USINISHAWISHI niamini kwamba bado humu ndani watu hatufahamu ni hasa maana ya mambo ya ndoa!!!!! Ina maana kibao chenye maandishi ni masuala ya ndoa Freema?! gimme a break lady! Sikuuliza kwanini hawapati mtoto! Sikuuliza kwanini mke wake amekonda au amenenepa! Sikuuliza kwanini kaoa mwanamke kama yule!! Sikuuliza wanatarajia kupata watoto wangapi! Sikuuliza kwanini kila siku wanakula maharage au nyama! Sikuuliza kwanini kaoa mke mrefu/mfupi! Sikuuliza..........!!!! Mlolongo ni mrefu, hivyo sikutarajia kama mtu anaweza kushindwa kutofautisha kati ya maisha ya ndoa/family/personal na issues ambazo ni za kijamii zaidi!!! Sio siri, baada ya kuona umeibuka na jazba, nikalazimika kurudia kuisoma post yangu tena na tena!!! Ajabu ni kwamba, sikuona sehemu yoyote niliyoandika kwamba mshikaji wangu sio mstaarabu!!! wewe hiyo umeitoa wapi?! naona ulichofanya wewe sio kutaka kuichangia post yangu, bali kuendeleza malumbano aliyoyaacha mtu anayejiita Gaijin ambae nilimwambia sitaki malumbano! Hayo ya kwamba nikatafute rafiki mwingine mstaarabu umeyatoa wapi bibie?! Hivi unaweza kunijuza chanzo cha jazba hiyo wakati niliyekuwa nimemshauri tulikuwa tunaongea kirafiki na wala hakukereka!!! Sasa mwenzangu wewe kinachokufanya ufure kiasi hicho nini?! By the way, niliuliza kama ni busara kuwa na maandiko kama hayo majumbani kwetu; mwenzagu badala ya kujibu hoja unakuja na jazba na kunitaka "nitafute" rafiki mwingine mstaarabu!!!!!!! hivi mwenzangu wewe huwa hutoi ushauri kwa rafiki yako?! Usisema huingilii personal issues kv ile sio personal issue na wala sio suala la kindoa!