Dena Amsi
R I P
- Aug 17, 2010
- 13,080
- 4,273
Kuna dada tunafanya nae kazi huku nje ya Tanzania, kaolewa mumewe yupo Dar ndoa yako ina miaka mitano, toka tumekuja huku jamaa anagombana na mkewe kila kukicha tangu mwezi wa 5 tuko huku huyu dada hana raha kabisa mumewe kila akipiga simu akisikia tu sauti hata ya gari ataanza kuuliza hapo uko wapi hujafika nyumbani na amesahau kuwa huku tunatumia usafiri wa public.
Mbaya zaidi amemkasirikia toka ijumaa hajaongea na yeye huyu dada hata kazi inamshinda analia tu kila mara. Amefikia kusema kuwa anataka kurudi maana hali imefika pabaya. Na mkataba tulipewa three years? Je? Aache kazi arudi Dar ama afanyeje mie nimeshindwa kumshauri maana ukiongea nae tu analia nikaona niilete hapa tumshauri. Tafadhali nisaidieni najua humu nitapata jibu