lolyz, pole sana mamii
tutakupa ushauri kibao hapa,mwisho wa siku ukweli unabaki pale pale,muamuzi wa mwisho ni ww. hakuna kitu kinachoudhi kama kumuona mwenzio anataka kukuharibia ndoto zako. kimbiza ndoto zako. kuna kitu kinaitwa tough love. kaa nae,ongea nae umpe feelings zako na umuambie jinsi ambavyo tabia zake zinavyokuathiri ww na watoto. muambie unamuachia jukumu la kuweka maisha yake sawa,ila akuambie ww unaweza kumpa msaada gani ili ajikwamue kwenye hiyo adha ya ulevi.muulize kama anayafurahia hayo maisha yake,na kwamba utaheshimu uamuzi wake isipokuwa itakulazimu ww uchukue hatua juu ya maisha yako mwenyewe.mueleze uko tayari kum-support awe mtu wa kuheshimika zaidi nyumbani na kwenye jamii pia,kwa sababu unampenda na unataka kumlinda. angalia atakachokujibu.chochote atakachokujibu,mkubalie. mind ur business, akirudi late usigombane nae wala kumuuliza ametoka wapi.mpokee kwa furaha,ila hakikisha hatumii hata shilingi yako moja.huo ugali anaokula hapo kwako hautakutia umaskini,ila endelea na mipango yako ya maendeleo muache aendeleze show zake. mwisho wa siku,inakulazimu umtoe moyoni mwako ili usiumie. ukiona unaumia bado hata baada ya kum-ignore,inabidi uchukue hatua ya kumuacha kwa kipindi. inabidi mkubaliane bila kugombana,kwa sababu itawaathiri watoto. mengine baada ya hapo unavuka daraja utakapokutana nalo. endelea kumuombea,ukali kupita kiasi utaendelea kumkimbiza. ukimya unaweza kuwa suluhisho,japokuwa mara moja moja unatakiwa kuwasha moto ajue ww sio mjinga.