Mume wangu hataki msamaha wangu

Kuna siku mlilala njaa? Kuna siku alishindwa kutimiza mahitaji ya home? Achana na simu
 
Kwa ufupi tu huyo hakupendi ashakuchoka kuna mtu kaichukua nafasi yako kwa kipindi kile ambacho haukuwepo mapenzi yamehamia kwa aliyekuwa anamhudumia wakati wewe ukiwa mjamzito.

Mkuu wewe ndo muhusika nini?[emoji16]
 
Chanzo nini sasa?? Kwa maana hakuna ugonvi usii na chanzo

Ila apo kwenye rungu 🤣🤣😂😂😧
 
Hiyo nayo ndoa au upo uwanja wa vita? Kwanza kwann ujifungue uambiwe uende kijijini? Asee anayekuhudumia aje mjini period
 
Afu chumbani kuna lungu na sime [emoji23][emoji23][emoji23]
Cc[mention]Everglow [/mention]
Kipenzi njoo uone vitu vyakuweka chumban kwetu
 
"chumbani kuna rungu na sime"..aisee nimecheka sana japo hili swala sio la kucheka.

Pole sana dada..
 
Ni kweli kwamba kuna muda unatakiwa kujishusha, lkn hii hapana, Msamaha umemwomba kwa kosa lipi?

Unatakiwa kukomaa na kumweleza wazi kuwa unaona mabadiliko katika mahusiano yenu, usikubali kuwa kondoo wa Kafarq, kosa analo na unatakiwa wewe ndiye wa kuyanusu hayo mahusiano.

Ukilemaa umepoteza huyu jamaa, wanawake wa nje wanatumia weakness zenu kumiliki waume zenu. KOMAAA USIJISHUSHE KIFALA!!
 
Ndoa kama vile tupo Kabul Afghanstan..sio kweli.

Sisi ambao hatujaoa tukiona hii mikasa tunajawa na wasiwasi sana na ishu ya ndoa.
 
nakushauri uondoke hapo kwake kwa muda,

kama wewe na mwanao mna umuhimu kwake

atakuja kwa magoti!

nakushauri usiombe msamaha, maana hujamkosea chechote

ondoka hapo, hata wiki haitoisha atakufata.
 
Step ya kwanza katoe rungu na sime chumbani alafu urudi tukuambie cha kufanya!
 
Kwa ufupi tu huyo hakupendi ashakuchoka kuna mtu kaichukua nafasi yako kwa kipindi kile ambacho haukuwepo mapenzi yamehamia kwa aliyekuwa anamhudumia wakati wewe ukiwa mjamzito.
mkuu unaweza kuta maneno yako yamefanya mtu ajinyonge huko
 
nakushauri uondoke hapo kwake kwa muda,

kama wewe na mwanao mna umuhimu kwake

atakuja kwa magoti!

nakushauri usiombe msamaha, maana hujamkosea chechote

ondoka hapo, hata wiki haitoisha atakufata.
Kwanini aondoke bila ruhusa ya mumewe,hawezi kuondoka na akiondoka kienyeji mwanaume anaweza kusema kuwa mke katoroka

Msamaha ni lazima aombe,maana yeye ndie aliyepokonya simu ya mumewe

Halafu ndoa si malumbano,usione ndoa zinadumu,bali bila mmoja kujishusha ndani ya nyumba inakuwa shida


Ndoa si jambo jepesi kama mnavyofikiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…