Mume amkata masikio yote mawili Mke wake kwa madai ya kupoteza simu yake

pantheraleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
693
Reaction score
889
Mkazi wa Kijiji cha Mesaga Wilayani Serengeti Mara, aitwaye Magori anadaiwa kumkata masikio yote mawili Mke wake Mkami Mwitonyi mwenye umri wa miaka 22 kwa madai ya kupoteza simu yake.

Imeripotiwa kuwa, mwanamke huyo amelazwa katika Hospitali ya DDH wodi ya Wanawake tangu juzi Jumatano, Oktoba 23, 2019 kwa matibabu zaidi.

Akisimulia tukio hilo Kaka wa Mwanamke huyo Muhoni Mbusi amedai ulitokea ugomvi kati ya wanandoa hao kisha Magori akachukua kamba na kumning’iniza Mkewe juu ya dari na kumkata sikio la kwanza na la pili huku akimwambia sali sala yako ya mwisho nakuchinja.

Inadaiwa kuwa wakati anajiandaa kumchinja mwanamke huyo alipiga kelele kwa nguvu majirani wakawahi kutoa msaada.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Juma Ndaki amethibitisha na kusema kuwa wanaendelea kumtafuta Mtuhumiwa ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
 
Hivi wakurya mna nini nyie watu!?..ubabe sio uanaume ni upumbavu na ujinga wa kimaskini tu..kama mnajazana ujinga na dunia hii kuendeleza ubabe inatakiwa mchunguzwe vichwa vyenu..
 
Kanda ya ziwa mweeeeeh[emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
 
duu jamani mimi naogopa watu wa mara....

Hao hua wanajimwambafai kwa wanawake tu.

Kuna jamaa anaitwa Zakaria alikua ana ma-bus huko Tarime, siku akiamua tu anakatisha route na wanaume wa tarime wanashushwa wote kwny bus huku jamaa akiwasubiri pale mlangoni na kiboko kila anayepita ni fimbo tu hakuna wa kumfanya kitu.
 
Kumbuka kule kuna mashamba ya bangi na gongo hakuna haja ya kuwapima akili.
Nilivutiwaga na mambo haya nikaomba kiwanja kule watani zangu hawa wakaona nitafaidi wakaninyima
Hivi wakurya mna nini nyie watu!?..ubabe sio uanaume ni upumbavu na ujinga wa kimaskini tu..kama mnajazana ujinga na dunia hii kuendeleza ubabe inatakiwa mchunguzwe vichwa vyenu..
 
Inasikitisha sana kumfanyia kitendo cha unyama na kovu lisilo futika maishani mtoto wa mwanaume mwenzangu
 
Lakini cha ajabu zaidi, huyo mwanamke akipona sinto shangaa akija kuiambia mahakama kwamba imuachilie mume wake, kwasababu yeye bado anampenda sana na watoto bado wanamuhitaji baba yao.
Huo mkoa wa Mara ni shida sana
 
Mkazi wa Kijiji cha Mesaga Wilayani Serengeti Mara, aitwaye Magori anadaiwa kumkata masikio yote mawili Mke wake Mkami Mwitonyi mwenye umri wa miaka 22 kwa madai ya kupoteza simu yake.

Imeripotiwa kuwa, mwanamke huyo amelazwa katika Hospitali ya DDH wodi ya Wanawake tangu juzi Jumatano, Oktoba 23, 2019 kwa matibabu zaidi.

Akisimulia tukio hilo Kaka wa Mwanamke huyo Muhoni Mbusi amedai ulitokea ugomvi kati ya wanandoa hao kisha Magori akachukua kamba na kumning’iniza Mkewe juu ya dari na kumkata sikio la kwanza na la pili huku akimwambia sali sala yako ya mwisho nakuchinja.

Inadaiwa kuwa wakati anajiandaa kumchinja mwanamke huyo alipiga kelele kwa nguvu majirani wakawahi kutoa msaada.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Juma Ndaki amethibitisha na kusema kuwa wanaendelea kumtafuta Mtuhumiwa ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Wana Mara mnatia fora kwa ukatili dhidi ya akina mama.
 
Mikurya ni mipumabvu sana.

Njoo huku ukonga uone inavyoishi kama iko kijijini, yani mijitu ipo mjini lkn ina lala na ng'ombe
 
Ukatili gani huu,Mara wa Mara wajiangalie sana,simu tu ndio uue mke wako?
 
Back
Top Bottom