Kumbe ungeyajua usingeolewa? Unaiongeza hofu yangu. Yaani sitaki kumwingiza mtu yeyote katika mazingira ya majuto maana itaniweka kwenye guilt kila siku. Je akitokea anayeridhika kuolewa na mimi nimwambie ukweli kuwa nilishakuwa na 5 girlfriends na mmoja wao ni outspoken HIV/AIDS activist aliyetangaza HIV positive status yake hadharani, na tena yuko very popular in the media siku hizi? Nisiposema akija kugundua atasema 'najuta'! Nikisema, hata suala la "tukapime kwanza" hatalitilia maanani, ataogopa unyanyapaa.
Halafu nyie wanawake ndio mnatufanya tuwe na ma-ex wengi. Mi katika exes wangu 5, ni mmoja tu nilimtamkia mimi kumuacha. Wengine walinipotezea kiaina kufuata "opportunities" na mimi sikuwa na hiyana maana mapenzi ni hiyari, na waliporudi na hadithi tofauti walikuta nimefunga milango isipokuwa ya urafiki wa kawaida au hata kunaniliu occasionally walipokuwa hawajaolewa but strictly no strings attached. Sasa leo nikioa bado nina historia ya rundo la exes, ambao nyie akina Mom na Nyamayao hamtaki hata tusalimiane nao!