza kumkamata Mullah lakini mwenyewe akajibu kuwa Ardhi ya Mwenyezi Mungu ni pana.
Kauli ya Mujahid huyu ndiyo iliyotimia ambapo hadi Bush anaondoka madarakani hakujua Mullah yuko wapi ilihali Vyombo vyote vya Kijasusi kuanzia Makachero wa Mossad, MG15, FBI, CIA walimwagwa Afghanistan kumtafuta kiongozi huyo shupavu aliyekuwa na msimamo usioyumba. Duru zote za Kijasusi zilishindwa hata kupata fununu ya wapi alipo Mullah, mshirika wa karibu wa almarhum Sheikh Usama Bin Laden.
Licha ya hadhi yake kubwa, hakuna mengi yaliyofahamika kuhusu Mullah. Habari zake zilifichikana mno. Kuna picha mbili tu ambazo pia hazijathibitika kama ni zake.
Picha inayoonekana katika makala hii ndiyo iliyotumiwa sana na Vyombo vingi vya Habari mwaka 2002 japo nayo imethibitika kuwa ni ya mtu mwingine. Picha zilizopo za Mullah zimebaki kuwa mjadala.
Hakuna kabisa picha ya Mullah, ikiaminika kuwa upigaji picha unakinzana na kanuni ya Uislamu. Yasemekana kuwa Mulla ana athari ya jicho moja, ana urefu wa Futi 6. Mullah anaelezewa kama mtu mwenye aibu-aibu sana na huwa si muongeaji sana na wageni.
Katika kipindi chake kama Amir (Rais) wa Afghanistan, Mullah Omar alitoka mara chache sana nje ya mji wa Kandahar na alikutana na wageni kwa nadra sana. Mara nyingi Waziri wake wa Mambo ya Nje, Wakil Ahmed Muttawakil ndiye aliyefanya mambo mengi ya kidiplomasia.
Iliripotiwa Julai 29, 2015 kuwa Mullah Muhammad Omari alifariki dunia. Taarifa hizo zilithibitishwa na Shirika la Ujasusi la Afghanistan na Taliban siku ya pili yake.
Maisha ya Mullah Muhammad Omari
Kwa mujibu wa vyanzo vingi, Mullah alizaliwa ama mwaka 1950 au 1962 katika Kijiji kilichopo ndani ya Jimbo la Kandahar au Jimbo la Urzgan. Baadhi ya watu wanasema kuwa Mullah alizaliwa mwaka 1950 au 1953, au alizaliwa mwishoni mwa mwaka 1966.
Mahali halisi alipozaliwa napo pia hapafahamiki kwa uhakika. Huenda alizaliwa katika kijiji kinachoitwa Nodeh, Wilaya ya Pajwai, Jimbo la Kandahar. Wengine wanasema kuwa Mullah Omar alizaliwa katika Kijiji chenye jina hilohilo katika Jimbo la Uruzgan.
Vyanzo vinasema kuwa Mullah Omari alizaliwa mwaka 1960 katika Kijiji cha Nuuri, jirani na kandahar. Kijiji hiki cha Nuuri kilichopo katika Wilaya ya Maiwand, Jimboni Kandahar ni mahali pa pili ambapo paliwekwa katika orodha ya vizuizi dhidi ya Mullah.
Kwa mujibu wa baiografia ya Mullah iliyochapishwa na Mtandao wa Taliban, Mwezi Aprili, mwaka 2015, alizaliwa mwaka 1960 katika kijiji cha Chah-i-Himmat katika Wilaya ya Khakrez, Jimbo la Kandahar.
Ukiacha mahali pa kuzaliwa, mahali alipolelewa Mullah katika kipindi cha utoto wake ni Wilaya ya Deh Rahwod, akiwa amehamia kijijini hapo na mjomba wake baada ya kifo cha babaake japo wengine wanasema kuwa hapo ndipo alipozaliwa Mullah. Mpashutum huyu alizaliwa katika familia masikini ya Afghanistan vijijini ambayo haikuwa na ardhi. Ni familia ya ukoo wa kabila la Hotak.
Kwa mujibu wa Hamid Karzai, babaake Mullah alikuwa ni kiongozi wa kidini katika eneo lake lakini familia ilikuwa masikini na haikuwa na nasaba kabisa katika miji ya Kandahar na Kabul. Walikuwa ni Waafghani wa tabaka la kati na yumkini hawakuwa watu wa jamii ya wasomi.
Babaake Mulla, mzee Mawlawi Ghulam Nabi Akhund alifariki dunia wakati Mullah akiwa bado mtoto mdogo. Kwa maneno yake mwenyewe, Mullah anasema alikuwa na umri wa miaka 3 pale babaake alipofariki dunia.
Na baadae, akalelewa na baba zake wadogo. Mmoja wa baba zake wadogo akamuoa mamaake, na familia yao ikahamia kijijini, Wilaya ya Deh Rawod ambako babaake mdogo huyo alikuwa ni mwalimu wa dini. Imeripotiwa kuwa familia ikaishi katika Kijiji cha Dehwanawark, jirani na mji wa Deh Rahwod.
Mullah Muhammad Omari alipigana vita kama askari wa Mujahidiin waliopambana na Majeshi ya Soviet akiwa chini ya kamanda Nek Muhammad. Kwa tambo lake, Mullah alikuwa ni mwembamba mrefu, lakini mwenye umbile lenye nguvu. Ndiye askari aliyeteketeza vifaru vingi vya Majeshi ya Soviet katika kipindi hicho cha Vita.
Mullah alijeruhiwa mara nne. Mullah Abdul Salam Zaif anasema kuwa yeye alikuwepo pale Mullah alipojeruhiwa jicho kwa risasi ya kufyatuliwa na mzinga yenye marisaa nyingi ndani yake katika mapigano yaliyotokea eneo la Sangsar, Wilaya ya Panjwaye muda mfupi kabla ya mapambano ya Arghandab mwaka 1987. Vyanzo vingine vinasema kuwa Mullah alijeruhiwa katika mapambano ya mwaka 1986 au 1989 mjini Jalalabad.
Tofauti na Mujahidina wengi wa Afghanistan, Mullah yeye alikuwa mjuzi na mzungumzaji wa Lugha ya Kiarabu. Alikuwa akitumia khutuba za Sheikh Abdullah Azzam na alifanya kazi ya kufundisha Madrasa mjini Quetta nchini Pakistan. Baadae Mullah alihamia Mjini Karachi ambako alikuwa Imam wa Msikiti mmoja wa huko. Huko ndiko alikokutana na Usama Bin Ladin kwa mara ya kwanza kabisa.
Kuasisiwa kwa Taliban
Baada ya majeshi ya Soviet kushindwa vita mwaka 1989 na kuanguka kwa Utawala wa Najibullah mwaka 1992, nchi ikakumbwa na hamkani huku makundi mbalimbali ya mujahidiin yakipambana kushika madaraka.
Mullah Omar akarudi zake mjini Singesar na kuanzisha madrassah. Kwa mujibu wa simulizi moja, ndoto ikamtokea Mullah akiambiwa na mwanamke wa Kiafghan: “Tunahitaji msaada wako, wewe ndio usimame kumaliza vurugumechi hii. Mwenyezi Mungu atakusaidia.”
Mullah akaanza harakatri zake akiwa na wanafunzi wake wa Madrassa (Vyuo vya Dini) Afghanistan wasiopungua 50. Wanafunzi hawa walifahamika kama Taliban.
Wale aliowafundisha walitoka katika madrassa na kambi za wakimbizi za Afghanistan katika mpaka wake na Pakistan. Hawa ndio waliopambana dhidi ya ufisadi ambao uliibuka katika kipindi cha vita vya wenyewe kwa wenyewe Afghanistan. Mullah alikubalika kwa Waafghani waliokuwa wamechoshwa na utawala wa wababe wa vita.
Nyendo hasi (bacha bazi) za wababe wa vita zilikuwa ni sababu kuu za Mullah kukusanya jeshi la wanafunzi (Taliban). Ikaripotiwa kuwa mapema mwaka 1994, Mullah aliongoza jeshi la watu 30 wakiwa na bunduki 16 aina ya rifle kuwakomboa wasichana wawili waliokuwa wametekwa na kubakwa na mbabe mmoja wa vita.
Wakamnyonga mbakaji huyo kwa mkonga wa kifaru. Tukio jingine lilitokea mwaka 1994, miezi michache kabla ya Taliban kuukamata mji wa Kandahar, askari wawili wa wababe wa vita waligombana kwa ubaradhuli wao wa kutaka kumlawiti mtoto wa kiume.
Kundi la Mullah likapambana na kumnusuru mtoto huyo. Maombi kutoka sehemu mbalimbali yakamiminika kwa Mullah kwamba aendelee na harakati hizo katika maeneo mengine ya mapambano.
Harakati zake zikapata nguvu katika kipindi cha mwaka mmoja, na kwa kipindi kifupi, akakusanya wanafunzi wengi kutoka shule za Kiislamu. Hadi kufikia mwezi Novemba, 1994, harakati za Mullah zikaweza kulikamata Jimbo zima la Kandahar, na kisha wakaikamata Herat Mwezi Septemba, 1995.
Mullah, Amiri wa Muungano wa Waafghani
Mnamo Aprili 4, 1996, Mullah alipewa na wafuasi wake madaraka ya Amir al-Mu’minin. Mnamo Mwezi Septemba 1996, mji wa Kabul nao ukaangukia mikononi mwa Mullah na wafuasi wake.
Mapambano ya wenyewe kwa wenyewe yakaendelea upande wa Kaskazini mashariki, jirani na Tajikistan. Muungano ukaundwa na kuitwa Muungano wa Kiislamu wa Waafghani na ukatambuliwa na nchi za Pakistan, Saud Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Akitajwa kama kiongozi shujaa na mchaMungu, Mullah Omari alitoka nyumbani kwake na kuonekana hadharani kwa nadra sana. Katika kipindi chote cha utawala wake, alitembelea mji wa Kabul mara mbili tu baina ya mwaka 1996 na 2001.
Mnamo mwezi Novemba, 2001, katika mahojiano yake na BBC, Mullah Omari alisema: Talaban wote wana siasa na msimamo wa kawaida. Kuna mambo mawili; ifraat (kufanya jambo kwa kupindukia kiasi) na tafriit (kufanya mambo kwa kiwango kisichotosha). Kwa maana hiyo, sisi ni wa kati na kati.
Kwa mujibu wa mwandishi mmoja wa Pakistan, Rahimullah Yusufzai, mwishoni mwa miaka ya 1990, Mullah Omari alisema, “tumemwambia Usama asitumie ardhi ya Afghanistan kufanya shughuli za kisiasa kwani zinavuruga malengo ya Taliban.”
Mnamo Mwezi Machi,2001, Masanamu ya Budha yalivunjwa kwa amri ya Mullah Omar ambaye alisema: “Masanamu yote yaliyopo Afghanistan lazima yavunjwe. Hii ni hatua iliyozusha kilio cha Kimataifa.
Katika mahojiano na BBC baada ya mashambulio ya Septemba 11, 2001, Mullah alisema, “Nyinyi (BBC) na Radio vibaraka za Amerika ndio mnaotengeneza hofu ya maisha (nchini mwetu. Sisi tunategemea nusura ya Mwenyezi Mungu. Ukweli ni kwamba inayotoweka ni Amerika. Na IshaAllah, Amerika itadondoka chini.”
Marekani yashindwa kumuona Mullah
Baada ya Vita vilivyoongozwa na Marekani nchini Afghanistan mapema Mwezi Oktoba 2001, Mullah alisadikika kuwa ndani ya Afghanistan au Pakistan. Marekani ilitoa donge nono la dola za Marekani milioni 10 kwa mtu yoyote ambaye angeweza kutoa taarifa za kusaidia kupatikana kwa Mullah.
Mwezi Novemba, 2001, Mullah aliyaamuru majeshi ya Taliban kuondoka mjini Kabul na kwenda milimani, akisema, “kupambana mijini kungeleta hasara kwa sababu ya mashambulizi ya anga ya adui.”
Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan, Wakil Ahmed Muttawakil alisema kuwa ‘eti Marekani ilieneza “propaganda” kuwa Mullah amekimbilia mafichoni. Mimi ningependekeza kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Blair na Rais Bush wa Marekani waje mahali fulani ambako Mullah pia atatokea halafu tuone ni nani atakayekimbia.” Waziri huyo alisema kuwa Mullah alibadili tu makazi yake kwa sababu za kiusalama.
Katika majuma ya mwanzo ya Mwezi Oktoba, 2001, nyumba ya Mullah Omari mjini Kandahar ilishambuliwa kwa mabomu na kuwaua mtoto wake wa miaka 10 na babaake mdogo.
Mullah aliendelea kuwa na mvuto na mafungamano na viongozi wa makundi mengine katika nchi yake ikiwa ni pamoja na Jalaluddin Haqqani. Kundi la Hasimu wake wa zamani Gulbuddin Hakmatyar nalo pia liliripotiwa kuungana na Mullah na Taliban.
Mnamo Mwezi Aprili, 2004, Mullah alifanya mahojiano kwa simu na Mwandishi Muhammad Shehzad. Katika mahojiano hayo, alisema kuwa Usama alikuwa hai na tena bukheri wa afya ambapo yeye binafsi aliwasiliana na Usama miezi kadhaa nyuma ya mahojiano hayo.
Msemaji aliyetekwa wa Taliban, Muhammad Hanif, alipata kuwaambia viongozi wa serikali kibaraka ya Afghan, Mwezi Januari, 2007 kwamba Mullah Omar alikuwa akilindwa na Shirika la Ujasusi la Pakistan (ISI) mjini Quetta, Pakistan.
Mwaka 2012, ilitolewa taarifa kuwa Mullah alimwandikia barua Rais Barack Obama mwaka 2011 akielezea shauku ya kufanya naye mazungumzo ya amani.
Kifo chake
Mnamo Julai 29, 2015, serikali ya Afghanistan ilidai kuwa Mullah alifariki dunia Mwezi Aprili, 2013. Kwa mujibu wa Shirika la Ujasusi la Afghanistan, Mullah alifariki dunia na kuzikwa sehemu fulani ya mpakani. Siku ya pili yake, Taliban ikathibitisha kifo chake na kusema kuwa naibu wake Mullah Akhtar Mansour ndiye angechukua nafasi yake. Mullah Mansour ndiye Amir wa Taliban hivi sasa.
Kumbe kumuokoa msichana asibakwe kumuokoa mtoto asilawitiwe ni ugaidi? Heil Roman C na usodomiz.Ligaidi likuu linalowakilisha ukatili wa wavaa mapedo
Lazima uwe mpinzani tu mkuu ...Naomba unielezee maana ya ugaidi mkuuLigaidi likuu linalowakilisha ukatili wa wavaa mapedo