Caroline Danzi
JF-Expert Member
- Dec 19, 2008
- 3,713
- 1,265
Kuna mke wa jamaangu mmoja ambaye aliamwambia mumewe baada ya kutoelewana ndani..."Nimechoka, naenda kwa Mamaangu!"
Familia hiyo ilikuwa na Watoto 7.
Basi mumewe akamjibu..."Ni sawa tu, nenda kwa mama yako, Ila sasa hivi na mimi nimeamua kurudi kwa Mama yangu mzazi, lakini ili mambo yaende sawasawa, na hawa watoto wetu saba wote waende kwa mama yao!
Mke yule kusikia hivyo akamwambia mumewe ..."Yaani Una maana watoto waje kwangu sio!"...Basi nimebadilisha mawazo siendi popote!
Familia zetu hizi ziko flagile sana, hakuna upendo.
hilo unalosema kweli lipo lakini kuna wengine tumekaa nao miaka kumi then ndio tukafunga ndoa lakini bado mbeleni mnabadilika sana na hivi sheria ni pasu kwa pasu ndio maana mnaringa siku ikitokea tumetengana sioi tena nageuka snake tu.......Tatizo ni kuwa watu huharakisha sana suala la ndoa......unakutana na mtu hata hujamjua vizuri unatatfuta wazazi wake uoe......unapokuja kumjua vizuri too late......ndio haya ya kuombeana vifo
Kwa maelezo ya huyu shostito ni kwamba yeye ndiye anatunza familia, nadhani wana mtoto/watoto, anayo kazi nzuri inayomuingizia kipato cha kutosha(ofcourse alitaja mahali anapofanya kazi, ni kampuni kubwa hapa nchini).
Kinachomtatiza ni kwamba mume haonekani kumjali kabisa, haonyeshi mapenzi yoyote kwake, anahisi kama ana mwanamke mwingine.
Mkuu huyu mwanamke alikuwa hazungumzii kurithiwa, alikuwa anamaanisha kwamba ataolewa na mwanaume mwingine anayempenda.
Utakumbuka alikuwa anamwambia mwenzake kwamba, tafadhali msije kuniuliza huyu mchumba nilimpata lini na wapi!!
Kwahiyo tayari mume mpya keshapatikana, kinachosubiriwa ni kifo cha mume wa sasa.