Mume wa jinsi hii........kama mke utavumilia kweli?


kuna haja ya kujua kabila lake..

Kama ni kabila hilo ninalodhani,avumilie tu... Hawarekebishiki...
 
Jamaa hana tatizo, hiyo ni haina ya personality (Haiba) ya MSONDANI (Introvert)
tena iliyolala kwenye extreme (-ve)! inabidi amzowee tu!
ila pia ni tabya ya Wadada/wamama kutaka waishi kama
marafiki/ndugu/majirani zao!
TTHERE IS NO YARDSTICK FOR THAT!
 
Ni kweli lizzy huyo dada inawezekana hamtoshelezi mumewe na si ajabu ukakuta ana nyumba ndogo ambayo inakatisha kiu yake!
 
kuna haja ya kujua kabila lake..

Kama ni kabila hilo ninalodhani,avumilie tu... Hawarekebishiki...


............mhhhh kabila gani hilo hawarekebishiki? Hebu sema basi hilo kabila unalodhani kabla ya kukutajia.
 

Tatizo hapa ni kwamba unatuelezea ni tabia gani mume wa dada huyu alizo nazo bila kutuambia ni kwa sababu gani anazo hizo tabia, kwa hiyo kitu pekee tunachoweza kufanya sasa ni kufanya guesswork bila kuwa na maarifa ya kutosha ili uwezekano wa hii guesswork kuwa sahihi uwe kubwa. Utuambie basi: je, ni nani mume wake anajibu anapoulizwa ni kwa sababu gani anabaki garini au kwa sababu gani hataki kwenda mkusanyiko wowote? Ni udhuru gani hasa anaotoa?
Watu wengi wanali-focus tatizo la tendo la ndoa kutofanyika na kuona kama matatizo mengine hayana umuhimu wo wote, lakini matatizo madogo yote yatajwayo yanastahili kuchunguzwa kwa umakini maana inawezekana yote ni matokeo ya tatizo jingine kubwa. Methalan, naweza ku-conclude kwamba labda matatizo ya pili na ya tatu ni matokeo ya yeye kutotaka kuonekana hadharani na mke wake kwa sababu moja au nyingine, sababu inayoweza kuwa kwamba kuna kitu ambacho hapendi kuhusu mwonekano wake, kitu kinachompa aibu, lakini hataki kuwa wazi kwake kwa hofu ya kumdharau. Hata tendo la ndoa kutofanyika anavyotaka mke inge-support hiyo hypothesis ya kwamba tatizo inahusu (mvuto wa) mwonekano.
Sisemi hii ndio sababu lakini, ni mfano tu kuonyesha kwa nini nafikiri factors zote hupaswa kuzingatiwa, hata zile zionekanazo kutokuwa muhimu.

.......jamaa kabadilika baada ya kuoana, enzi za uchumba walikuwa wanatoka wote out. Inawezekana alikuwa anajitahidi kufanya hivyo ili ampate mwanamke.


Finally, in response to wanaodhani introversion ni sehemu ya personality yake basi ni bora mke avumilie maana haiwezi kubadilishwa, sikubali kwa sababu kama ingekuwa personality yake, nadhani asingalibadilika ghafla baada ya ndoa (isipokuwa amepatwa na maradhi fulani, trauma n.k.). Inawezekana katika pindi yote walimokuwa wana-date alikuwa anajifanya mtu ambaye si yeye ili kumpata mwanamke, lakini hiyo nayo ni improbable (isipokuwa hawaku-date kwa muda mrefu wa kutosha na kuoa bila kufahamiana vizuri vya kutosha as a result).
 

Hapo nilipokuwekea nyekundu, ndio matatizo ya wanawake wengi ambao wanashindwa kujituma.

Msiwalee watoto zenu wa kike wakawa tegemezi kwa wanaume. Kama huyo mwanamke kabweteka na kutegemea kila kitu kwa mwanamme ndiyo inabidi aishi nae.

Isitoshe, hayo mengine yote sio muhimu, wengine raha zao wakiona wake zao wanasifiwa na watu wengine.

Kuhusu sexuality ya mwanamme ni mwanamke ambae ana majukumu ya kujuwa mbinu za kumfanya mumewe awe anatamani, kama hajui mbinu anaweza kumkosa. Kuna mambo ambayo anaweza kuwa anayafanya huyo mwanamke yanayomnyima raha mumewe na huyo mwanamke hajui au hataki kubadilika.

Kuanzia namna ya kuongea, kuvaa, manukato unayotumia, namna unavyojipamba, namna unavyomhudumia mumeo, namna unavyo "demand" kutoka, sehemu unazopenda wewe kwenda yeye hazipendi.

Aanze kubadilika yeye kabla hajaanza kujaribu kumbadilisha mumewe. Ni rahisi sana kujibadilisha kuliko kumbadili mtu mwingine.
 
Sasa wewe ukipata mwanaume ambaye anavyote hivyo ambavyo huyo hana,alafu hana hata kimoja ambacho huyo anacho utamvumilia?yaani mwanaume ambaye hajali matatizo yako,ukivaa ukipendeza anakusifu tuu japo hajachangia hata gharama ya kifungo cha hilo vazi lako,mwanaume ambaye kila dakika network inasoma yaani hata ukiwa jikoni anataka mambo,ukikohoa anataka mambo,kwenye sherehe yeyote ile hata iwe kitchen party anataka kwenda na wewe,huyo unamuonaje atakufaa???

 

Huyo dada anataka mapenzi ya kichuochuo? What is out na dinner? Yuko tayari kwenye ndoa, atulie na kulea watoto.
 
Pole
 
Na huyo Mdada ni wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…