Unajua Ndoa ni vile nyie mnaishi, usifuate sana sijui mwanaume anatakiwa awekwewe maji ya moto asubuhi, wewe miaka yote mtakayoishi wewe unawekewa maji tu si unamtesa mtoto wa watu bure. Mimi km nna nafasi namwekea mamsap wangu maji nenda kaoge, nikikuta taulo lake sijui linazagaa zagaa naliwekwa kwa omo nafua, room sijui wife hajarudi iko na vumbi napiga usafi kote, akirudi anafurahi akicheka mwenzie naanzisha mchezo, tukitoka hapo hakuna sijui mume wangu leo nimechoka! nisipokuwepo home saa mbili ntapigiwa simu mpaka nichanganyikiwe, wife na yeye anajiona ana mume. sasa wewe kariri tu eti mke wahi kutoka kazini, kaniwekee maji, akufulie kila kitu, room yenu adeki yeye, watoto wako akutunzie, yaani chaos zoooooooooooooooooooooooooooooooote yeye afanye, ndio maana humu utasikia mtu analalamika oooh wife siku hizi hanipi mchezo kila nikiomba eti kachoka, kweli mnawachosha, vile vikazi vidogo vidogo vinachosha kwa kweli. ANGALIZO na nyie akina mama mmeo km anakusaidia namna hiyo sio ndo umlazimishe, mwache afanye anapojisikia hapo heshima itakuwepo.