Mume: Kajala nitoe jela

Mume: Kajala nitoe jela

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Siku chache baada ya gazeti pacha la hili , Ijumaa Wikienda, toleo la Jumatatu iliyopita kuripoti juu ya utajiri mkubwa wa staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘ K’ , mumewe Faraji Agustino amempigia saluti na kumuomba amtoe gerezani. Kajala na mumewe wakiwa mahakamani .

KWANI ILIKUWAJE? Machi mwaka jana, Faraji alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela au faini ya zaidi ya Sh . milioni 200 baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC , Tawi la Dar ambapo jamaa huyo alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘ akiozea’ Segerea au Segedansi kama wanavyoita mastaa wa Kibongo.

UTAJIRI WA GHAFLA Katika msala huo, Kajala alihukumiwa miaka mitano jela au faini ya Sh . milioni 13 kwa kukutwa na hatia ya kuuza nyumba yao iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru ) ambapo alilipiwa shilingi Milioni 13 na Wema Isaac Sepetu na sasa anapeta mtaani na utajiri wa ghafla .

HOJA YA MSINGI

Baada ya kuokolewa jela na Wema , Kajala ametembelewa na utajiri ambapo amekuwa akitanua mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar , akisukuma magari ya kifahari , kupanga ghorofa maeneo ya Sinza - Madukani anayolipia Sh . milioni 3.2 kwa mwezi , akimiliki kampuni ya kuzalisha sinema ya Kay Entertainment huku akaunti yake ikiwa imenona kwa mamilioni kadhaa .

GEREZANI SEGEREA

Hivi karibuni , ‘ mtu wetu ’ alikwenda kumtembelea Faraji kwenye Gereza la Segerea , Dar ambapo alipata nafasi ya kutoa la moyoni juu ya mkewe Kajala ambaye alifunga naye ndoa kanisani miezi michache kabla ya kukutwa na msala huo .

Akizungumza kwa huruma , Faraji alisema habari za Kajala kuwa na utajiri wa kutupwa alianza kuzisikia kwa ndugu zake hivyo kumuomba staa huyo kumkumbuka kwenye ufalme wake.

Kajala na mumewe siku ya ndoa . Jamaa huyo alisema kila akikaa huwa anakumbuka good time ( kipindi cha matanuzi) yao ambapo ilikuwa ni bata mwanzo mwisho hasa nyakati za wikiendi. Kwa mujibu wa mtu wetu huyo , Faraji alimwambia: “Mwambieni K akumbuke yeye ni mke wangu.

Nimemsaidia kwa mengi , asiniache nateseka huku yeye anachezea pesa ambazo anaweza kunilipia na nikatoka kifungoni. Pia akumbuke ahadi yetu ya ndoa kanisani na jinsi tulivyoishi kwa upendo . “Bado ni mke wangu, bado nampenda sana.

Nilisikia alishavua pete ya ndoa lakini ukweli ni kwamba bado mapenzi yetu yapo palepale . Kama kweli Kajala amepata utajiri naomba anitoe gerezani, sitamsahau maisha yangu yote. Kama nilivyoahidi kanisani , nitampenda na kumtunza hadi kifo kitutenganishe . ”

Chanzo hicho kilidai kwamba Faraji alisema Kajala amuonee huruma , azungumze na wadau wake wote wamtoe gerezani halafu atajua jinsi ya kurejesha fedha hizo .

Habari nyingine kuhusu suala hilo ilisemekana kwamba jamaa huyo ametengeneza netiweki akiwa gerezani kupitia kwa watu wake wanaomtembelea ambao wapo tayari kuungana na staa huyo ili kufanikisha jambo hilo. Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K ’.

INAWEZEKANA?

Akizungumza na gazeti hili , mmoja wa wanasheria wenye uzoefu na kesi za mastaa aliyeomba hifadhi ya jina alisema kwamba jambo hilo linawezekana endapo mteja ( mume wa Kajala ) ataomba kesi yake ifanyiwe ‘ reference ’ ( mapitio ) . “Unajua haya ni mambo ya kisheria , kwa mtu wa kawaida anaweza asiyaelewe kirahisi lakini uwezekano upo bila hata kukata rufaa.“Faraji alihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ( Dar ) .

Kitakachofanyika ni kwamba kama akitaka kesi yake itafanyiwa reference kwenye mahakama ya juu. “Baada ya hapo Faraji au wakili wake anaweza kuomba kulipa faini badala ya kifungo kwa sababu hukumu ilisema kifungo cha miaka saba au faini ya hiyo shilingi milioni 200 .

“Kama kweli Kajala ana hiyo fedha si mbaya akafanya hizo process ( taratibu ) , akamtoa mumewe,” alisema ‘ loya ’ huyo.

KAJALA ANASEMAJE?

Baada ya kujazwa data hizo , Jumatano iliyopita Ijumaa lilimtafuta Kajala ambaye simu yake haikuwa hewani kila ilipopigwa na hata alipofuatwa nyumbani kwake hakuwepo lakini kwenye makabrasha kulikuwa na maelezo yake juu ya mumewe alipohojiwa siku kadhaa zilizopita.

Kwa mujibu wa Kajala , Faraja bado ni mumewe na huwa anakwenda gerezani kumuona kila wikiendi na anatamani awe huru ili waendelee na maisha kwani hawakuwa wamefaidi penzi lao, hata mtoto walikuwa hawajapata.

MARAFIKI WANASEMAJE ?

Marafiki wa wanandoa hao waliozungumza na Ijumaa walisema kwamba kama kweli Kajala ana nia hiyo , basi afanye hiv yo kwani itakuwa thawabu kubwa kwake kama alivyofanyiwa na Wema aliyemnusuru kifungo cha miaka mitano jela.

Chanzo: GPL
 
Hivi hua wanatoa hizo milion 200 kabisa kabisa au??? Kajala fanya mambo ila akikukimbiaa msoto utaupataa
 
mmmh milion 200 parefuu. halafu hivi utajir wa masupa staa wetu ni kumiliki magari tu?
 
Hata kama ana utajiri hana hiyo pesa ya kuweza kumtoa.
 
Kama alikuwa anakula bata mwanzo mwisho na pesa haramu, sasa ni zamu yake kuliwa na bata mwanzo mwisho.....
 
Hizo 200m kma za Zimbabwe sawa ataweza kulipa ila kma z bongo ni shida.yeye kajala huo uwezo hana maisha yake ni maigizo tu yani fekeroo

hili neno
by the way hakuna ndoa hapo kuna makaratasi ya sign tu
kiapo chetu kinasema naahidi ntakua muaminifu
 
Ml 200... ni pesa ndefu, but hakuna kinachoshindikana hope K anajipanga mambo yakiwa fresh atamtoa gerezani mumewe
 
Ndoa haikuanzishwa na wanadamu.....ni mpango wa Mungu....hivyo unapotaka kuingia kwenye mpango huo ulioanzishwa na Mungu mwenyewe........lazima ujue sifa za Mume/Mke kwa mujibu wa Mungu mwenyewe.........otherwise tutaendelea kumpa sifa shetani kwa kejeli maarufu za "siku hizi hakuna ndoa".......:cool2:
 
Ml 200... ni pesa ndefu, but hakuna kinachoshindikana hope K anajipanga mambo yakiwa fresh atamtoa gerezani mumewe

Hawezi kumtoa ata kwa dawa kwa hiyo pesa, we mtu toka k atoke jela hata ku post picha au kuonyesha kumkumbuka mume wake, yeye kutwa picha za mwanae na marafiki zake, mara kapanda ndege business class, mara kapiga picha yupo china, yan mpaka mda mwingine nasahau kama aliolewa,yani hii mijanamke ya bongo movie malaya kabisa mbwa hawa
 
Hamtowe hiyo pesa ajambie wapi? Hata ingekuwa ni millioni 100 hana uwezo huo.

Hana mapenz na mume wake, angeshindwa kutembeza mabakur kwq mastaa wenzake kama kama kawaida yao na yeye kuongeza hizo mil kadhaa anazohongwa , toka mwaka juz had leo walah angefikish hata nusu akaendela ku fight ,maana kwa umalaya wa kajal angewez ku make plus misaad ya wat mbali mbali,sema ye hana huo mpango
 
Hivi hua wanatoa hizo milion 200 kabisa kabisa au??? Kajala fanya mambo ila akikukimbiaa msoto utaupataa

tatizo ni kuwa K akimtoa jama atataka waendelee kuishi nae maana ashasema bado ni mke wake na anampenda ..na hiyo itaamanisha zile trip za China..na vimchempuko basiiiiiii tena...sasa si atakufa njaa kama mama Ubaya
 
tatizo ni kuwa K akimtoa jama atataka waendelee kuishi nae maana ashasema bado ni mke wake na anampenda ..na hiyo itaamanisha zile trip za China..na vimchempuko basiiiiiii tena...sasa si atakufa njaa kama mama Ubaya

Oooh upo sawaaaa
 
Back
Top Bottom