- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, Maria amekuwa akijihusisha na masuala mbalimbali ya siasa kwa kipindi kirefu sasa, amekuwa akizifanya harakati zake katika mitandao ya kijamii ikiwemo X zamani ikijulikana kama twitter ambapo amejizolea umaarufu mkubwa. Hivi karibuni kumekuwepo na Taarifa mvalimbali zinazohusishwa na yeye ambazo nyingine zimebainika kuwa si za kweli mara baada ya kuletwa na JamiiCheck kutaka kupata uhalisia wake.
Madai
Kumekuwapo na Taarifa zinazosambaa kuanzia tarehe 17/04/2025 zikieleza kuwa mume wa Maria Sarungi amekamatwa na kilo 150 za unga (madawa ya Kulevya) huko China. Taarifa hiyo imeambatanishwa na grafiki zinazozofanania na grafiki ya chomba cha habari cha Mwananchi na MillardAyo. Tazama hapa
Uhalisisa wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia kwa kina madai hayo na kubaini kuwa hayana msingi wowote wa uhalisia hivyo si ya kweli. JamiiCheck imefanya ufuatiliaji kwa njia ya maneno muhimu yaani ‘Keyword Search’ na kubaini kuwa Taarifa hiyo haijachapishwa na chombo chochote cha kuaminika. Matokeo yaliyoloyeletwa yameonesha taarifa hiyo imechapishwa na watu wa kawaida bila kuweka vyanzo vya kuaminika.
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao na google reverse image search, JamiiCheck imebaini kuwa grafiki zilizotumika hazijachapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya vyombo hivyo vya habari yaani Mwananchi pamoja na MillardAyo.
Aidha Maria Sarungi amekanusha madai hayo kupitia ukurasa wake wa X na kubainisha kuwa madai hayo kuhusu mumewe hayana ukweli wowote. Tazama hapa