Ok just a question to you and Sipo, ukioa na ukakaa vizuri tu na mkeo ukazaa watoto saba, ukafa watoto hao wanalelewa na nani? wajane wanaitwa nini? au mnadhani single parent ni CD? ndo maana nawaambia usi discriminate watu na ku assume ndo sababu ya failure
je umeishasikia wasiosoma ukioa wana taabu, waliotoka kabila hili, waliotoka familia maskini/tajiri ni hivi? Ndo maana nakwambia usibebe sifa za familia yako kwenye ndoa ACT yourself!
Mjane sio 'single mother', tafadhali sana kwa hili, usitutukanie mama zetu. Mjane ni mjane, mwanamke mwadilifu aliyeolewa akaishi na mumewe hadi siku kifo kilipowatenganisha. Watoto wa mama kama huyo sio kama wa single mother, ni watu wenye kumbukumbu ya malezi ya baba yao, na hata wao na mama yao huwa wanamkumbuka baba yao huyo.
'Single mother' ni kitu ingine kabisa, ukimuuliza mwanae babako yuko wapi, usishangae ukajibiwa 'simjui'! Lakini mtoto wa mama mjane ukimuuliza atakujibu kuwa baba alifariki. Sababu ya mjane kulea watoto bila baba ni kuwa huyo mumewe alifariki, lakini kwa single mother ni kuwa huyo mume hajawahi kuwapo!
Kujibu swali lako, nikioa na kuzaa watoto 7 kisha nikafa, mke wangu hatakuwa 'single mother', atakuwa mjane. Na watoto wangu nitakuwa nimeshirikiana na mke wangu kuwalea hadi siku hiyo nitakapokuwa nimekufa, na hata kama yule wa 7 atakuwa mdogo, wale wakubwa zake watakuwa wamepata muda na baba yao si haba, na watamweleza mdogo wao kuwa baba alikuwepo akafariki, mama yao sio single mother ni mtu mwenye heshima zake.
Kumwita mjane 'single mother' ni tusi lisilovumilika. Single mothers ni watu waliochagua aina hiyo ya maisha wakati wanawake wenzao walipoamua kuwa watazaa katika ndoa. Matokeo ya uchaguzi huo ndiyo tunayojadili hapa. Yaani mie kwa kifupi kuhusu suala la kuoa binti wa single mother, jibu langu ni moja tu: SIDANGANYIKI.