Mulugo awataka wanafunzi kutotembelea JF

Mulugo awataka wanafunzi kutotembelea JF

Akihojiwa mapema leo na wapo FM kasema ataongoza msako wa wanafunzi wanao miliki simu nakuperezi FB na JF kwani hawaruhusiwi kutumia simu.



Yaani huyu waziri nafikiri ana funza kichwani. Sasa mwanafunzi situmie simu ili iweje? Na wale (wanafunzi) wanaokula na wabunge Dodoma watawasiliana vipi na ATM zao? Jamani wabunge watamkubalia huyu mtu kweli?
 
Yaani kama naona watanzania watakavyokwenda kuattach youtube ya Tanzania ni muunganiko wa Zanzibar kwenye ile sred aloifungua. Na atalia siku atakapokuta CV zake zipo huko watoto wanazisoma. Hivi kumbe bado hajajiudhulu tu na ameshamshtaki Sugu?
 
mi nafikiri hapo muheshimiwa mulugo, umekurupuka, usitumie ghadhabu, tumia hekima,,je unafikiri ni kazi rahisi kuwapata hao wanafunzi katika hyo mitandao...kwa hilo nasema umekurupuka,..jipange
 
amimu achapwe viboko kwa kudanganya umma.....
 
Mwacheni Mzee bhana, ndiyo uwezo wake wa kufikiria unapoishia hapo, hata watoto wake wanaona aibu sana kuwa na baba kilaza, muongo na mwizi kama huyo!
 
Amesema atampeleka mahakamani kwa yeyote yule atakaye sema yeye ameghushi vyeti.
 
Serikali imewaagiza wakuu wa shule za sekondari nchini kuchukua hatua kali dhidi ya wanafunzi watakaobainika kumiliki simu za viganjani na kuwanyang’anya na kisha kuziteketeza kwa moto au kuzitupa chooni.

Agizo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo, wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanika katika kijiji cha Totowe wilayani chunya.

Alisema sheria haiwaruhusu wala kuwapa haki wanafunzi kumiliki simu wakiwa shuleni, hivyo mwanafunzi anayekwenda na simu shuleni anakuwa amevunja sheria na taratibu za shule ambazo zinamzuia kumiliki na kutumia masomoni.

“Nawaagiza walimu kuwa ukimwona mwanafunzi ana simu na kuitumia nyakati za masomo, mnyang’anye na kuichoma moto au kuitupa chooni kwa sababu wakati mwingine simu hizo wanakuwa wamenunuliwa na wapenzi wao na hivyo kuwafanya washindwe kusoma vizuri na matokeo yake wanafeli mitihani, sisi Wizara ya Elimu hatujaruhusu na wala hatufanyi hayo mambo,” alisema Mulugo.

Alisema akitokea mzazi akalalamika au kumsumbua mwalimu kutokana na kunyan’anya mwanae simu akiwa shuleni, maofisa watendaji wa vijiji na mitaa wamchukulie hatua za kumkamata na kumpeleka Polisi ili afikishwe mahakani.

Mulugo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songwe wilayani Chunya, alisisitiza kuwa wanafunzi wakiachwa bila kudhibitiwa nidhamu zao, ndio cha kushindwa kusoma na kupata matokeo mabovu kwenye mitihani ya kitaifa na baadae kuharibikiwa kimaisha.

Alisema vijana ambao hawadhibitiwi nidhamu wawapo shuleni ndio wanaoshindwa kufanya vema masomo yao na baadaye kuwa mzigo kwa taifa kutokana na kujihusisha na mambo ya hovyo kama vile maandamano yasiyo na tija, utumiaji wa dawa za kulevya na uhalifu mwingine kwenye jamii.

Aidha, Mulugo aliwataka walimu kuanza kutembeza bakora kwa wanafunzi watukutu ili kuhakikisha nidhamu ya wanafunzi inarejea mashuleni na kuwafanya watoto warejee kwenye masomo badala ya kujihusisha na mambo ya hovyo.



CHANZO: NIPASHE

Hivi zinamtosha kweli huyu Naibu Waziri? Kifungu gani cha sheria kitatumika kumfungulia mashitaka mzazi pale atakapolalamika kuhusu simu ya mwanawe? Ninaamini kuna wazazi wanaowanunulia watoto wao simu za mkononi ili kuwezesha ama kurahisisha mawasiliano baina ya wazazi na watoto. Waziri ana upeo mdogo sana anapofikiria tu ya kuwa mwanafunzi kuwa na simu ni utovu wa nidhamu. Vituko vya huyu jamaa vitaisha lini???
 
Mulugo ana akili sawasawa?kama ameshindwa kufikiri namna ya kuboresha elimu Tanzania,aachie kiti mapema.
 
Duu, wengine wanaweza kuanzisha vibanda vya kuuza simu ni vema suala hili likawekewa utaratibu mzuri
 
Amesahau kuwa siku hizi wanafunzi wanafundishwa jinsi ya kutumia simu ikiwa ni pamoja na kutuma sms? au hiyo syllabasy ni batili?
 
Hana jipya. . . .eti atafuatilia mwenyewe suala la simu shule hadi shule!!tehtehteh!!. . . .hana jipya!!
 
mlugo kilaza tuu

Kabisa aisee....huyu jamaa hata kujibu maswali hajui...nilikuwa namsikiliza wakati ana hojiwa na redio wapo juzi daaah!!jamaa anatia aibu.Mtangazaji anamuuliza namnukuu "Unafikiri kwa nini walimu wameshindwa kufuatilia hili na kudhibiti wanafunzi kwenda na simu mashuleni?". . .Mulugo likajibu namnukuu "Sijui ila mimi nimesema nitalifuatilia". . .ZEROOO KABISA
 
Back
Top Bottom