Hao mashosti waliokuwa wamekaa bar wakinywa na kula mdudu bila waume zao hapo tayari kwa mtazamo wangu sio sahihi. Unategemea nini hapo kama watapata ofa ya wanaume wengine hapo na kinywaji sio chai au supu kikishaingia kichwani vizuri na kushuka sehemu zote za mwili, kama wanalipa jamaa wanawachukua kwenda kufanya ngono kirahisi kabisa. Pombe ikishaingia kichwani changanya na uchungu wa magomvi ya nyumbani ni rahisi sana kujikuta mtu anafanya dhambi haswa ya uasherati sawa na mtu aliye na pepo mchafu. Ndoa zote inabidi ziwekwe mikononi mwa Mungu bila hivyo hakuna ndoa itakayosimama hata kama wanandoa wawe matajiri, wasomi, masikini au watu wa kawaida, waendakanisani sana, watoa sadaka sana au waimbakwaya sana.