Mume kafanyiwa ndivyo sivyo!!!

menny terry

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
509
Reaction score
670
jamani okoeni hii ndoa wanajamvini...Huyu dada kaolewa miaka 6 iliyopita lakini wakati anaolewa alimkuta mumewe kashajijenga kwa mali nyingi ijapokuwa sio saana! Mumewe kiufupi kwenye 6*6 anajiweza.Tatizo ni huyu bwana huko nyuma alikuwa anafanya kazi ya ubaharia ambayo ndo imempa hizo mali lakini kumbe moyoni ametunza siri yake na ameona amwambie mkewe kuwa aliwahi kufanyiwa usodoma na ma capten wa meli sasa dada kachanganyikiwa wakiwa faragha hana hamu kabisa na mumewe.Ushauri tafadhali.
 
Dah! Pole kwa kaka, ila huyo dada apunguze jazba, mumewe kamwamini ndo maana kamweleza siri ambayo hajawahi kuitoa maisha yake kwa mwingine. Pili, wakati wanaoana alikiri kumvumilia kwenye shida na raha na kwamba matatizo yao ya ndani yanakuwa siri yao, sasa anavopaniki hivo haoni kama anavunja maagano? Plz plz plz, dada awe mvumilivu, hiyo ni changamoto ya maisha yao na kwamba akumbuke pia kuwa hayo yalitokea wakati wao hawajaoana hivyo haina maana sana kuyatilia maanani kama mumeo anamridhisha kwenye godoro.
Afanye na kuyachukulia taarifa ya mumewe kuwa ni kama utani, atasahau tu na kurudia ktk hali yake ya kawaida.
 
si anafaidi hizo mali na aliapa kwenye shida na raha ss ndo avumilieee weeeeeee mpaka mwisho wa safari
 
Mke ana haki ya kumtosa jamaa kwa sababu kama jamaa angekuwa wazi kabla ya ndoa kusema kuwa alisha chokonolewa huko nyuma basi mke angefanya right decision before marriage.
Sioni mantiki ya jamaa kusema siri hiyo sasa,anataka utajiri zaidi au?
 
Ndo maana hua nasisitiza watu wawe wakweli kuhusu mambo yanayoweza kuinfluence maamuzi ya wenza wao au yanayoweza kuwaumiza!!Sijui hata nishauri nibu maana sijui ingekua mimi ingekuaje!!Pole yao..,,,
 
Aah!Mimi naona aibu sana mambo haya,mpaka nasikia usingizi!
 
Ndo maana hua nasisitiza watu wawe wakweli kuhusu mambo yanayoweza kuinfluence maamuzi ya wenza wao au yanayoweza kuwaumiza!!Sijui hata nishauri nibu maana sijui ingekua mimi ingekuaje!!Pole yao..,,,

Kweli Lizzy ukweli tu ndo dawa,huyu jamaa angesema ukweli b4 dada wa watu angeamua mbivu au mbichi....:sleepy:
 
Jamani, kwenye ndoa kila mtu ana siri ya moyoni mwake. Sio kila kitu huw akinawekwa wazi (ingawa nakubaliana na Lizy kwamba ni vema kusema ya moyoni mwako mapema). Sasa jamaa hakusema muda wote, kaona nafsi inamsuta kamwaga radhi! Dada msamehe mumeo. Kwani na yeye akigundua/au ukimweleza kuwa zamani ulikuwa msagaji itakuwaje?

Mshauri huyo dada, to Get it out of her mind and move on! Maisha ya ndoa magumu, mbona mengi hujayaona! Unachoka asubuhi na mapema? Ndio shida na raha hizo!!!
 
Japo sijaona uhusiano wa mali za jamaa na tatizo walilonalo, kudumu kwa ndoa hii kunategemea sana busara na ustahimilivu wa huyo dada. Ni kweli ni kitendo cha aibu kwa mtu mwenye maadili mwanaume kuendewa kinyume na maumbile na mwanaume mwenzie hata kwa kupewa nini lakini huyo dada akumbuke ahadi yake.
Nina hakika kabla jamaa atakuwa alisema 'mke wangu nina siri nzito naomba univumilie na unisamehe kwa nitakayokuambia' na huyo dada kasema 'usihofu mume wangu, lolote utalosema sitaacha kukupenda', vinginevyo jamaa asingetoa aibu iliyomtesa maishani mwake. Avumulie ndo chungu za tamu anayokula.
 


Kwa mwanamke ku admit alifanya usodoma ni rahisi kuliko mwanamme...
kuna sababau kaamua kumwambia hivyo mke wake - labda anataka wife
anondoke but sijaona sababu ya msingi ya yeye kumwambia the wife kama
yalitokea huko nyuma na hafanyi tena... itakua anaji emasculate... na NO
man anataka kufanya hivyo in front of his woman...

Kwanza nashangaa hata huyo dada kukusimulia.. hio ni issue nzito saana
ambayo maamuzi yoyote yatayochukuliwa ilitakiwa iwe kati yao wawili
kutangaza mumeo kisha wahi fanya hivyo.. unaongozana nae vipi njiani??
 

kwa kweli Asha D im in love with you,una mabusara sana,
mim pia nilijiuliza why on earth amueleze mkewe hayo mambo yaliyopita,mim nina hofu kuwa huyu mume bado ana huu mchezo,anataka hata mkewe akiyasikia aseme hayo ni yale mambo ya zaman.Au kama ulivyosema anataka mkewe ajue,au kwa vile wanaume wenye tabia hizo ni wagonjwa wa akili usikute anajaribu kutaka kumshirikisha mkewe ktk huo mchezo,maana kuna mtu nasikia ndo michezo yake lkn ameoa hivyo wana bwana mmoja wanafanya nae threesome.
 

Siyo lazima iwe hivyo. Huenda jamaa anafeel guilty sana na anataka peace of mind. The only way ya kuwa na peace of mind ni kueleza tatizo linalokusumbua na jamii ikupe moyo na ushauri. Labda kama jamaa anaendelea ni kesi nyingine.
 


Cheusi Mangala it is an honor wewe kusema hayo maneno kwenye RED... THANK YOU... I want you to know kua umenigusa saana na nimefurahi... (na hapa naona wanaume woote wanaotolea macho Avatar yako wanatamani wawe mimi right now...lol)

On a serious not hio statement kwenye blue is the most logical explanation.. sikufikiria kabisa katika angle hio (which gives me the right ya kukwambia una busara pia) BUT hivi umesema naona ndo the most logical explanation.. kamuanzia mbali ili waanze huo mchezo mchafu. Ndo tatizo la wanaume siku hizi huko vijiweni, ndo story wanazo piga na jinsi gani ya kushawishi wenza wao... Disgusting!!
 
Siyo lazima iwe hivyo. Huenda jamaa anafeel guilty sana na anataka peace of mind. The only way ya kuwa na peace of mind ni kueleza tatizo linalokusumbua na jamii ikupe moyo na ushauri. Labda kama jamaa anaendelea ni kesi nyingine.

ni kweli sio lazima iwe kama nilivyosema ndo mana nikasema nahisi,inawezekana pia ikawa kama unavyohisi wewe,sisi wote tunajaribu kuona ni kwa nin amweleze mkewe,ukweli anao yeye na mungu.
 
I think ni kwa sababu huwa ham ya kudo ni ndogo thats why wife wake akahitaji maelezo why yuko hivyo,othewise hakuhitaji kusema yaliyopita!
 
Nadhani ni tatizo la kisaikolojia zaidi,japo alichelewa kumwambia kabla hawajaoana.Wawaone wataalam wa saikolojia na madaktari.
 
Kama kuna kitu kimefichika hapa,kwa nini asimueleze wakiwa wachumba? Kama aliona bora ibaki kuwa siri kwa nini aitoe sasa? Kuna sababu,na ni huyo baba pekee anayeijua. Pole sana kwa huyo dada ila amuombe sana Mungu ampe busara ili atoe maamuzi sahihi.
 
Hapo jamaa anataka kumtosa huyo mama, nadhani jamaa hakuwahi kufanyiwa mambo ya kisodoma ila kamwambia hivyo ili achukie na aondoke. Akili kumkichwa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…