Mume wa ndoa akikujibu hivi utajisikiaje?

Bi dentamol

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
1,018
Reaction score
2,130
Una mume mnaishi pamoja kama mwaka hivi, hamjabahatika kupata mtoto. Tangu umeolewa jamaa amekuwa mzito sana kukuhudumia na akitokea amekuhudumia, ni mpaka kumetokea ugomvi mkubwa.

Yeye anachojua ni kuhemea chakula ndani tu.

Unavyojaribu kumuuliza mbona mimi hanihudumii anajibu "Nilisoma kwa ajili ya ndugu zangu tu, na ninatafuta pesa kwa ajili ya ndugu zangu tu"

Je, kama wewe ni mke utajisikiaje, na utachukuwa maamuzi gani?
 
Binafsi nakusanya kilichochangu kama tabia ni sugu na hana dalili ya kujirekebisha wala siagi natembea na bwana yann kujikera nafsi

Heri uishi pekeako ila kwa raha kuliko kuishi na mtu ila ni kwenye kero, manyayaso,maudhi
 
Ila kina mama huwa mna uvumilivu mkubwa sana aisee. Hivi mtu hadi anakujibu hivi unasubiri nini tena akwambie ili ujue hamna ndoa hapo?

Alisoma kwa ajili ya ndugu zake tu dah!

Hivi raha ya kuolewa ni ile kuvaa shela na kulala kitanda kimoja na mwanaume bila woga au ni ile tu watu wakiona waseme Lady in action kaolewa bwana, ana mume. Hizi ndio maana pekee za kuolewa hivi? Mbona hapo hakuna hata maana moja ya kuolewa?
 
Alisoma kwa ajili ya ndg zake, hapo ni kuchakarika kutafuta zako ili ujihudumie na uhudumie ndg zako, mimi binamu yangu kaoa muda kidogo, wifi akawa analalamika hasaidii ndg zangu, kuja kulalamika kwa mama yangu, na kufunguliwa akili wewe upo home umekaa tu toa cherehani yako upinde kanga upate hela usaidie ndg zako. Hadi saiz ndg zake wakija anawasaidia fresh tu haya mambo ya kumtegemea mwanaume binafsi siyawezi.

FANYA MPANGO WA KUTAFUTA PESA YAKO, USIMTEGEME
 
Huyo mume ana kazi ya kuajiriwa au biashara ya kueleweka au anapata pesa kwa deiwaka za hapa na pale?
Kwa sababu wakati mwingine unaweza ukamlaumu mtu kumbe tatizo ni kipato chake hakigawanyiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiwango Cha chini ambacho anaweza pata ni 2m icho nikiwango Cha chini
 
Hapa watu watatoa hukumu kwa ushahidi wa upande mmoja tu.
Anaweza kuonewa mumueo kimakosa.
Huenda kuna tatizo upande wako pia zaidi ya kutopata watoto. Hilo la watoto shida yawezekana ipo kwa mumeo.
Mlete mumeo JF nae aje ajitetee kwanini anafanya mambo ya kitoto na kishamba kama hayo.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…