Mulumba Ndaye: Mchezaji mpira maarufu Afrika afariki dunia

Kinyungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2008
Posts
19,484
Reaction score
38,416
_105354121_gettyimages-93758016.jpg

Mulumba Ndaye akiwa ameshika jezi ya zamani ya timu ya taifa ya Zaire pamoja na Abed Pele kushoto na Danny Jordan kulia mwaka 2010

Mchezaji Mpira wa DR Congo Mulumba Ndaye amefariki dunia huko nchini Afrika Kusini akiwa na miaka 70.Mulumba alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo yaliyosababisha atembelee "wheelchair" kwa muda mrefu.

Mchezaji huyo hadi sasa ndiye anayeshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi kwenye mchuano mmoja kwa michuano ya Mataifa ya Afrika. Alifunga magoli tisa kwenye michuano iliyofanyika nchini Misri mwaka 1974 ambako DRC au (Zaire) walichukua ubingwa wao wa kwanza Afrika ambao uliwapa pia nafasi ya kuwakilisha Afrika katika michuano ya kombe la Dunia huko Ujerumani Magharibi.

Katika michuano hiyo ya FIFA, Mulumba alikuwa Captain wa timu ya taifa ya DRC na anakumbukwa kwa kutolewa nje kwa kadi nyekundu kimakosa kwenye mechi dhidi ya Yugoslavia sababu ya refa kumfananisha na mchezaji mwenzake.

Nchini DRC Mulumba alichezea timu ya AS Vita kwa miaka 16 hadi alipokuwa na miaka 38 akiwasaidia sana kuchukua ubingwa wa Africa mwaka 1973. Wakati wa michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 1998 ilisemekana Mulumba amefariki kwenye ajali ya mgodini huko nchini Angola na kupelekea mechi ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya DRC na Burkina Faso kusimama kwa muda kwa ajili ya heshima kwake. Hata hivyo habari hiyo ilikuja kujulikana kuwa haikuwa kweli.

Mwaka 1994 katika kumbukumbu ya miaka 20 tangu aweke rekodi huko Misri shirikisho la soka Afrika, CAF lilimtunukia medali ili kuenzi mchango wake kwa soka la Afrika . Hata hivyo alivamiwa na watu waliotaka medali hiyo na pesa. Ili kuokoa uhai wake Mulumba alikimbilia nchini Afrika Kusini ambako amekuwa akiishi katika hali ya umasikini mkubwa kwenye kitongoji cha mafukara cha Khayelitsha nje kidogo ya Cape Town.

_105354113_gettyimages-542922961.jpg

Mulumba Ndaye akiwa Captain wa Zaire alitolewa nje kimakosa kwenye mechi ya kombe la dunia kati ya nchi yake na Yugoslavia huko nchini Ujerumani Magharibi mwaka 1974.

African legend Mulamba Ndaye dies in South Africa aged 70
 
maisha ya afrika ni jehanamu tosha, pesa yako ila watu wanaitaka kwa nguvu na bado wanaichukua na hakuna wa kukutetea
 
Kuishi Afrika ni changamoto sana. Ndiyo maana vijana wanaona bora wakafie bahari ya Mediterrenian kuliko kuishi Afrika
 
r.i.p lakini Kongo inawachezaji ulaya yote yaani wahamiaji,wazamiaji maana kila mweusi utaambiwa mbegu kutoka kongo
 
View attachment 1010839
Mulumba Ndaye akiwa ameshika jezi ya zamani ya timu ya taifa ya Zaire pamoja na Abed Pele kushoto na Danny Jordan kulia mwaka 2010

Mchezaji Mpira wa DR Congo Mulumba Ndaye amefariki dunia huko nchini Afrika Kusini akiwa na miaka 70.Mulumba alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo yaliyosababisha atembelee "wheelchair" kwa muda mrefu.

Mchezaji huyo hadi sasa ndiye anayeshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi kwenye mchuano mmoja kwa michuano ya Mataifa ya Afrika. Alifunga magoli tisa kwenye michuano iliyofanyika nchini Misri mwaka 1974 ambako DRC au (Zaire) walichukua ubingwa wao wa kwanza Afrika ambao uliwapa pia nafasi ya kuwakilisha Afrika katika michuano ya kombe la Dunia huko Ujerumani Magharibi.

Katika michuano hiyo ya FIFA, Mulumba alikuwa Captain wa timu ya taifa ya DRC na anakumbukwa kwa kutolewa nje kwa kadi nyekundu kimakosa kwenye mechi dhidi ya Yugoslavia sababu ya refa kumfananisha na mchezaji mwenzake.

Nchini DRC Mulumba alichezea timu ya AS Vita kwa miaka 16 hadi alipokuwa na miaka 38 akiwasaidia sana kuchukua ubingwa wa Africa mwaka 1973. Wakati wa michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 1998 ilisemekana Mulumba amefariki kwenye ajali ya mgodini huko nchini Angola na kupelekea mechi ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya DRC na Burkina Faso kusimama kwa muda kwa ajili ya heshima kwake. Hata hivyo habari hiyo ilikuja kujulikana kuwa haikuwa kweli.

Mwaka 1994 katika kumbukumbu ya miaka 20 tangu aweke rekodi huko Misri shirikisho la soka Afrika, CAF lilimtunukia medali ili kuenzi mchango wake kwa soka la Afrika . Hata hivyo alivamiwa na watu waliotaka medali hiyo na pesa. Ili kuokoa uhai wake Mulumba alikimbilia nchini Afrika Kusini ambako amekuwa akiishi katika hali ya umasikini mkubwa kwenye kitongoji cha mafukara cha Khayelitsha nje kidogo ya Cape Town.

View attachment 1010841

Mulumba Ndaye akiwa Captain wa Zaire alitolewa nje kimakosa kwenye mechi ya kombe la dunia kati ya nchi yake na Yugoslavia huko nchini Ujerumani Magharibi mwaka 1974.

African legend Mulamba Ndaye dies in South Africa aged 70
. a rfs d
 
Back
Top Bottom