Mume kutaka kuua mke kisa jeans ya mtumba ya elfu 3, kweli ndo tulipofikia?

Mume kutaka kuua mke kisa jeans ya mtumba ya elfu 3, kweli ndo tulipofikia?

Ukikisoma vizuri hiki kisa utabaini ni tabia ya muda mrefu ya mke kujichukulia maamuzi ambayo hayamfurahishi mmewake.
 
Nguo ni kitu kingine kabisa ambacho kimebeba nguvu kiroho (Jasho na thamani yako).

Mpe mwanao nguo hiyo au mkeo aivae ila sio mtu mwingine.

Ukitaka kumpa mwingine basi kamnunulie dukani umpe.

Watu wanafungwa kupitia nguo.
Kuna mtu niliwahi kumpa nguo na tulikuwa tunaishi naye nyumba moja. Hatukuwa na undugu bali ni rafiki ndugu. Nilimpatia hiyo mara baada ya mimi kutaka kuitupa na akaiomba, nikampa. Toka alipoiomba sikuona ameivaa, wala sikuwahi kuiona tena ila tu majanga yakaanza kuniporomokea. Ikabidi niingie vitani (Maombi na kutafuta kujinasua). Ndio pona yangu, mizigo yote ikarudi kwa ndugu rafiki. Hadi nilimuhirumia.

Kiukweli, nguo ulioivaa mpe mtu ambaye bado hajaijua/haijui dunia. I mean mtoto yatima au kichaa/mwehu.
__________________

Ila huyo wa kupiga mke kafika mbali japo kuna wanawake ni vichwa ngumu, kuta hapo kaulizwa tu kidogo yeye akaanza kupayuka. Tusiegemee upande mmoja.

Kuna mwanamke unakuta huna hata huna shida ya kumuadhibu ila sasa yeye anazidi kukupandisha vibe unajikuta ushamchoresha chips shavuni. 😀
 
Mimi sijatetea tabia ya kugawa vitu vya mtu bila ruhsa yake , Bali hata kama ndio kagawa , ndo umpige mangumi, mateke na kutaka kumpiga na chuma, si alitaka kuua!?.

Hiyo nguo alimgawia mtoto wa dada yake, siku huyo mtoto kaja kaivaa ndo akaiona mume kupanick.
 
Back
Top Bottom