Mume wangu mtarajiwa ni mwanaume katili

Status
Not open for further replies.
Nitajaribu kufanya hivyo dear.[emoji120]
Halafu Mungu akitoa kibali cha ndoa nitamuomba Mr. aniruhusu tulete mtoto mwingine wa kiume ili wawe wawili mana nahisi hii kucheza na huyu pacha wake wa kike kila mara labda sio nzuri sana.

sio mbaya mana wamelala kwenye tumbo moja na wamekua pamoja ila muwaelekeze hao watoto wajue mipaka ya kila mmoja mwa mwenzie wa kike ajue kua huyo ni kaka ake same kwa wakike[emoji4][emoji4] pia msiwaringanishe wala wasijiringanishe au kufananishwa kwa chochote kila mtoto ana namna yake ya kukua sio kiakili tuu
 
Sijui mkuu.
Mimi babu yangu alikua anatuchakaza mbaya mbovu, akikushika anakucharaza bakora na ngumi zipo ila ajabu ni kua hakuwahi kumpiga mkewe hata kofi tu.

Bibi nae alikua anatuambia hilo kua mumewe pamoja na ukorofi na ukali wake woote lakini hakuwahi kumgusa hata kidogo. Sijui ni mila maana hata mkamwana wake hakuwahi kumfokea wala kumuagiza chochote.

Labda asemayo ni kweli mkuu, ila jaribu pia kufatilia historia yake.
 
Hali inaogopesha mwenzangu
 
Kwa nin wanasema wewe ni mwanaume,
Binafsi sijapata kiunganishi chochote Cha kuona wwe ni mwanaume
Mwenzangu acha tu😂.
Juzi kati nilirusha uzi wa kuwasema mashoga na matapeli wa kiume wenye ID za kike na pia nikaelezea jins hizo ID zinatumika kuibia watu.
Kabla ya ule uzi sikuwa nashambuliwa wala kuitwa mwanaume😂😬😃🤣😆.

Inshort wamenigeuzia kibao🤣.
Ni wana hasira balaa ila mimi hata hainisumbui kuitwa mwanaume.
Na mwenye hasira sana na mim ni mmoja ila ananijia kwa sura tofauti tofauti🤣😆😃😬😂.
Fuatilia vizur huu uzi utagungua kitu dear😂😬😃😆🤣
 
Mwenyewe pia anadai hajawahi na wala hawezi kupiga mwanamke.Anadai aliongea vile sbb ya hasira tu.
 
Nimempenda sana babu yako mkuu🙏🙏.
Mungu ampe yeye na bibi maisha marefu🙏🙏
 
Ni kweli dear ila naona umuhimu wa kiume wawe wawili.

Huyo wa kike akifananishwa na kaka yake anavyonuna sasa🤣.Anasema hana masikio makubwa kama ya kaka yake🤣.

Asante kwa ushauri dear🙏
 
Daah!
Uzuri nampenda siwezi kuchepuka
Huyo huwezi kumuacha. Nakumbuka Dada yangu aliolewa na jamaa ambae alikuwa akimpiga mara kwa mara na Dada alikuwa akirudi Nyumbani kwa kukimbia vipigo na wazazi walikuwa wanamrudisha kwa mume wake.

Baada ya mwaka mmoja Dada alishindwana nae wakaachana. Cha ajabu na mtu mwingine aliekuja kumuoa nae anatabia za kitemi kama zile za yule alieachana nae.

Hivyo nilichogundua ni kwamba kuna uhusiano wa moyo wako na aina ya watu unaowapenda. Si ajabu ukipata mwanaume mpole unaweza ukamkinai mapema tu.
 
Dizaini kama Chai 🍵 🍵🍵
 
Duuh!
Ni kweli napenda mwanaume mkali asiyependa ujinga ila naogopa kipigo.
 
K
kwa hasira za namna hiyo hapana kwa kweli maana anaweza kuua mtu
 
Wanaogopa sheria mkuu. Japo hata mimi siwezi kumpiga mwanamke na sijawahi kumuona baba yangu akimpiga mama.
binafsi, mwanamke akinyoosha mkono juu yangu, there is no guarantee kwamba hatakutana na ngumi tena nzito. hata hivyo, najizuia kwa kumwogopa Mungu tu ila sioni ajabu.
 
binafsi, mwanamke akinyoosha mkono juu yangu, there is no guarantee kwamba hatakutana na ngumi tena nzito. hata hivyo, najizuia kwa kumwogopa Mungu tu ila sioni ajabu.
Hapo yeye kwenye kuanza kunyoosha mkono kwangu anaweza kujikuta yupo pale wodini mwaisela aisee.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…