Mume wa kunistiri uko wapi jamani?

Dah...safi sana..hapa mshana jr ..mzizimkavu..na wanatunguli wengine wote out...ushindani utakuwa mdogo sana..nicheki PM inbox yako...nimekutumia CV yangu ya kurasa 23..tena kwa kiingereza 🙂
 
Baby Anka, nimeguswa sana na uliloliandika hapa! busara za hali ya juu, dalili za ucha mungu, subra na hekma zilizokujaa. Hakika kila penye uzito kuna wepesi (Rejea Qur an 94:5). Kuusadikisha ukweli kwamba hutaki zinaa na ukawa tayari kuwaruhusu walioshindwa sharti hilo waende ni ujasiri wa hali ya juu na ni dalili njema ya kuwa wewe utakuwa mke bora kabisa.

Umesema elimu yako ni ndogo lakini nakuthibitishia kwamba uelewa wako ni mkubwa, umeelewa na kufaham kwamba sisi wanaume haturidhishwi tu na ngono, na wote ambao wameachana na wewe kwa kuwa hukuwa tayar kufanya nao ngono (my thoughts) hawakuwa wema kwako. Mimi ni mwanamme pia na sio kama ni mtakatifu hapana! mimi nimewahi kuzini na najua ni namna gani sisi wanaume tulivyo linapokuja suala la ngono. Kwa hiyo ndugu yangu baki na msimamo wako huo huo na Mola wako ataikidhi haja yako.

Ni kweli wengi ambao tabia zetu ni njema na tunahofia zinaa mara nyingi tufikapo miaka 25-28 tunakuwa tumeshaoa kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo, hivyo basi ikiwa atatokea kijana mwenye tabia njema na ukaridhishwa na dini yake basi usijali kwamba utaingia kwenye ndoa ya mitala. Kama wewe ni muislam unaeijua dini yako naamini hilo halitakuwa tatizo.

Acha nisiongee sana lakini nkipata wakati ntakuandikia ninayotamani nkuandikie PM

Angalia (Qur an 2:200) Allah anasema " Enyi ambao mmeamini, fanyeni subra na mvumilie na muwe imara na mcheni Mwenyezi mungu ili mpate kufaulu.

Kila la kheri ndugu yangu
 
Ungeweka na kapicha ingependeza zaidi.
 
mhh kazi kweli kweli-haya walio mitandaoni wakawa wana sifa hizi wajitokezeee
 
Amiin
InshaAllah
 
Inategemea na MTU sio wote wana tabia mbaya,kwa MTU mwenye hofu ya Mungu sio rahis kufanya mambo mabaya yanayomchukiza Mungu
 
Jamani dunia ina Mambo. Umetembea na Wangapi? Ndo unataka sasa wa kuja kumalizia makombo? Tafuta kene hio listi yako mama sisi huku Jf ni wa kuchart tu. Labda tukusaidie kukutongoza tu kama hujatongizwa muda mrefu
Isemee nafsi yako wastaarabu wapo,na wenye nia ya dhat pia wapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…