Phobia
JF-Expert Member
- Mar 29, 2021
- 1,156
- 1,819
Mume wa mtu miaka 5 hataki kunioa nimapata MWANAUME mwinagine naye ni mume wa mtu!
Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 5 na tuna mtoto mmoja. Ni mwanaume ambaye ananihudumia kwa kila kitu, ananijali na sijawahi kukutana na mke wake, hata sijui kama ananifahamu kwani huyu mwanaume ana masharti sana. Hata kwenye kupiga simu, ni mpaka yeye anipigie; hata kama nina shida gani, nikimpigia au kutuma meseji, anakasirika na anaweza kuninunia hata kwa miezi sita. Kwa hiyo, nimeshajua nafasi yangu.
Kinachonikera ni kwamba yeye ni mwanaume mwenye wivu sana, ananichunga hadi kuweka watu kunifuatilia. Amenipangishia na ananihudumia kwa kila kitu ila hataki nifanye kazi au hata kutoka nje. Sasa kuna mwanaume mwingine nimekutana naye mtandaoni, tumekuwa tukichat kwa muda mrefu kama wapenzi.
Kuna kipindi nilienda kusalimia kwetu na nikapata nafasi ya kuonana naye, tukaanzisha mahusiano. Nilimuambia kuwa mimi nina mtoto na yeye akaniambia kuwa ana watoto wawili wako na mama yao na wameshaachana, hivyo akaniambia anataka kunioa.
Anataka kuja kwetu mwezi wa 11 na nilishamkubali, lakini katika kufuatilia kwenye watu wanaomfuata Instagram, nikaona picha yake imepostiwa na mwanamke, na nikagundua kuwa huyu mwanaume ana mke tena ndoa ya Kanisani.
Nilimuuliza akakubali kuwa ni kweli, lakini anataka kunioa mke wa pili. Sijui nifanyeje, anaonyesha kuwa yuko siriasi na mimi, na nawaza nimkubali niachane na huyu mwingine au nifanye nini. Nimechoka kuishi mwenyewe, natamani kuwa na familia yangu!