Mume wangu amenitenga baada ya kupinga manyanyaso ya ndugu zake

Natamani nizungumze lakini nahisi nitapigwa BAN,ngoja hasira ziishe kwanza!
 
Nina dadangu mwongeaji sana...alikuwa anatuambia ana suggest vyeti vya ndoa viwe vinaandika vigezo na masharti ya kila ndoa...hiyo ingesaidia kuamua kama bado unataka kuolewa au kuoa. Hasa kuhusu mila hizi ambazo ni ngumu kwa watu ambao wanatoka kabila tofauti. Mtu aseme ataishi ki western au mkewe lazima aishi migombani kwenye cheti kabisaaaa.

Hili ni tatizo si kwetu tu...juzi nilipata muda wa kupiga story na kaka wa ki Nigeria.
Akanambia next year anaenda kwao kuoa. Nikaanza kumpiga maswali maana nawajua sana thru movies nilitaka kujua kama ni acting au ndivyo walivyo

Nikamuuliza;
Mimi: Wewe ni Yoruba au Igbo
Yeye: Yoruba
Mimi: Wife to be ni Yoruba au Igbo
Yeye: Siwezi kuoa Igbo...wazazi wanaweza hata kuni disown
Mimi: why
Yeye: We are quit different, tunaamini Igbo women wanaua waume zao kwa sababu ya mali using witchcrafts.
Mimi: NA wewe unaamini hivyo au ni wazazi na wazee wa ki Yoruba.
Yeye: SI suala la imani; hiyo ni fact.
Mimi: Kwa hiyo ntakuwa right nikisema ni mara elfu uoe mtanzania kuliko Mnigeria wa kabila lingine kama Igbo
Yeye: Mara laki, ila na penyewe kuna ugumu wake
Mimi: Upi?
Yeye: Unajua sisi wanaigeria kwa ujumla hasa Yoruba tuna utamaduni wa extended families na hatuishi kwenye nuklia families; ndugu zangu hawata feel welcomed kama nina mke ambae si Yoruba.

Well tuliongea mengi mpaka tabia yao ya show off kama za kufanya shoping za Harusi majuu...na yeye akakiri kuwa ameshaenda ku shop na wife. Na kunambia kuwa ndoa kwao ni very costly kwani hakuna cha michango and yet still mwanaume anapaswa agharimie kuanzia kwa mkewe mpaka sherehe yake mwenyewe.

Nilichojifunza ni kuwa tuwe makini sana na uchaguzi wa wenza wa maisha. Kama mtu ni wa kabila lingine (kama mimi na mume wangu) make sure wazazi wake wana ka u western otherwise maisha yanaweza kuwa ni ya majuto na mateso.

Uamuzi ni wako dada...huyo mwanaume ambaye number one kwake ni ndugu zake...sioni kama ni mume enough...ingawa ni ngumu kumesa.
 
Nakushauri wasome Kongosho na gfsonwin vizuri afu fanyia kazi ushauri wao. Mwanamke wa sasa anatakiwa awe jasiri na siyo anaelialia kama wa zamani.
 
Last edited by a moderator:
Nakushauri wasome Kongosho na gfsonwin vizuri afu fanyia kazi ushauri wao. Mwanamke wa sasa anatakiwa awe jasiri na siyo anaelialia kama wa zamani.

jmani lkn ukweli Asprin kuna wababa zaid ya kisamvu cha kopo hana anachojli kwa mwanamke. inasikitisha sana.
 
Last edited by a moderator:
unajua mijanaume ambayo nyumba zao zimeshikwa na mama zao huwa wanasumbua sana....

kama unaweza kutunza watoto wako shida ya nini? ondoka...

ukishindwa kuondoka, as long as hamlali pamoja, piga moyo konde, inabidi uwe imara haswa, kinachompa kiburi huyo mwanaume ni kumjali, pia kulia lia kwako ndiko kunawapa kiburi wanajua unaumia.....sasa wewe mpotezee mazima, yaani ishi kama hayupo, ishi as if awepo asiwepo, akuhudumie asikuhudumie wala haikuumizi na wala hujali..........
in short ishi maisha yako acha kusumbua kichwa kwa ajili ya huyo mwanaume, wewe muombee tu Mungu ambadilishe mapema kabla hajajuta, maana hajui thamani ya lichonacho mpaka akipoteze....
 
huyu binti story zake huwa sizielewi kabisa, sijui alikulia kwenye friji??


Pamoja na machungu yake bado huwa namuona hazitoshi hivi au anaishi kwenye kisiwa kuwa yeye hana ndugu hata mmoja??

Ngoja niondoke hapa nitachafua hali ya hewa bure wakati ni mzazi huyu.

Nakushauri wasome Kongosho na gfsonwin vizuri afu fanyia kazi ushauri wao. Mwanamke wa sasa anatakiwa awe jasiri na siyo anaelialia kama wa zamani.
 
Last edited by a moderator:

unajua Kongosho ndo maana huwa nasemaga nina roho mbaya, yaani kuna wakati sifai kumshauri mtu hasa kwenye jambo kama hili. hakya Mungu angeondoka yeye humo ndani kwani huwez kumfungia vioo? kaa nyumbani mwako stail iwe ya dont see me. bize na kazi zako akitaka atafute pa kweda na siku akikusemesha moto ndo uwake uwwiiiiiiiiiiii

yaani miye nilifanya mtu hadi aka hire private investigator alihisi nitamwua kwa mchuno niliopiga bize na wanangu yeye akawa kama fenicha tu ndani na akaumia zaid kaleta kahaba nikawa ngangari sikulia tmekula kila mtu 50 zake ikawaka taa ya njano kwenye fahamu zake na hivi huyu ni mpalestina hakya Mungu ataniua hawez akawa binadam. kumbe nilitaka kumuonyeshe mimi nikisha ingia ndani sitoki labda kwa kifo na manyanyaso huko huko ndani huwez manake sikuombi hata 100 na msosi natafuta mimi kila kitu. pita nenda kwa rum na kahaba na mimi naenda kwa rum na wanagu manina wakllah mbona alisalim amri.

ukaksi ukaksi tu kama vipi achukue time yeye ila si mimi.
 
Last edited by a moderator:

Wasema nini kaka the Magnificent? Huamini mwanaume anaweza kuwa katili? Hujasikia kile kisa cha mwanaume mmoja huko mkoani mara aliyemburuza mkewe kwenye lami kwa kutumia gari lake?Upo ukatili wa kutisha unaofanywa na baadhi ya wanaume kama huyu mume wa Lonely Heart.
 
umeona eeeh Kongosho, anahitaji Mtambuzi ampe kauseling maana haelewi, toka alivyoambiwa asonge mbele bado yupo tu, hawa ndo wanaoogopa kusonga mbele na kupambana na maisha, wapo radhi wadhalilishwe mtaa mzima wao wapo tu...





 
Last edited by a moderator:
ndugu ninao 2.Tulifunga ndoa ya kiislam
Sasa kinachokushinda kumuacha ni kitu gani? Kama ungekuwa huna ndugu ningesema, lakini kama una ndugu zako wakusaidie ili uweze kumwacha mwanaume huyo mnyanyasaji.
Ninachofahamu mimi ni kwamba uislamu hauna ugumu sana katika talaka, hata mwanamke anaweza kumuacha mumewe kwa talaka, labda kama unashindwa kulipa mahari ya watu ambayo nadhani utadaiwa kwa sababu wewe ndio unayemuacha huyo mwanaume. Vinginevyo mimi nitaamini kwamba huna nia ya dhati ya kuachana na mwanamume huyo mnyanyasaji.............. unalia lia hapa lakini huenda unajua lililo moyoni mwako, na hiyo ni kutokana na kwamba unajua dhahiri kuwa ndugu zake ndio wakorofi na sio mwenzi wako.

Dada chukua maamuzi magumu muache mwanaume huyo......... Jinsi unavyozidi kuneng'eneke hapa ndivyo unavyozidi kuzuia ridhiki zako na kujiwekea ukuta. Kwani hujawahi kuambiwa kwamba mlango mmoja ukifungwa, mwingine uko wazi pembeni yako.

Mwenye enzi Mungu katika aya za Kurani ametueleza wazi kwamba, kila jambo gumu lina wepesi na akasisitiza tena kwa kusema, Hakika kila jambo gumu lina wepesi.

Haiwezekani uuone wepesi ilhali umejitwisha mzigo wa mwanaume mnyanyasaji kichwani. utue kwanza huo mzigo ndipo upate ahueni......................

Sijui nikisaidieje....................!
 
Pole sana. Kuna wanaume wengine wana roho mbaya sana utadhani si binadamu. Pole sana. Kama una mahali pa kwenda bora ufanye hivyo ili kuyakimbia mateso.

 

na kwa nini hao wifi zako wasirudi kijijini kumlea mama yao jipe moyo jikaze na uwe imara wakiona hauteteleki watajirudi wenyewe
 
gfsonwin, huyu binti anashindwa kuelewa kuwa kila mtu ni 'amiri jeshi mkuu' wa roho yake na furaha yake.

Sasa asipojilindwa mwenyewe hakuna atakayemwonea huruma, kazima uweke mpaka wa uvumilivu si kulalamika tu.

Haoni watanzania tumedhamiria hata kupigia SAU 2015? Yeye anashangaa shangaa tu na kulia.

Unaona wee ulivyokomaa sasa hivi isikite mmeo adabu 100%.
 
Last edited by a moderator:

Eti ukaishi wapi? hivi bado kuna wanaume wa jinsi hii, aisee kazi ipo!
 
kwa moyo uliopondeka ukifunga kwa siku 9 kwa maombi Mungu atakujibu, kama ni mkatoliki sali novena siku 9, i believe kabla hujamaliza Mungu atakuwa amekujibu kama una mwamini na kumtumaini yeye pekee
 
Unajua nimesoma mateso unayopata na nimeumia as if wewe ni dadaangu wa tumbo moja. Kama haujadanganya hii stori (of course tunakusikiliza wewe tu) basi kwangu mimi unazo 'guts' za kuondoka kwa mumeo na kwenda kwenu. Ikumbukwe kwenda kwenu kutakupa pumbazo na tulizo la moyo. Na kwa ndugu zako au wazazi wako itawapa picha ya mkwe waliyenaye. Kuanzia hapo mambo ya Talaka yanaweza kufuatia.

Sikushauri mambo ya kung'ang'ania nyumbani kwa mumeo hapo kama walivoshauri wachangaji wengine. Kuna wanaume wengine wanaweza kukupasua kweli. Kama mtu umeshamuona ukatili wake toka una mimba hadi sasa una mtoto..pleeaase epusha msongamano..nenda kwa wazazi au walezi au ndugu zako ukapumue..Kuolewa sio waranti ya kuteswa bwana!
 
Nimejikuta nacheka.


 

Kwa hiyo unalala wapi na mtoto?..banda la uani ama??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…