The last don
JF-Expert Member
- Aug 3, 2011
- 1,053
- 1,232
Mi nafua lakini sijawahi hata kujiuliza hayo maswali kama ni "lazima, hiari au wajibu"
Ila naona raha sana kufua boxer za hubby...na yeye naona anaona raha kuona always boxers ni safi yeye anachagua tu avae ipi.
Suala la kusafiri na kuchanganya kuwa mfuaji hayupo...nadhani linaongeza sababu za yeye kuni miss. Lol. Maana hajazoea ati kufua mwenyewe na inabidi afue sasa. Utasikia 'naona shida sana kuwa mbali na wewe' kumbe ni mchanganyiko wa mengi kuanzia mambo ya 6X6 na 'other services'
Nimefurahia sana mchango wako dada yangu na Komandoo wa ukweli King'asti!!
Katika familia, kuna vitu ambavyo mmoja wenu anavifanya vizuri sana kiasi kwamba inakuwa kama vile ni jukumu lake la kudumu....Ila hilo halina maana kwamba mara moja moja mwenzake hawezi kufanya..
Halafu kuna kazi ambazo zimekaa kidumu dume au kike kike....haya pia tunayafanya sana. Ila haina maana kwamba familia nyingine haziwezi kuwa na utaratibu tofauti...
Kitu ambacho Da Pretty amekataa kutueleza ni kama ameburutwa kwa mateke, mangumi na vichwa kufua kufuli za mzee...Which I suspect might be the case!!
Ndo maana wenzenu tunaimba kila siku kwamba ndoa ni raha sana...Na wazee wanatambua kuwa, mara bibi akipigwa RIP basi safari ya babu nayo imekamilika (and vice versa)!!
Babu DC!!
Mimi wangu atafua suruali, mashati yangu lkn kufuri zake hawezi, mie ndo hurekebisha miaka yote hii ya ndoa, anaona raha sana nikifua so maisha yanaendelea!!
Hahaha, babu najua hukutegemea jibu hili from me. Mie najua kulea babu, japo bhange zinanivuruga kichwa. Namfulia vyupi, namuosha miguu, I clean the bedroom myself, napika (strange eeh?) Ila sera za ki-beijing ni mwake mwake! Hujauza mbuzi before I approve or else...,
I used to tell my mom, let me do everything for you ili nikiondoka hapa kwako uliee! Well, nililia mie na kuona gap. So nikiwa sipo I am miss-able,lol
Hahahha mkuu umetisha
Unajua Ndoa ni vile nyie mnaishi, usifuate sana sijui mwanaume anatakiwa awekwewe maji ya moto asubuhi, wewe miaka yote mtakayoishi wewe unawekewa maji tu si unamtesa mtoto wa watu bure. Mimi km nna nafasi namwekea mamsap wangu maji nenda kaoge, nikikuta taulo lake sijui linazagaa zagaa naliwekwa kwa omo nafua, room sijui wife hajarudi iko na vumbi napiga usafi kote, akirudi anafurahi akicheka mwenzie naanzisha mchezo, tukitoka hapo hakuna sijui mume wangu leo nimechoka! nisipokuwepo home saa mbili ntapigiwa simu mpaka nichanganyikiwe, wife na yeye anajiona ana mume. sasa wewe kariri tu eti mke wahi kutoka kazini, kaniwekee maji, akufulie kila kitu, room yenu adeki yeye, watoto wako akutunzie, yaani chaos zoooooooooooooooooooooooooooooooote yeye afanye, ndio maana humu utasikia mtu analalamika oooh wife siku hizi hanipi mchezo kila nikiomba eti kachoka, kweli mnawachosha, vile vikazi vidogo vidogo vinachosha kwa kweli. ANGALIZO na nyie akina mama mmeo km anakusaidia namna hiyo sio ndo umlazimishe, mwache afanye anapojisikia hapo heshima itakuwepo.
Huu uzi umenifanya nifurahi sana na kujihisi kama Babu wa Ukweli!!
Utaachaje kufurahi baada ya kusoma post za kuguza hisia kutoka kwa watu special kama King'asti na nyumba kubwa??
Nimeona hapo juu hata ndugu yangu The Boss katoa standing ovation kwa nyumba kubwa!!
Babu DC!!
Nipo Mkuu!!!
Unajua nini mkuu...Ukisoma baadhi ya post za wadau na kufuatilia kwa muda...hutashangaa kukuta kwamba wanapinga baadhi ya mambo (wengine wanaita ya mfumo dume) halafu baadaye wanakuja kuyapigia upatu kupitia kwenye thread nyingine!
Utakuta baadhi wanapinga sifa za mwanamume au mwanamke wa Kiafrika ila ikitokea thread ambayo mwanamume analia lia au mwanamke kaonesha ujeuri, wanakuwa mstari wa mbele kumkomalia ili awe kwenye maadili ya Kiafrika...
Yaani ni raha sana kusoma hizi nyuzi..
Babu DC!!
Ubarikiwe sana Kamanda na huyo mdao wako anayepigiwa deki na kufuliwa nguo amebarikiwa pia!!
Wenzio hatufui kabisa....ila siyo kwa sababu hatuwapendi sana wadau wetu!!
Babu DC!!
kumbe na wewe umewaona?
mimi huwa napata burudani sana
kuna threads mtu anavyoshambuliwa wakati
'mafunzo tunayatoa kila siku' na somo hawaelewi labda lol
Mi sijaoa ila mabinti ambao nakua na mahusiano nao nawatengenezea mazoea ya kufua
nguo zangu zote na hivyo sijawahi fua toka 2005 sasa kama nikioa sijui huyo nitakae muoa
atafua au atakua longolongo na hapo ndoa itakua shakani kutokana na mazoea