Mume aliyejela amuagiza mkewe chakula chenye sumu ili afe lakini kilipimwa na mke kukutwa na hatia

Mume aliyejela amuagiza mkewe chakula chenye sumu ili afe lakini kilipimwa na mke kukutwa na hatia

FK21

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2019
Posts
8,600
Reaction score
10,760
Mshikaji mmoja yupo jela kwa kesi ya mauaji. Alimuacha mke vizuri na kila kitu sasa mke wake akawa anakitembeza sana, anachapwa sana mtaani na vijana jamaa. Stori zikampata ikamuuma sana.

Siku mke kaenda kumtembelea jamaa kamwambia mke wangu humu siwezi kutoka niletee chakula chenye sumu nife.

Mke kweli wakati uliyofuata kaleta chakula chenye sumu, kimefika tu jamaa akamuomba mkewe akionje mke kakataa ndiyo jaama kuwaambia ma askari hakiamini kikapimwe icho chakula. Kwenye kupimwa kikakutwa na sumu, sasa hapo nani mshindi?
 
Haijaondoa ukweli kuwa mkewe kagongwa na wahuni.

Halafu si ni askari wanaokwambia uonje chakula? Ilikuwa ni mara ya kwanza kupeleka chakula hakuwa akijua ataambiwa aonje?

True story yako ina utata
 
Mshikaji mmoja yupo jela kwa case ya mauaji
Alimuacha wife vizuri na kila kitu sasa wife wake akawa anakitembeza sana anachapwa sana mtaani na vijana jamaa story zikampata ikamuuma sana

Siku wife kaenda kumtembelea Jamaa kamwambia mke wangu humu siwezi kutoka niletee chakula chenye sumu nife
Wife kweli next time kaleta chakula chenye sumu kimefika tu jamaa akamuomba mkewe akionje mke kakaaa ndo jaama kuwaambia ma askari hakiamini kikapimwe icho chakula kwenye kupimwa kikakutwa na sumu sasa apo nani mshindi?
Hii sio true story mkuu hii chai tena unatak tunywe saa 1 hii na jua kali lote hili
 
Leo humu watu wanajitungia tu story.
Na mimi nashusha uzi wa kujitungia muda si mrefu. Stay tuned.
Shush kwamba una mimba yangu ya miezi nane afu nimempa tena housegirl mimba moja na nusu
 
Leo niwape story moja ya kitaa ambayo imetokea na mdau akashare. Nawe pia lete stories za Mamasta na Mamistress Hapa Dunia.

"Mjini hapa, Kaa Kimaster"

Jamaa alipata msala akawekwa ndani. Ilikuwa issue flani hivi imekaa vibaya. Lakini jamaa alijua tu angetoka kama kuna michakato flani ingefanyika.

Akamwambia "Wife tafuta wakili mzuri hii kesi nashinda maisha yanasonga mbele baada ya hapa."

My wife wake kumbe alishaingiwa tamaa.akicheck ukwasi walio nao akaona hapo ndo pa kumchinjia mumewe baharini ili damu pia iende na maji.

Akawa busy kweli hata kwenda kumwangalia mshkaji ni kwa mbinde sana. Ila akawa anakula sana maisha. Jamaa wengine wakija wanampa habari jamaa mkeo anaonekana saba viwanja na jamaa flani flani.

Jamaa akaumia sana, akija muuliza mkewe inakuwa ugomvi na mke anajibu tu ili mradi. Basi mara ya mwisho mke kuja jamaa akamuuma sikio " wife, najua kama binadamu kuna sehemu nimekukosea n.k nimewaza sana na kupata ushauri kwa baadhi ya mawakili/wanasheria. Wameniambia hii kesi SITOKI"

"Mimi nimekata tamaa ya kuishi na naona pia hii kesi kama nikisema nikomae nayo itamaliza pesa zote na mali tulizo nazo. Nimewaza nimeona ili mambo yasiharibike tukapoteza kila kitu mimi nife tu nikuache ujipange na maisha. Weekend ijayo ukija na chakula niwekee sumu nikila nife"

Mke wa mshkaji akashtuka kidogo....jamaa akamtuliza. Akamwambia

"Wala siyo big deal. Wengi tu huwa wanafanya hivyo na last week jamaa wawili wamerudisha namba kwa style hiyo kwa msaada mmoja wa mke wake mwingine wa mama yake."

Na akamwonya asithubutu kumwambia mtu yeyote ibaki kuwa siri yao tu. Ili pia kumlinda mke asije patwa na changamoto. Akamwelekeza akanunue sumu ya panya aina flani packet kadhaa achanganye kwenye pilau na siku hiyo apike la kuku. Na pia alete na juice nzuri nayo aweke hiyo kitu.

Mke akatoka akiwaza sana. Usiku akiwa home akawaza na kuwazua akatabasamu, yes. Akaona lile lilikuwa jambo la busara. Atabaki na magari, majumba na miradi mingi. Ata enjoy sana life. Then ataolewa na jamaa yake ambaye wana tokanaye kwa kuibia kwa sasa.

Kweli siku ya siku akaweka sumu kwa kufuata maelekezo akaenda navyo kumwona jamaa. Sasa ukipeleka msosi n.k gerezani inabidi uonje. Na bi dada kwa kuwa alikuwa hajawahi peleka hakujua jambo hilo. Siku zote alikuwa anaenda ki-sister du.

Basi akaambiwa aonje ile pilau na juice. My wife wa jamaa akawa anasita sita. Akasisitiziwa sana akagoma. Askari wakashtuka why agome kitu kidogo tu kama hicho akidai yeye huwa hapendi pilau. Basi onja hata juice. Hataki. Wakamweka kwanza pembeni chini ya uangalizi. Wakaita wataalamu wa mambo hayo. Kufuata utaratibu kwenda pima chakula na kinywaji...

Wakakuta vina SUMU. my wife wa jamaa akawekwa chini ya ulinzi na kufunguliwa mashtaka. Naye amepelekwa Gerezani. Tena Gereza lile lile upande tu wa wanawake.

Jamaa aliona bora basi wote wakae ndani. Kama Mbwai Mbwai tu, Ukimwaga mboga wadau wanamwaga wali halafu wanauchanganya kabisa na mchanga.

Tuendelee kupeana stories za kweli za Kitaa. 🤜🤛

"Kumbuka Mjini hapa, KAA KIMASTER"
 
Haijaondoa ukweli kuwa mkewe kagongwa na wahuni.

Halafu si ni askari wanaokwambia uonje chakula? Ilikuwa ni mara ya kwanza kupeleka chakula hakuwa akijua ataambiwa aonje?

True story yako ina utata
Aliambiwa chenye sumu na mmewe
 
Story za kukopi hazina issue. Jela chakula huonjwa na aliyeleta kwanza kabla ya kupewa mahabusu.

Story ya kukopi uongo
 
Aliambiwa chenye sumu na mmewe
Ukipeleka chakula kwa mfungwa askari wanakwambia ukionje? Ilikuaje akavuka kizuizi cha askari?
Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kupeleka chakula?
 
Wewe na Rollymsouth mmekaa pamoja na kutunga hii kitu. Maana na yeye ameipost huko Twitter.
 
Ukipeleka chakula kwa mfungwa askari wanakwambia ukionje? Ilikuaje akavuka kizuizi cha askari?
Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kupeleka chakula?
Alipoambiwa kukuionja akagoma mmewe kuulizwa mbona hataki kuonja uyu akasema basi kipimwe ndo ikabainika
 
Imetokea magomeni mikumi
 
Alipoambiwa kukuionja akagoma mmewe kuulizwa mbona hataki kuonja uyu akasema basi kipimwe ndo ikabainika
Basi huyo maza ni chizi. Iweje asijue ataambiwa aonje?
 
Back
Top Bottom